wadau wameomba taswira hii kujikumbusha tulikotoka, ambapo safari ilikuwa inachukua hata siku tatu endao kama kuna mvua. siku hizi iwe jua iwe mvua mwendo mdundo tu maana barabara ya nyanda za juu kusini lami hadi itungi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2009

    Da hakika enzi ya Mwalim kwelikweli maana nakumbuka kitambo hicho kulala porini hadi barabara ikauke ilikua ni jambo la kawaida kabisa. Kitu cha Leyland mkubwa, maharage maharage hivi,, dah walale pema peponi wale wote waliotangulia!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2009

    hii kweli ilikua enzi ya UJAMAA watu walikua wamechoka, barabara zimechoka hata mabasi yamechoka.MUNGU atusaidie tusirudi huko tena.

    ReplyDelete
  3. Nyerere kawatesa kweli Watanzania kwa sera zake za UJAMAA. Thanks to former Pres.Ally Hassan Mwinyi kwa freedom uliyowapa Watanzania. God bless you, and all people of great nation of Tanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2009

    Mithupu ama kweli umenikumbusha mbali saaana.Hapo mahala kama sikosei ni Mafinga au Iringa kwa hiyo miti yake.Watoto wa juzi wanafikiri Nyerere alitutesa lakini sisi ulikuwa una safiri kwa WARRANT ukiwa mwanafunzi kwenda sehemu YOYOTE nchini Tanzania.Mtu ukiwa mwanafunzi hasa wa sekondari kulikuwepo heshima kubwa.
    Hayo mabasi ya RAB yalianza zamani lakini nakumbuka RAB 502,503,504,505, 506 na hilo kwenye picha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2009

    daaa michu mimi ni mama wa watoto wawili 9yrs,4yrs.enzi za hilo bus nilikuwa na miaka 9 mimi na mama yangu,wadogo zangu tulikuwa kila likizo ya mama tunatoka mwanza tunaweka kituo kwa mama yetu mkubwa maogomeni mapipa then safari ya iringa kwa kupanda basi hilo nakumbuka repotingi taim ilikuwa jioni na safari ilikuwa jioni daaa tumetoka mbali

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2009

    hahaha hii nadhani ni pale kwetu Ilula-Isele{Itunda} kwa Mwakulanga likiokea Image hureeee miaka alufu ulela ulela enzi za mchaka mchaka asubuhi na mwenge ulee siyo huu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2009

    hawa wote wamekumbuka, ila wamesahau kitu kimoja..kusafiri na unga,mboga na sufuria ilikuwa jambo la kawaida.zaidi ya hapo hakuna haja hata ya kusema kuwa nyerere(R.I.P) alifanyanini wabongo,inapasa wakumbuke kuwa Enzi hizo kuwa na basi tu ilikuwa ni jambo lilikuwa limeendelea,itafikia wakati,kukiwa na subway,hata hao akina Mwinyi,Likapa,JK wataonekana kuwa hakuna kitu,kwani kila kipindi na mambo yake.barabara Zote zilikuwa za vumbi,ukisafiri hukawii kuaga familia,hujui utafika lini ,au salama,maana lol..! hamkawii kufika njiani,abiria mkashuka ili msaidie kuweka sawa barabara,ila yote maisha.mambo ya kupakatwa kutoka Dar hadi Iringa mbona ilikuwa kawaida tu kwa sisi watoto.(kama vile mwendo wa third Class kwenye relwe ya kati,kama wote mpoa national services viel.angalia pia mfano zamani kulikuwa na UDA(kuingia kwenye basi ni kwa mlango wa nyuma tu-usinisome vibaya) hapa Dar,sasa kuna uchafu wa vijidaladala,ghafla sasa ni vibajaji hukawii kusikia tuna baiskeli kibao hapa DAR.wakati watu wanaelekea huko mawinguni kwa maendeleo.

    Akihito

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2009

    ...nyela kubooma ipoo...

    maisha yalikua so peaceful zamani,upendo,utu,kujali nk

    sio sasa!!

    asante balozi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2009

    Du! Umemkuna sana mdau wa Isimani hapo, Mkuu! Enzi hizo foleni kuubwa mashine ya Kusaga Unga, ambayo ipo kama km 10 kutoka chamdindi!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2009

    kwa kweli misupu taswira hii imenikumbusha mbali sana. mabasi yalikuwa yakisafiri kuanzia saa 12 jioni na kuendelea ngoma usiku kucha inaunguruma.enzi hizo mabasi yalikuwa ni aina moja tu, Leyland albion ama british.basi lipo segera wewe mtu wa hare makinyumbi , unalisikilizia kwenye lami, yalikuwa yanajua kulalamika kwa sauti ya juu na hasa gia inapoingia!! ilikuwa starehe bwana!! ukikaa kiti cha mbele ndio kabisa usingeweza kuwasiliana na mwenzio kwa kelele zake.
    Hongera kwa taswira nzuri sana. umetukumbusha mbali.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2009

