Balozi wa Afrika ya Kusini, Mheshimiwa Lindiwe Mabuza, akifungua rasmi sherehe za kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika hapa nchini Uingereza.
Mheshimiwa Balozi wa Botswana, na ambaye ni Mkubwa wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza Bwana Roy Blackbeard, akitoa hotuba katika kuadhimishwa siku ya Afrika hapa Uingereza.

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, Mama Mwanaidi S. Maajar {katikati ya Picha} akiwa pamoja na Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard {kushoto} na Balozi wa Afrika ya Kusini Mama Lindiwe Mabuza {kulia mwa Picha} wakibadilishana mawazo katika kuadhimisha Rasmi siku ya Afrika hapa Uingereza.
Ujumbe wa Tanzania katika kuadhimisha siku ya Afrika hapa Uingereza. Kutoka Kulia ni mwa picha ni Bwana Othman Mashanga, Dada Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, na Bwana Sylvester Ambokile, maofisa wa Ubalozi wa Tanzania.
Baadhi wa Wajumbe na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania hapa Uingereza wakiwa kwenye picha ya pamoja na, Mheshimiwa Balozi wa Tanzania, Mama Mwanaidi Senare Maajar {Kushoto mwa Picha}, Bwana Zahran, Bwana David Maira, Dada Suzan Mzee.

Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza.
Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Blackbelly.
kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Afrika ya Kusini, Mheshimiwa Mama Lindiwe Mabuza, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa nchi za Afrika na wageni mbalimbali waalikwa kwa kuwashukuru na kujumuika kwao na Waafrika wote Duniani katika kuadhimisha rasmi siku hiyo hapa Uingereza.
Upendo, Ushirikiano ,Mshikamano miongoni mwa nchi zote za Afrika, Kufuta Umasikini, kudumisha Amani vilihimizwa sana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2009

    Susan mzee anafanya kazi gani?Chadema mbona hawana mwakilishi wao?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2009

    Susan Lyimo Mzee ni mwenyekiti wa CCM UK na mke wa mwandishi mahiri Ayuob Mzee ambaye pia ana BLOG yake.hiyo Mzee ni jina la mume wake.MR.AYOUB MZEE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2009

    Jamani mbona hii siku hapa USA hatujaishangilia?

    Mchumi wa Texas

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2009

    Ayoub Mzee ni mdau wetu huwa anatuletea mapicha ya ukerewe humu.hongera mr.Ayub mzee ila shemeji yuko busy sana na minuso.mtafutie kazi afanye.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2009

    labda shemeji susan alikuwa anamwakilisha mumewe kwani naona kabeba bonge la kamera utafikiri michuzi enzi za 1990s alipokuwa hana Digital.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2009

    WEWE ANONYMOUS
    1.(June 01, 2009 3:03 AM, Mtoa Maoni)

    2. June 01, 2009 4:28 AM, Mtoa Maoni

    3. (June 01, 2009 2:26 PM) Mtoa aoni,

    4. (June 01, 2009 4:01 PM, Mtoa Maoni)

    a)ANAITWA, SUSAN MZEE (SIO SUSAN/SUZAN LYIMO MZEE.

    b)YEYE NI KATIBU WA TAWI - CCM UINGEREZA na SIO MWENYEKTI(HILO UNALIJUA FIKA, ILA UNALETA UZUSHI).

    c)MUME WAKE ANAITWA, MBARUKU MZEE (SIO AYOUB MZEE) (HILO PIA UNALIJUA LAKINI BADO UNAENDELEZA UZUSHI NA CHUKI BINAFSI).

    d)ANAMWAKILISHA MUMEWE!!!!! WAPI??? "ETI UNAONA KABEBA BONGE LA KAMERA UTAFIKIRI MICHUZI ENZI ZA 1990s ALIPOKUWA HANA DIGITAL"(WEWE UMEIJUAJE HIYO, MBONA KATIKA PICHA HIYO KAMERA HAIONEKANI VIZURI!!!!)
    UNAANDIKA MAONI/MASWALI NAKUJIJIBU MWENYEWE, ACHA MCHEZO WAKO MCHAFU, TUTAKUANIKA HAPA KWENYE HUU MTANDAO WA JAMII HALAFU USHINDWE KUJINASUA, ANYWAY UNAJULIKANA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2009

    hivi hawa wanaosema susan mzee ni mke wa ayoub mzee mbona wamechemsha sana, yeye ni mke wa mbaruku mzee kijana mmoja safi sana. mke tu ndio mbwembwe nyingi mara ccm , sasa naona anataka kuwa katibu wa blog ya jamii maana camera ya michuzi haitoshi kunasa vya ulaya.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 02, 2009

    Susan unakataa nini wakati umeshika bonge la kamera?
    pia umekasirika sana kwenye picha hii au ulilazimishwa kubeba hilo kamera?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 02, 2009

    Susan unataka kutishia watu Nyau?lakini Mr.AYOUB Mzee ana blog jee hizo picha kwanini hazionekani kule kwa Mr?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...