JK akizungumza na wakurugenzi watendaji wa mitandao ya simu za mikononi za Zain, Zantel na Tigo. kutoka kushoto ni bwana Nabil Tofilis wa Zantel, Pablo Guardia Vasquez wa Tigo na Khaled Muhtadi wa Zain Ikulu leo
February 18, 2009: Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wamebeba waya (fibre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar kwa ajili ya kutoa huduma ya network nchini. Toka kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba akifuatiwa na Meneja Mkurugenzi Anna Rupia na kushoto ni Eng. Jon Avery. Habari hiyo kamili inapatikana hapo


---------------------------------------------------

Tushirikiane kujenga Mkongo wa Taifa,

Rais Kikwete ayaambia makampuni ya simu


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ya Teknolojia ya Kompyuta – National Fibre Optic – unaojengwa nchini utakuwa na shabaha kuu ya kusukuma mbele maendeleo ya taifa.


Aidha, Rais Kikwete ameelekeza Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kukaa chini na makampuni binafsi ya simu nchini na kuangalia jinsi pande hizo zinavyoweza kushirikiana katika ujenzi wa mkongo huo utakaokuwa na urefu wa kilomita 7,000 ukisambaza mtandao wake katika nchi nzima.


Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumanne, Juni 23, 2009 wakati alipokutana na kuzungumza na viongozi wa makampuni ya simu ya Tigo, Zantel na Zain, Ikulu, mjini Dar Es Salaam.


Rais Kikwete amesema Serikali yake inataka kuyashirikisha makampuni hayo katika ujenzi wa mkongo huo badala ya kila kampuni kufikiria kujenga njia yake yenyewe kwa sababu mkongo huo ni kwa manufaa ya pande zote.


Ujumbe huo ulionana na Rais Kikwete kumweleza nia ya makampuni hayo kutaka kushirikiana na Serikali katika ujenzi huo baada ya makampuni hayo kusita kwa muda mrefu kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa mkongo huo.


Mkongo huo unalenga unalenga kuiwezesha teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta kutumika kikamilifu na kwa ufanisi zaidi kwa maendeleo ya taifa.


"Yalikuwa maelekezo yangu na nia yangu tokea mwanzo kushirikisha wadau wote katika ujenzi wa mkongo huo kwa nia ya kupunguza mzigo kwa kila upande kwa sababu mkongo huo utatumiwa na sisi sote," amesema Rais na kuongeza:


"Hayo ndiyo yalikuwa maelekezo yangu kwa Wizara husika, lakini naona awali nyie mlisita kushirikiana na Serikali katika hili," amesisitiza Rais na kuongeza:


"Lakini sasa maadamu mko tayari basi kaeni chini ya wizara husika na kuangalia jinsi ya kukamilisha ujenzi wa mkongo huo."


Mkongo huo unatarajiwa kugharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 170. Serikali imeamua kuzikopa fedha hizo kutoka China ambayo imekubali kutoa mkopo huo.


Rais amewasisitizia viongozi hao wa simu za mkononi kuwa ni muhimu kwa Serikali kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa mkongo huo kwa sababu Serikali inataka mkongo huo utumike kwa ajili ya maendeleo ya taifa na siyo kwa ajili ya faida tu.


"Tunataka mkongo huu utumike katika kuboresha huduma za elimu, huduma za afya, shughuli za utalii katika kila ncha ya nchi yetu, katika mikoa yote, iwe mijini ama vijijini.


Kwetu sisi ni wajibu wa kitaifa kwa sababu kwa Serikali nia yake kubwa ya kujenga mkongo huu ni kuhakikisha unatumika kwa maendeleo ya nchi." amesema JK.

--------------------------------

picha na habari zaidi kwa kiinglishi

BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2009

    Naomba kumnukuu Gado 'tunajenga mkondo wakati umeme hakuna' hiyo teknolojia ndio inahitajika ila angalau tuanzie na tatizo na umeme likifuatiwa na maji

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2009

    duh, mzee njumba uko juu! nikirudi lazma nikutafuta babaangu!...........

    ReplyDelete
  3. Michuzi,

    Mimi Magazeti-Patrick Nhigula nimefanya kazi kwenye Kampuni hapa South Carolina, Columbia kama Senior Network Analyst kwa miaka kumi sasa katika kampuni ya Spirit Telecom. Kazi yangu ni utaalamu juu ya mambo ya technologia ya Frame Relay, ATM, SONET. Technologia hii Rais anaongelea inahitaji investment ya hali ya juu sana na serikali lazima iwe na wataalamu watakao tengeneza sheria ya simu na mawasiliano. Tanzania inahitaji kwanza kuwa na kampuni za simu zinazohitwa "Independent Telephone company" kwa mfano, Kinondoni Telephone company, hii kampuni itakuwa inatoa huduma ya simu na services kwa maeneo ya kinondoni tuu", na shirika hili litaunganishwa na shirika la simu kubwa kama TTCL. Mfano, TTCL au shirika kubwa linajenga mtandao wa kuziunganisha mashirika madogo madogo ambayo yanatoa huduma kwenye mawilaya,tarafa, na mikoani. Mashirika madogo yanapeleka huduma kwenye mabiashara na makazi ya wananchi. Mashirika madogo ya simu ya nunua huduma kwa mashirika makubwa. Sasa lazima kila wilaya tena lazima wawe na Fiber optic kampuni ambayo inafanya biashara na shirika dogo wilayani,tarafani, na mkoani. Lazima mashirika yaungane na kushirikiana kukata gharama za operation. Kama Wanataka technical and operational consultation tuwasiliane tupo tayari kutuo maoni.Patrick. Nhigula@bcbssc.com
    Fungua hii link utaniona niko kazi.
    http://www.spirittelecom.com/index.php?option=com_content&task=view&id=45&Itemid=1034

