Kweli kuishi kwingi kuona mengi! Wimbo Umezua balaa!
Ras Makunja na mkwala wa Mbwa DomoBaya kwa Kizabizabina
Kiongozi wa bendi ya The Ngoma Africa aka FFU, Ebrahim Makunja aka Ras Makunja "Bw.Kichwa Ngumu",juzi juzi amewaacha hoi mainjinia katika studio huko ujerumani baada ya kutinga na mbwa studio humo na kumshirikisha mbwa huyo aitwaye "Domo Baya" katika kurekodi sauti!
Mbwa huyo alibweka sana na kurekodiwa vizuri! katika kuchangia wimbo wa "Kizabi Zabina" na "Mzee Pazi si mtu mwema"
Wadaku wametonya kuwa hatua ya kumpeleka mbwa huyo studio ilichukuliwa kwa hasira na Ras Makunja baada ya mwanamziki huyo kupokea ujumbe wa simu ya kiganjani kutoka kwa mtu asiyejulikana. Simu hiyo ilimuonya Ras Makunja kuwa aachane na wimbo huo. Hapo kamanda wa kikosi cha Ngoma Africa au FFU, uzalendo ulimshinda akaamua kukodisha mbwa aina ya Domo Baya, na kwenda naye studio kuzidisha vitisho!
Baadhi ya wanamziki wake walimsihi kuwa "Ras hapo huoni kuwa unamtishia mbwa kizabi zabina "Mzee Pazi"! Ras Makunja nae alilamika kuwa mbona yeye ananitishia maisha kwa ujumbe wa simu!?.
inaelekea song hilo lenye kutangaziana bifu kati ya Ras Makunja na "Kizabi zabina! ( Mzee Pazi) na kuingia sura mpya kabla halijatolowa hadharani!
Ngoma Africa wamesema Jamii ndio itakayoamua nani mchokozi kati ya Kizabi zabina na mtunzi wa nyimbo hiyo Ras Makunja,ambaye naye mara nyingi analalamikiwa kuwa mchokozi, lakini katika hili jamii ndiyo itakayo toa uamuzi...
Katika songi hilo, Ras Makunja anamkoromea "Kizabi zabina" Mzee pazi na kumwambia atakapokaribia nyumbani basi ajue atafukuzishwa na mbwa "Domo Baya"
Hii kitu haijatulia na it does not make any sense! Kuweni wabunifu na mtunge nyimbo zinazotoa mafunzo kwenye jamii.
ReplyDeleteAchaneni na mambo ya bifu mbuzi mbuzi kama hizi ambazo hazitatufikisha anywhere.
Ras Mnyepe
Ocho Rios, Jamaica
ras Mnyepe wa Jamaica au Jamdown,wenzio hawa kama utawafuatilia sana,utagundua kuwa wametoa mchango mkubwa kwa jamii,kupitia nyimbo zao hapa bongo,na wamekubalika kitaifa na kimataifa!
ReplyDeletesasa wewe usiwaonee wivu au kuwaelekeza nini?wafanye.Unachotakiwa nawe jaribu kutoa mchango wako kwa tanzania.
Sasa huko Jamaika unafanya nini?
Usilete mashindano ya kufuga Rasta kwani kuwa na nywere ndefu haina maana heti ndio una akili nyingi.
Wenzio hawa wameitangaza Tanzania kimziki je?wewe umeshafanya hilo?
Tafuta cha kuongea! acha kutoa maoni pumba.
Any where
Mdau wa Mbezi Beach
hii!kamanda Ras makunja hii kali ya mwaka! unajua tabia za uzabi zabina zimejenga mizizi katika jamii yetu ya wabongo bora unavyotoa onyo, Kama Kizabi zabina akisogerea nyumbani kwako, basi isije kuwa lawama,maana Mbwa Domo Baya! hana msalie
ReplyDeletemtoa maoni Ras Mnyepe,
ReplyDeletehili bifu la Ngoma Africa aka ffu na Kizabizabina waachie wenyewe usije ukayavaa mawe anayorushiwa mdaku kizabizabina
Ras makunja si unaona ulivyokuwa na hasira? mara nyingi wewe ndiye unayeanzaga,lakini hili la leo huyu Kizabizabina kahamua kudeal na wewe,sasa vipi?tena unamtishia Boby!tena mbwa wenye DOMO BAYA.