    Ule usemi wa kawia ufike, hapo ndio mahala pake, kwa kweli wakati huo walijipanga.EAR kwani kila walipofika ktk vituo vyao waliwapeleka abiria kula, bus linaenda ktk ukaguzi,asante mchonga! anaesema katubana nasema tatizo lake ni UPEO! alitupeleka kutokana na wakati kaka!!Enzi hizo tulikua tuna kula buruga mchana, maziwa asubuhi, wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2009

    Leyland CD ilikuwaq inalalamika vizuri sana hasa kwenye mlima.Ilikuwa inatia raha sana.
    Mdau Orange County.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 29, 2009

    Machozi yanalengalenga kwa nostalgia. NAKUMBUKA pale mzee Simon Makwaia akitukatia tiketi kwa shillingi kama themanini hivi (1984) halafu unapanda basi mpaka Iringa. Asubuhi unafika unapanda basi kuelekea Tosamaganga baada ya chai pale 'hoteli' ya msomali stendi ya Iringa.

    Hongera sana bto. Michuzi tungeyapata wapi mambo haya, duuuuh!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 29, 2009

    anony wa pili na mchangiaji wa tatu hapo juu, manonyesha elimu ilivyowapita pembeni. someni nyakati na mtafumbuliwa macho. kabla ya nyerere babazenu walikuwa wanatembea kwa miguu. ni Juhudi za mzee wetu NYERERE,kuwepo mabasi hayo. someni hisitoria ya tanzania na dunia walkati huo. mabadiriko muonayo duniani ni ya siku hizi. INDIA BASI HIZO BADO ZIPO SANA, nao wamlaumu mahatma.
    AMA KWELI SHULE MUHIMU.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2009

    DUU MICHUZI UMETOKA MBALI, HAPO KABLA UJAKUWA CHIEF PHOTOGRAPHER HAPO YMCA ULIKUWA UNAPIGA DEBE KWENYE MABASI HAYO, KUMBUKUMBU ZANGU NILIKUWA NAKUONA SANA STESHENI. NAOMBA UWAAMBIE VIJANA MAISHA KUTAFUTA MAANA SASA HIVI HATA SERIKALI INAKUTAMBUA.WAKO BOBO CHURA

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2009

    Wakati huo walikuwa wakishindana na mabasi kama "Kwacha" na baadaye "Kiswele"

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2009

    Mnaomlaumu Nyerere yawezekana mlisafiri kwa waranti kwenye haya mabasi. Wengine wenu mmeweza kuandika ujumbe wenu humu kwa sababu mlisomeshwa bure. Mnachekelea yaliyotokea baada ya enzi za Mwalimu na kusahau kwamba shirika la Relwe ndio hilo hilo linaitwa TRL enzi hizi. Wawekezaji wa kidosi wamewawekeza kweli kweli manake wananchi mnaendelea kulipia gharama za kuendesha shirika wakati wao wanafanya kazi ya kukomba cha juu tu. Maendeleo hayaji kwa siku moja na hatuna sababu ya kuchekelea kuacha kupanda Leyland CD na kuanza kupanda Scania Marco Polo wakati si Leyland wala Scania iliyoundwa nchini.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2009

    Ulietaja Ismani hapo umenikumbusha mbali foleni ya kusaga Nyang`oro mashine ya Mwarabu Brek.

    Watu walitoka vijiji vya mbali kwenda kusaga kwani hakukuwa nasehemu yoyote ambayo unaweza kusaga zaidi ya hapo kama mashine ya kijiji ikiharibika. Nakama hakurudi ndo tunarudi makwetu hadi kesho yake tunaenda kusubiria tena bila mafanikio.

    Hapo tunasubiri kaenda Iringa town kununua spare ya mashine wakati huo ndo kulikuwa na bus linaitwa Lupembe lilikuwa linalala kijiji cha Kihorogota.

    Kwama wengine walivyosema kila kipindi kina mambo yake tusikashfu walotangulia. Hakuna mtu aliekamilika. Tumetoka mbali sana.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2009

    Wanyjucha Enzi za Mwalimu Owaitu tukaba twine ebasi Ya BUDEKO,Rehemturah,Kagera Tetco,Chipukizi,Vicror Na Byonabushai,kazabaire ziruka Bukoba Zemerera Kyaka,Kayanga ,Omurushaka,Nkwenda mwisho Kaisho

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 30, 2009

    tatizo wengi walio toa maoni wakamlaumu Mchonga inaonekana ni wa toto na wasio na uchambuzi tosha wa maswala.