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2009

    WADAU SAMAHANI SANA NAOMBA MNIELIMISHE MKONGO MAANA YAKE NINI?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2009

    Hi Michu, I'm a Telecom expert here in Tanzania, I just want to give a brief introduction of optic fiber communication.
    First Digital optical fiber communication system consists of optical transmitter, optical fibers and optical receiver, from Hierarchical point of view, the optical transmission network is generally divided into three layers: access layer,convergence layer and core layer. the access layer implements the access of subscribers of different types, the convergence layer converges the disperse access points; and multiplexes, transmits and exchange data;it provides the function of traffice control and subscriber management. The core layer exchange the high-speed information of the whole network and interconnect with the backbone network.
    In the initial stage of network construction, the convergence layer and the core layer can be combined based on the network scale, to form a two-layer structure of access layer and convergence layer.

    Advantages of Optical Fiber Communication:
    1. Broad transmission band and large communication capacity.
    2. Low attenuation and long distance transmission
    3. High adaptability
    4. Abundant raw material resources and saving non-ferrous metals.

    Thanks

    Mdau Dar
    email: agngowi@gmail.com

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2009

    sijaelewa nielimishwe me lay person

    na ule mkonga wa kenya je??juzi apa BBC akiongea waziri odinga kwamba kenya sasa itaweza saidia mawasiliano nchi kadhaa na tanzania aliitaja,kwamba kenya ndo CENTRE

    sasa lipi ni lipi?ni vitu 2 tofauti au ndo masheuzi ya majirani zetu??je mikonga inafanana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2009

    Mbona wakuu wa hayo makampuni wote ni wageni? Hivi hakuna wabongo wenye uwezo wa kuongoza hayo makampuni?

    Wabongo kila leo wanamaliza MBA. So mkazitumie hizo MBA zenu kuongoza haya makampuni?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2009

    mh jamani ni mkongo au mkonga? naomba kuelimishwa hapa wadau.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 24, 2009

    We anon wa 1:11 pm hebu kuwa na subira kidogo, kwani hujui kuwa haya makampuni(Zain,Tigo na Zantel) ni multinationals? kwa mfano Zantel pale Kampuni ya Etisalat ya uarabuni wanamiliki 51% of shares, na ndio financer wa miradi yote hapo, sasa haya jamaa lazima wataleta watu wao ili kulinda maslahi yao, kumbuka Telecom projects zinainvolve pesa nyingi sana, kwa mfano kaka unataka kupata full coverage ya Tanzania, unahitaji si chini ya dola million 300, kwa kuanzia, hivyo mtu awezi akaweka pesa nyingi kiasi hiki halafu akuweke mmatumbi eti kwa sababu una MBA, hata wewe Mtanzania ukiwekeza nje kiasi kama hiki basi lazima utamuweka shemejie ili akulindie mali kaka,

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 24, 2009

    yan annon apo juu hadi nshachoka kuongea naishia kutikisa kichwa tu

    ivi izi kazi wabongo wooote tuliosoma ivi why thiz opportunities to be directors ktk izi makampuni hawapewi wabongo??watu wana mashule na maprofesheno na maexperiences ya kazi lakini ikija bongo,no m-bongo

    ebu ona iyo aibu rais kakaa na wageni/wakoloni eti ndo CEOs wetu

    ndo mana watu wanaishia kubeba box na kutorudi bongo,bora mtu ajifie ukouko...

    nyambafu

    ReplyDelete
  11. Magazeti-PatrickJune 25, 2009

    Ngowi,

    Mimi ninaona unaongelea academic tupu, mimi nimefanya kazi kwenye kampuni ya simu hapa Marekani, South Carolina. Tuna kampuni ya Fiber optic huku zinaitwa interexchange carrier, na tuna kampuni inayounganisha au kuuza DS3, OC3, NA T1. Tunapata light za Fiber kutoka kampuni yetu ya Fiber optic. Kufanikisha mkonga au Mkongo huu ni lazima yaanzishwe makapuni ya simu mikoani na wilayani yatakayo shirikiana interconnection and long-haul. Hii siyo kama unachukua mkopo leo na unaanza biashara kesho. Vile vile, kuna gharama za application na software management za kuangalia carrier switches na dark fiber.Mimi ninaona lazima research study lazima wanafunzi na wanachuo local wafanye na "right way" na sheria zitungwe kabla ya kurukia mambo. Kama serikali inakopa 176 Million huu mkopo utalipwa vipi..D3, T1 voice and DATA CIRCUITS siyo bei rahisi kama watu wanavyosema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...