ReplyDeleteKaka Braza Ras, angalia jinsi ulivyokuwa mkorofi,mambo mengine unayaanza mwenyewe,harafu watu wakikurudishia madongo,unawawekea mkwala?na kuwatangazia hali ya hatari! unajua kumtishia mtu na mbwa wa aina hii ni hatari sana,si bora tu mngekaa mkayaongea na kumaliza mambo
ReplyDeleteKaka Misupu,kwanza asante sana kwa kutuletea hii mechi kati ya Ras Makunja na Kizabizabina,au tuseme
ReplyDeleteBifu la Bw.Kichwa ngumu Vs Kizabizabina,sijui nani? ataibuka na ushindi,inaonyesha huyu kizabizabina anatangaza ubaya ubaya na kamanda wa ffu,na Ras nae anamkwala wa hatari ya mbwa kichaa,tena dog DOMOBAYA,
acha tuone mwisho wake.
ras makunja vipi?mbona mkwala mzito?si mmgehelewana tu,wakati nyinyi wote ni mabingwa wa gubu,japokuwa gubu lako wewe linakwenda na mziki,hila huyo mwenzio ana uzabizabina wa mtaani.
ReplyDeleteNaona Ras...onyo lako kali tena la hatari tupu.
Any way wewe mwenyewe pia mtu akikusikiliza sana nyimbo zako,zinatia uchungu fulani.
Hili bifu lenu sisi wasikilizaji tutatoa uhamuzi nani mshindi
hello! ras makunja wa ffu,hapa umenikosha sana,unajua mimi pia yamenikuta jirani yangu pia kizabizabina,ana shahada ya juu katika sekta ya fitina,ananigombanisha mpaka na maiwaifu wangu,lakini kuanzia leo nitafuga dog kichaa domobaya
ReplyDeletemungu wangu! kamanda wa ffu na mbwa mkali?haaa!! sasa hii ni kali ya mwaka.
ReplyDeleteKizabizabina bora kaa mbali kichaa ana mbwa mkali huyo.
Tueleze, unasema wewe ni maarufu sana,mbona sisi hatukujui wewe ni nani kwanza? tukisoma maoni yako tunaona kua ni wewe mwenye umeandika,utaona dakika za maoni zimefuatana, usifanye mabo ya watoto ras, umaarufu hautafutwi hivyo.
ReplyDeletekizabizabi shughuli unayo kichaa huyo mpaka kijulikane
ReplyDeletekamatieni hapo hapo wachizani msimwachie mdaku huyo,tena akijisogeza mwanadamisheni na bomo baya.
ReplyDeletehuyo Anony,Jun 30,07:06:PM
ReplyDeleteInaelekea umekerwa sana na wimbo wa hawa ngoma afrika "Kizabizabina",maoni yako yanaonyesha kiasi kikubwa sana?ulichomwa na ujumbe wa kutishiwa mbwa.Sasa umesema kuwa ngoma afrika uwajui!au Ras ndiye nani? sasa watu usiowajuwa kwanini?wakuninyime usingizi,ulivyoandika "mbona sisi hatukuji" sisi inamaana wewe na familia yako,na walio wengi wanautambua na kuheshimu mchango wa mwanamziki huyo na ngoma afrika,si jambo baya kwa wewe na familia yako kutowatambua na ulazimishwi kuwajua.
tujaribu kuzingatia onyo kuwa Kizabizabina chunga sana ngoma afrika wanaulinzi wa mbwa kichaa.