    Kipindi hcho haya mabasi yalikuwa hot cake. technology imebadilika na ndio sasa mnapanda mabasi ya raha na ya kasi haya hayakuwepo nyakati hizo sio tu tanzania bali hata nchi nyingine. ni jambo la kipumbavu ku kurupuka na kumlaumu Mwalimu bila kuwa na uelewa. Kumbukeni barabara na magari haya ni jitihada za kujikwamua toka katika hali mbaya aliyotuacha nayo mkoloni. Je Nyerere angelifanya nini kubadilisha kila kitu over night?

    Pamoja na hayo nakumbuka nilikuwa nikisafiri toka Moshi mjini kwenda Rombo Tarakea wakati shule zilifungwa ama kufunguliwa, ili upate usafiri basi inabidi usakanye basi mitaani ijapo kulikuwepo na stend nzuri tu pale moshi mjini. Enzi zangu nakumbuka nilipanda mabasi ya Albion ambayo gia namba moja ikiingizwa basi kila mtu anakwenda mbele na nyuma. gear stick yenyewe iibidi konda amshikilie dereva kwa jinsi ilivyokuwa inayumba toka upande mmoja kwenda mwingine. Steling yake ilikuwa kubwa kiasi kwamba kama dereva alikuwa hajala vyema basi ni kukuru kakara patashika nguo kuchanika. Ilikuwa ni kawaida kusimama safari nzima toka moshi mjini hadi rombo ambayo inachukua zaidi ya masaa nane. Cha ajabu tulikuwa tunadunda hivyohivyo, tena usisahau kama mvua imenyesha basi kazi kwenu kusukuma gari likinasa.


    Cha kushangaza hapakuwa na wa kulaumu wala wa kulalamika. sote tulikuwa Happy.
    NAfikiri yote haya yalikuwa poa kwani hapakuwepo na cha kulinganishia na tulimshukuru Mungu kwa kilichokuwepo
    eleweni basi

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 30, 2009

    duuu wewe wa ILULA ISELE MIMI NILIKUWA NAENDA ILULU PALE LUGANGA KWA BIBI YANGU MUHAME.DAA BASI LETU LA RELWE MWEEEE NGURUVI HEBU TURUDISHE ENZI YA MABASI YA IMAGE(MTATIFIKORO),COMFORT (MWANYATO)
    DA ILULA YETU WENYEWE

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 30, 2009

    PEDE MUYENU NZIWIKE KUTALII DA PALA PI TUNDA,KUMWAYA,KUSIMA,KU LUGANGA,KU IKUWALA HUKO KOTE TUKASOGWE KUTEGULA AMAHAUSI GELI.

    KAKA MICHUZI HILI BASI WE ACHA TU WEWE MICHUZI UMELIPATA WAPI? AU NA WEWE WA KWI RINGA? MANA KAMA HUKUONDOKA NA RELWE BASI IGESA YA MTATIFIKORO

    HIVI WOTE HAWA WAKOWAPI ? MICHU HEBU TUHABARISHE

    MAANA WAILULA WOTE WALIKUWA HAWAPANDI MABASI MENGINE

    WAO WALISEMA TWISAKA YA MTATIFIKORO WA ILULA MWENZETU

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 30, 2009

    mdau 10:53 am

    alee bela,kubooma kunofu swelaga

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 30, 2009

    Mimi nakumbuka ,kulikuwa na mabasi ya relwe yakiwa na second class viti vya mbele ambapo kulikua na mlango mwingine ukipanda ngazi upande wa kushoto.upande wa nyuma ni daraja la tatu.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 11, 2009

    Mdau wa mwisho hayo yalikuwa ya kwenda Zambia.

    ReplyDelete
  26. naomba mnisaidie jamani nasikia huduma za daladala zamani enzi za mwalimu zilikuwa nzuri kuliko sasa,pia nasikia kulikuwa na mabasi marefu kama haya ninayoyaona huku mamtoni je ni kweli?maana watoto tuliozaliwa juzi hatujui utamu wa mambo enzi za Baba wa Taifa,halafu nasikia shirika vitu vingi vilikuwa vinatengenezwa Bongo badala ya kununua kutoa nje nasikia hata treni ya reli ya kati ilikuwa ni nzuri kweli sawasawa na nchi zilizoendelea kipindi hicho nasikia shilingi ya tanzania ilikuwa sawa na dola 20 ni kweli ,mtusaidie vijana wa siku hizi hatujui.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...