JK akimtambulisha Hasheem Thabeet kwa wageni walioghudhuria hafla iliyoandaliwa Beverly Hills Hilton hotel jijini Los Angeles kwa heshima ya JK
Hasheem akisalimana na bosi wa NBA anayempongeza kwa kulamba bingo Memphis Glizzlies

Hasheem akionesha furaha yake baada ya kupata timu ya kuchezea
Hasheem akiwa na wenzie wa tano bora wa NBA Draft 2009. Toka shoto ni Jordan Hill, Tyler Hansbrough na Brandon Jennings.

SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF) PAMOJA NA WADAU WOTE WA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA TUMEPOKEA KWA FURAHA KUBWA KWA MTANZANIA MWENZETU HASHEEM THABEET KWA KUCHAGULIWA KWAKE KUWA MCHEZAJI NAMBA MBILI KATI YA WACHEZAJI THELATHINI KATIKA RAUNDI YA KWANZA KUCHEZEA TIMU YA MEMPHIS GLIZZLIES.

HAKIKA JANA SAA MOJA NA DAKIKA THELATHINI NA TISA ITAKUA IMEWEKA HISTORIA KWA HASHEM NA WATANZANIA WOTE BAADA YA KAMISHNA MKUU WA NBA DAVID STERN KUMTANGAZA HASHEEM KUWA NDIO CHAGUO LA PILI AKITANGULIWA NA BLAKE GRIFFIN AMBAYE AMEENDA LA CLIPPERS NA KUWAPITA KWA MBALI WASHINDANI WAKE WALIOPEWA NAFASI ZA JUU WAKATI WA MCHAKATO DE JUAN BLAIR (37) AMBAYE AMEENDA SAN ANTONIO SPURS NA RICKY RUBIO (5) AMBAYE AMEENDA MINNESOTA.

TBF INAWAPONGEZA WOTE WALIOWEZESHA MAFANIKIO YA KIJANA WETU AMBAYE ATATULETEA SIFA NA KUITANGAZA TANZANIA, RASI WA JAMHURI WA TANZANIA KIPEKEE KWA KUMSHAURI NA KUMPA MOYO KILA WAKATI, CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU CHA MKOA WA DAR ES SALAAM, MAMA HASHEEM NA NDUGU ZAKE PAMOJA NA UBALOZI WA MAREKANI KWA KUTUTAARIFU MARA KWA MARA NA KUFUATILIA MAENDELEO YAKE NA KUTUPA MOYO.

MUNGU MBARIKI HASHEEM
MUNGU IBARIKI TANZANIA

LAURENCE CHEYO

KATIBU MKUU- TANZANIA BASKETBALL FEDERATION


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2009

    kaka michuzi kwenye picha ya pili huy si mmiliki wa glizzles ila ni commissioner wa NBA au unaweza kumuita mwenyekiti kwa lugha nyingine

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2009

    acheni umbeya TBF huyo Hasheem hamkumsaidia hata kiduchu kufikia alipofikia ni jitihada zake!shame on you !

    ReplyDelete
  3. Je uraia wa nchi mbili upo hau haupo JK? Kwa sababu ya kodi lazima atakuwa Mwamerika soon

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2009

    HONGERA HASHEEM, HUO UREFU SIDHANI KAMA UNA HAJA YA KURUKA WE UNANYOOSHA MKONO TU KITU NA BOX.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2009

    hiyo picha ya pili, huyo siyo owner wa Grizzlies, ni NBA Commissioner David Stern

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 26, 2009

    hongera sana hasheem! ni furaha kwetu watanzania kwa kutuwakilisha! we support u! hureeeeeeeeee hasheeem!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2009

    Aisee!,hawa jamaa ni warefu,maana kama wanaringanaringana na hashimmu hivi!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 26, 2009

    Wadau, mie nina swali, hivi tumezoe kwenye soka, mchezaji akijiunga na timu fulani, basi kunakuwa na kitita anapewa aidha wewe mwenyewe au kupitia wakala, sasa mimi sijui utaratibu wa mpira wa kikapu, hasa NBA, Je huyu Hasheem Thabit amelipwa pesa zozote au ni ujiko wa kujiunga na timu tu ikiambatana na mshahara?, naomba kuuliza

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 26, 2009

    mkuu huyo anayesalimiana naye hapo sio bosi wake wa memphis grizzlies ila ni commissioner wa NBA David Stern. Na hao alionao sio tano bora, katika hao kwenye tano bora yuko yeye na Blake Griffin tu (kulia kabisa).

