warembo watakaopanda jukwaani leo usiku kwa ajili ya kinyang'anyiro cha kumsaka malkia wa Miss Morogoro 2009 kwenye ukumbi wa Hoteli ya Masuka ya Mjini Morogoro.
WAREMBO 11 wanatarajia kupanda jukwaani leo usiku kwenye ukumbi wa Hoteli ya Masuka village ya kwa ajili ya kinyang’anyiro cha kumpata malkia wa Miss Morogoro 2009.
Mkurugenzi wa Kampuni ya FG arts Promotion, Frank Kikambako , ambao ni waandaaji wa shindano hilo , alisema jana mjini hapa kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika.
Alisema kutokana na ubora wa warembo waliojitokeza mwaka huu ana imani Mkoa wa Morogoro utafanya vizuri katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Tanzania kitakachofanyika baadaye mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, aliwataka warembo wanaotarajia kupanda jukwani kwenye kinyang’anyiro hicho ni Shekha Washokera ( 23) Upendo Paul ( 18),J oyce Peter ( 20), Tory Oscar (21), Frola Florence ( 19) na Lorna George (18.
Wengine katika kinyang’anyiro hicho ni Nicole Denis (19) Jacquline Laizer (21), Upendo Damian ( 19) , Mariam Didi (21) pamoja na mlemavu wa kiziwi Carolyn Emmanuel (21).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, shindano hilo limedhaminiwa kwa pamoja na Kampuni ya simu za mkononi ya VodaCom, Ze Club, B one Lodge na Masuka Village na litasindikizwa kwa burdani za wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kwa Tunda Man, Spark na Madee pamoja na muziki waTaarabu.
Kwa upande wao warembo hao wakizungumzia kwa nyakati tofauti wakiwa kambini kuhusu kinyang’anyiro hicho, walisema shindano hilo ni ngumu kubashiri mshindi kwa kuwa kila mshiriki ana vigezo vinavyojitosheleza kuibua mshindi.
uncle michuzi mbona miss dodoma hatuwaoni..........?????????tuwekee mapicha hayo basiiiii
ReplyDeletehayo mambo ya miss miss inaboa kweli, hao wadhamini kama wanauwezo wa kuandaa mambo kama hayo kila siku kwa nini hizo hela wasisaidie mahospitali hasa za wazazi hii imeshakuwa too much
ReplyDeleteanyway na jua waosha vinywa mtasema sana, nchi umeme wa mgao maji maeneo mengine hamna usalama mdogo kwa wananchi ajira kwa vijana nichache then misssssssss every where around the country
Mwenye nywele natural anyoshe mkono.
ReplyDeleteduh...mbona hata mmoja hana nywele za kiasili...au kuona aibu wa uswahili!!!
ReplyDeleteOld McDonald had a farm, e i e i o
ReplyDeleteAnd on the farm he had a Miss, e i e i o
Like Miss, Miss, Miss
Miss here, Miss there, everywhere Miss ...
mwaka huu morogoro ikipata hata mmoja kwenye kumi bora nitashangaa sana.!!! utadhani wanapulizia moto!!!
ReplyDeletehaya mtaalam wa pajazzz uko wapi au hujainasa hii bado!!!
mbona sijaona anayefaa hapo.
ReplyDeletewaruguru typical!!! miguuni viazi ka' mkude au mogela!! morogoro mmeanza ubaguzi wa kikabila?? si mnge-consida na makabila mengine wajameni???
ReplyDeletemh nisiinase!!!! nimeinasa sana tu,. mi nisipoingia michuzi globu usingizi ntaupata???? sema morogoro wamekuwa biased kidogo!!! wameshindwa kuniteka kabsaaaa!! bado nina hang-over ya miss EU. ule mdatisho kwakweli utachukuwa muda kunitoka kichwani. still in mission incomplete!!!
ReplyDeletemdau wa pajazzzzzzz!