Watani wa jadi wa timu za kandanda za watanzania za scandinavia Fc Bongo ya Finland na Kilimanjaro Fc ya sweden zitakamuana Katika viwanja vya KAPYLA Helsinki leo saa saba mchana kuwania kombe la (TANZANIA CUP SCANDINAVIA).

Mabingwa wa kombe hilo mwaka jana Kilimanjaro Fc wako mtumbwini VIKING LINE kuelekea Helsinki kutetea kombe lao ambalo mwaka jana walilinyakua kimungumungu huko kwao sweden.

Inasemekana kuwa zaidi ya watanzania 200 kutoka sweden wako njiani kuelekea helsinki kushuhudia makamuzi hayo.

Habari kutoka Helsinki zinasema kwamba vijana wa Fc Bongo wako fulu-mziki mwaka huu na wanawasubiri kilimanjaro kwa kiu kali sanaaaaa.
Na FC Bongo wameahidi kutoa pilau yenye nyama na vipapatio baada ya gemu. Habari za ndani toka Helsinki zinadai kwamba baada ya 'babu' kuchungulia imeonekana kwamba hadi mapumziko, Kilimanjaro Fc 0 na Bongo Fc 2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2009

    Mpira umekwisha. Kilimanjaro FC, Sweden wameibamiza FC Bongo, Finland mabao 8 kwa 1.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2009

    vijimambo tu vya kupasha misuli! Na uoga wao kuchezesha kina Machupa na Shekhani Rashidi kwenye match mbuzi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2009

    hatimae tumefanikiwa kufungwa duh noma babake

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2009

    Leo Iikuwa fully kipigoo kwa vijana wa helsinki na hiyoo ndio habarii kaka michizii 8-2 sio machezoo vijana wa sweeden nomaaa...Mdauu KONTULA

    ReplyDelete
  5. speechless....chacha..ezza mambo vipi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2009

    Oya annon wa pili siku nyingine mtapanga list yetu (Kilimanjaro) ili msilalamike au nikikurahisishia sema utasema nani haruhusiwi kucheza kati ya wale waliokuja halafu mambo yatakuwa poa
    Mdau Stockholm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...