Kikosi kabambe cha TASA United kabla ya gemu. Kunradhi jezi tumeagizia ila bado hazijaja
Stori na Taswirazzz na Jennifer Sumi
Timu ya Jumuia ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma NEW DELHI India na jirani( TASA), jana katika kuungana na watanzania kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu ya wakulima SABA SABA ilipimana nguvu na Timu ya wanafunzi wa watani wa jadi, KENYA, Katika mchezo uliofanyika kwenye kiwanja cha Chuo kikuu cha Delhi, North Campus.
Hata hivyo katika mchezo huo ambao ulichezwa kwenye mazingira magumu ya Jua na Joto KALI la INDIA hasa wakati huu wa majira ya JOTO..SUMMER),wanajumuiya watanzania walijitokeza kwa wengi wakiwemo wa Hydrabad, Jamia Hamdan, na Delhi ya kusini yote ikiwa ni kujumuika pamoja na kubadilishana machache.
Mchezo ulikuwa mgumu huku kila upande ukiwa na kiu ya kuweka rekodi, lakini hata hivyo Wakenya walifanikiwa kuondoka na ushindi wa Mabao 5 -3. Hata hivyo, japo walitufunga chenga tuliwala ile mbaya!
Huu ni uwanja wa soccer au mbio za farasi?
ReplyDeleteNimeamini hivi sasa bongo nguvu mpya hali mpya kandanda mpya sabasaba mpya jezi mpya. kawaida kandanda ilikuwa inachezwa na wachezaji 11 kwa kila timu lkn hali mpya wachezaji ni 9. s/kukuu ya wakulima huwa tarehe 8/8 kila mwaka lkn hali mpya ni tarehe 9/6. jezi za timu huwa sare lkn hali mpya ni papa na nguru
ReplyDeletemdau
kisiju pwani
Duh walevi tangu lini mkaweza kucheza soka?.Mmejitahidi ndani ya 45°C na bado mkala 5-3 lazima niwape heko.
ReplyDeleteWakati mwingine muombe msaada toka mitaa ya huku Kashmir kuna kamati ya ufundi ya uhakika.
Kisiju ndio unachanganya watu kwama uji wa kihindi...8/8 ni siku ya wakulima au ya peasants?, na sabasaba (7/7) ni siku ya wakulima au wafanyakazi, full mixing hapa, au mimi sijui hebu nielezee uzuri weye Kijusi cha Pwani.
ReplyDeleteby mdau,
Ashkmatiti
sikukuu ya WAKULIMA, SABASABA tar 9/6/2009??????????????????????????
ReplyDeleteau "watanzania" wa india mnatoka nchi gani?
labda sielewi elewi...
nsaidieni
wee jennifer sumi
ReplyDeleteizo sikukuu za nchi gani???
SMAHANI ETI NI iringa au india????mbona kama kumefanana au ni mimi tu mijicho yangu?
ReplyDeletekaka 2licheza na timu ya hostel kwanguhapa.kama walikwambia ni kenya walikudanganya walikuwa na mchezaji mmoja 2 sasa wangechezaje....
ReplyDeleteAaah!! KIZITO baada ya kudisco UDSM kumbe ulikimbilia elimu ya kina kuchi kuchi otahe? Dah sie tupo bongo kama kawaida yetu tunaendelea kukomaa kuliokoa taifa letu. Kimsingi DARUSO bado ipo na mwendo ni uleule ingawae sasa hivi tuna mamluki kibao. We miss you sana brother, we remember your patriotic and ativist movement. we loved you alot big up sana brazaa ila wadau wanasema we mtoto wa fisadi mkuu wa wilaya ya nanilii because when tulipokuwa pamoja UDSM, you claim alot kwamaba we mtoto wa mkulima but leo uko NEW DELHI? tunadoubt upignaji wako. Sie tupo tunaendelea na slab kama kawaida yetu.
ReplyDeleteMdau Nyagonde
mh!! na hao ndo wasomi tunaowatemea warudi nyumabni na kubadilisha hali halisi iliyopo sasa!! msomi wa chuo kikuu INDIA hajui hata tarehe ya sikukuu ya nanenane!!!!
ReplyDeleteSasa naamini maneno ya wengi, kuwa kila kilaza anakimbilia kusoma india!! ninamfano wa watu 2 mabongolala ila cha kushangaza wapo sasa hivi huko wanakula nondo!! mmoja ya sheria mwingine ya comp science!
Kama wahindi elimu yao nzuri mbona wenyewe wanakimbilia nje kusoma hizo comp science na IT!!! hapa nilipo kuna wahindi kibao, kama darasa la IT wamejaa wenyewe!!, sasa sisi wa TZ kwanini tukimbilie kusoma kwao ilhali wao wenyewe wanakimbia kusoma hizo kozi nchini mwao!!
Hey Jenifer,waaooo can't beleive it,whats ya contacts its me an old friend frm Tabata.
ReplyDelete