Kwa mara ya kwanza nchini Ujerumani, waafrika hususani wale wa pwani ya Afrika Mashariki, watakuwa na Summer party la nguvu itakayofanyika ndani ya meli (pichani), katika mji wa Dusseldorf ambao ni makao makuu ya jimbo la North Rhine Westphalia.

Akizungumza na glob ya jamii kwa njia ya simu, muandaaji wa sherehe hizo, Shekale Bwana Kelly ambaye ni mkurugenzi wa kampuni inayoshughulika na burudani na vyakula, PAPA AFRICA, amesema kuwa sherehe hizo zitafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 18 mwezi Julai, ambapo watakaofanyikiwa kununua tiketi wataingia ndani saa moja mjini Dusseldorf hadi siku ya pili yake, ambapo meli hiyo itakwenda katika miji mingine kama vile Cologne, Bonn na Koblenz.

Ndani ya meli hiyo kutakuwa na sehemu mbili za burudani, moja kwa ajili ya vijana na nyingine ambayo ni chini ni kwa wale wazee wa zamani yaani old skull, hapo kutapigwa zile nyimbo za enzi hizo.Pia kutakuwa na bendi itakayokuwa ikitumbuiza usiku kucha, huku watu wakila raha na pia kutavukizwa udi ili kupata ladha halisi ya pwani.

Mbali ya hivyo Kelly pia amesema kutakuwa na burudani ya chakacha itakayooneshwa na mabinti kutoka Mombasa, pamoja na Samba itakayooneshwa na wasichana kutoka Brazil.

Amesema watu wote watatakiwa kuvaa nguo nyeupe, ikiwa ni ishara ya amani, kuionesha dunia hususani watu wa Ulaya kuwa Afrika na haswa Afrika Mashariki ni watu wa amani.


Kelly ambaye ni maarufu nchini Ujerumani kwa kuandaa matamasha makali, amesema kuwa kiingilio kwa maana tiketi ya kuingia ndani ya meli hiyo ya kifahari ni euro 20 na kwamba chakula ambacho kitakuwa ni cha pwani kitauzwa.

Tayari sherehe hiyo ya ndani ya meli ambayo itakuwa na ladha ya kimwambao imekwishakuwa gumzo katika eneo hilo la Ujerumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2009

    Hii kitu mbona inafanyika kila mwaka hapo Minnesota

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2009

    taratibuni hayo maudi na maharufu ya pombe katikati ya bahari,
    msije rudi nusu kiroba!
    kila la kheir!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2009

    dj nani????mbona ujasema au kade wa kade....haaaaaaaaaa..sawa ujerumani.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2009

    Kutakua na Heineken?Lazima mtu aokotwe kwenye maji.Wabongo na Heineken check yangu macho

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2009

    nawapa hi sana masela wote kule munich, kiel, magdeburg, konstanz karibu na uswisi, dussedolf, frankfurt,hohenheim, achen nakazalika, bigup wakubwa hasa mnaosoma hapo ujerumani manake shule ya mabwana hao si masihara iko juu kishenzi ingawa dunia haitaki kutambua ukisoma kwa mfano economics au econometrics ujerumani kama si mzembe basi utakuwa aluwatani wa uchumi au econometrics na unaweza kufundisha popote duniani. c ya

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2009

    chakacha na mabinti wa"jirani zetu"
    mabinti wa samba ya brazil


    afu iweje??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...