Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara kama ifuatavyo kwa lengo la kujaza nafasi zilizokuwa wazi pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi kwenye Wizara kama ifuatavyo:-

Bwana ELIAKIM CHACHA MASWI - ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI) atakayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kabla ya uteuzi huo, Bwana Maswi alikuwa Kamishna Msaidizi wa Bajeti, Wizara ya Fedha na Uchumi.
Bwana JUMANNE ABDALLAH SAGINI – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI atakayeshughulikia Elimu ya Msingi na Sekondari. Kabla ya uteuzi huu Bwana Sagini alikuwa Mratibu wa Mradi wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Dr. SHAABAN RAMADHANI MWINJAKA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Kabla ya uteuzi huu Dr. Mwinjaka alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Makamu wa Rais.
Bi. ELIZABETH JOKTAN NYAMBIBO – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu Bi. Nyambibo alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
Bwana ULEDI ABBAS MUSSA – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi huu Bwana Mussa alikuwa Mkurugenzi wa Biashara na Uwekezaji kwenye Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dr. PATRICK S. J. J. MAKUNGU – ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Kabla ya uteuzi huu Dr. Makungu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa ‘Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology’, Arusha.

Uteuzi huu unaanza tarehe 13 Juni, 2009.

(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU MKUU KIONGOZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2009

    kishoka wetu ha ha ha teh teh teh teh koh koh koh aaaaaaanha!!! michuzi kweli kazi unayo!!! kwani umelazimishwa????!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2009

    Makungu!!!! jiko lina sebure ya mamsosi ya kienyeji pale laundiabauti ya sua moro jirani na baa ya kambarage!!!! pale mambo yose ni loko utapata sato, mrenda, mtindi, mayaiyakienyeji, majaniyakunde, majaniyamaboga, matembele, choroko, mbaazi, kunde, uduvi, nguruka na mazagazaga yose dagaa nini!!!!!!! mnaona sasa mungu asivyomtupa mja wake, huduma nzuri kwa wananchi. mamsosi ni nachulo ukiyapiga ukashiba ukaingia kazini unaweza kuua!!! goma litakuwa kingi libeneke mpaka moniee ka bomba vile waweza ita polisi. na mlupo wenyewe ka' ndo kuku wa kisasa basi dhahama hatari hatari hatari hatariii!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2009

    Duu! Noma. Ulaji mwingine huo umenipitia kando.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2009

    Hongera homeboy SAGINI kwa kuongezewa majukumu. Wale madent wa Nyamisisi Primary 1982/83 twakumanya ulivyo makini.
    Tumia utaalam wako kuimarisha mfumo wetu wa elimu kwani huu wa sasa tunapoteza muda, pesa na rasilimali watu buree tu.

    Elimu bora kwa kila mtoto inawezekana tutimizeni wajibu.
    Mdau toka Oslo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...