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 26, 2009

    We huyo nanihii sio bosi wa timu ya Memphis ni kamishna wa chama cha NBA anaitwa David Joel Stern na pia ni Lawyer kutoka Columbia University School of Law. Kucheza mpira ni muhimu na kusoma ni muhimu.Michael Heisley ndio majority owner wa Grizleis ya Mpemphis.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 26, 2009

    Kaka Michuzi waliokupa hizi picha hawajakupa "caption" kamilifu, hiyo picha ya pili sio mmiliki wa Memphis, ni Kamishna wa shirikisho la kikapu la Marekani (NBA Commissioner) David Stein. Na hao sio 5 bora wenzie, hapo tano bora yupo Blake Griffin tu, wengine hawakuchaguliwa katika tano bora.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 26, 2009

    Michael E. Heisley is an American businessman who is the majority owner of the Memphis Grizzlies. He orchestrated the move of the team from Vancouver in 2001, after promising to keep the franchise in Vancouver when he purchased it in 2000. Heisley regularly appears on the Forbes 400 Richest Americans list.

    Heisley is also involved in multiple business ventures, such as:

    Heico Holding, Inc.
    The Heico Companies, LLC
    Heico Acquisitions
    Stony Lane Partners
    Heisley was born in Washington, D.C., grew up in Alexandria, Virginia, and lives in Chicago, Illinois. He graduated from Georgetown University. Heisley is the director of the Heisley Family Foundation.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 26, 2009

    Mdau Anonymous wa Tarehe Fri Jun 26, 02:17:00 PM kukujibu swali lako ni hivi atapata kitu inaitwa Rookie Season Salary na itakuwa US $4,458,840 yaani dola za kimarekani milioni nne,mia nne na hmsini na nane eflu,mia nane na arobaini.
    Kwa habari zaidi fuata hii link
    http://hoopshype.com/draft.htm

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2009

    kikwete kasimama au amekaa,

    ReplyDelete
  15. Video kwa waliokosa kuona draft live hii hapa
    http://nukta77.blogspot.com/2009/06/congratulation-to-hasheem-thabeet.html

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 26, 2009

    SASA MHESHIMIWA RAIS JK,TUNAOMBA MSAADA WA KUKUZA MCHEZO HUU WA BASKETBALL NCHINI..KAMA ULIVYOTIA NGUVU KWENYE FOOTBALL,..TANZANIA INA NAFASI YA KUTOA AKINA HASHEEM WENGI TUU..we now need serious basketball Programs and Scholarships for our Kids..A NEW MODERN BASKETBALL ARENA WILL BE A GOOD START..KBC*

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 26, 2009

    sasa na nyie mliomkomalia mithupu..oooh sio boss mwenyekiti
    iweje???annon alotoa mwongozo mwanzo anatosha nyie vihere vya nini kwamba tujueje?ovyoooooooo

    go boy go...hongera sana...ila naskia ana asili ya rwanda imekaaje apo???ufafanuzi

    yan ao wooote wafupi????

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 26, 2009

    Mi-gravy uungwana huwa ni kuwa ukisahihishwa una acknowledge kuwa ulichemka na kufanya masasahisho lakini siyo kufanya masasahihisho kimya nakufanya wadau wanamakengeza. Wadau waliona hiyo ingekuwa kwenye paper ulichofanya ni kudesa ambacho ni aibu kwa mwandishi mzoefu kama wewe. Najuautaibania tu hii lakini ujumbe utakuwa umekufikia.
    Kwa anony wa june 26 12:46 umesema kweli tu hawa jamaa wanajua kupongeza tu hebu watuambie mchango wao kwake nini? Na hata sasa njia imefunguliwa ukiwauliza wana mkakati gani kuinua vipaji watatoa mimacho tu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 26, 2009

    Anon wa Fri Jun 26, 02:17:00 PM ni kwamba NBA hakuna transfer au purchase fees, kuna mkataba wa kucheza NBA ambao una-negotiate na timu inayokuchukua. Kama alivyosema mdau hapo juu huo ndo mshahara wake wa mkataba wa mwanzo. Akimaliza huo mkataba wa kwanza (rookie) anaweza kupanda au kushuka chati ikitegemea performance yake uwanjani.

    vilevile anaweza kupata endorsements nyingi kutoka makampuni mbalimbali, lakini kunakuwa na sharing scheme ya image rights kati yake na NBA....

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 26, 2009

    ongera sn kaka......japo na cie watz tupate mtu wa kumshangilia ktk ligi za kimataifa

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 26, 2009

    MPIRA WA WAPI HUO MCHEZAJI ANAPEWA PESA, LABDA HUKO BONGO, MCHEZAJI ATAKACHOPATA NI MSHAHARA TU NA MAPOSHO MENGINE ATAKAPOANZA KUCHEZA,KAMA VILE MATANGAZO YA BIASHARA % FULANI AMBAYO YEYE ATASHIRIKI NA HII INATEGEMEANA NA WAKALA WAKE ATAKAVYO-NEGOTIATE MKATABA AKIZUBAA HATA PIA ANAWEZA AKAKATWA PANGA KWENYE ADVERTS, WANAOPATA PESA NI MAWAKALA TU WANAMUUZA MCHEZAJI, KWANI KILA MCHEZAJI HUO NA WAKALA NA MENEJA WAKE, KATIKA MCHANGANUO WA KUNUNUA NA KUUZA HAPATI HATA SENTI TANO, ATAKACHOPATA NI MSHAHARA AKIANZA NGOZI.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 26, 2009

    Hongera HASHEEM, Dah Mdau hapo juu asante US $4,458,840 sio mchezo, Yaani hata kwenye Ndoto ni ngumu kuiota... Kutoka Sinza mpaka NBA kwa mshahara huo!??? Mungu Mkubwa... Im so Happy kwa Hasheem na Familia yake nzima...
    Sasa ukatulie ucheze kikapu cha kueleweka tukuenzi kama D.Mutombo na wengineo wanaowakilisha bara letu la africa, sio ulewe sifa uishie kuwa kama Lile huni la Bulls zamani D.Rodman...###
    NB: JEZI YAKO IKITOKA TU NANUNUA, Ntaivaa kila kona kupeperusha chata...

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 26, 2009

    get more for Thabeet
    http://www.youtube.com/watch?v=u_NKlU5iMqc&NR=1

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 26, 2009

    TBF sasa muache kuzurura ovyo na vi semina kibao visivyokuwa na maaana tena mfungo midomo yenu kuhusu Hasheem, tunajua vyema alikosota na hadi aliposikia...hakuna mkono wenu humo msijipendekeze...nendeni usukumani au umasaaani mkatafute akina Hasheem wengine siyo kujifanya mnalo mnalo lijua kuhusu dogo na juhudi zake binafsi.
    Wakati anasoma makongo mlikuwa mnamuona ka fala fulani, msitake tuboe yote nyie ni watu wazima nyie kina Cheyo...naaawambia fungeni domo wacha dogo afanye mambo na akamate mshiko labda baadaye ndiey tutamchagua rais hapo TBF ala....@@$$%%##%^^TBF

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 26, 2009

    nawaomba wanasiasa waache kumfuata fuata huyu dogo. mwacheni acheze basketball.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 26, 2009

    VICHECHE VYA KIBONGO HAPA MAREKANI KAMA NAVIONA VILE VITAKAVYOANZA KUJIPENDEKEZA MAANA NAONA WENGINE WATAJINYIMA KILA KITU ILI WAENDE KWENYE MECHI
    HASHIM KUWA MAKINI SANA ASILIMIA KUBWA YA KINADADA HAPA USA NI MAGOLD DIGGER

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 26, 2009

    TBF safirini na hiyo momentum kuimarisha mchezo huo bongo. Tengenezeni na kutekeleza mikakati ya kuinua mchezo, tusiishie kupongezana tu kwa kumwomba Mungu mwenzetu afanikiwe.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 26, 2009

    YAANI UMASKINI NDIO CHANZO CHA KILA KITU WAZEE,UKIANGALIA JINSI MITAA HII YA KWA OBAMA KULIVYO NA VIWANJA VYA BASKET,FBALL/SOCCER,TENNIS,SWIMMING POOL ETC YAANI MTU UWEZI KUSHINDWA KUCHEZA MCHEZO FLANI,YAANI KI UKWELI NINGEZALIWA HUKU AU KUJA HUKU TANGU UTOTONI,AMSURE KWA SASA NINGEKUWA ANOTHER NUMBER,BONGO MNATUCHOMESHA MAINDI SANA YAANI,WE LOST OUR REAL TALENTS KIRAISI TU!!HASHIM HILO NI ZALI MZEYA WE KAMUA ACHA UTANI!!

    ReplyDelete
  29. bulichekaJune 26, 2009

    hongera hasheeem, your success story thrills from internet cafe dar es salaam to NBA (mephis) huenda cafe ulisubiria foleni bila kukata tamaaa (JITIHADA BINAFSI).... kweli dream to reality we have seen ur ONLINE STORE hope tutanunua 2 hizo vitu
    his online store linkhttp://www.cafepress.com/HasheemThabeet/6767950

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 26, 2009

    Hongera Hasheem
    Wekeza nyumbani Usijali lolote zaidi ya kufuata moyo na unapokuwa na nafasi basi unawasaidia watoto ambao wanahitaji msaada kwa watu kama wewe.
    Umeweka historia pekee :) BONGO JUU BWANA.kAMA OBAMA vile.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 27, 2009

    That's my boy!!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 27, 2009

    MHESHIMIWA KIKWETE DUAL CITIZENSHIP INAKUWAJE?

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 27, 2009

    Dogo fuata nyoyo za wachezaji wengine kutoka africa kama Mutombo kutoka congo jamaa akuendekeza anasa au totoz badala yake amesaidia sana congo kahiyo kijana be careful we dondosha vitu kwenye nyavu tunataka tukuone kama most valuable player katika NBA

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 27, 2009

    Jamani, suala la uraia wa nchi mbili ni pana. Tulijadili kwa makini na tahadhari kubwa. Wengi tunaunga mkono kuwa ni kitu kizuri kwa WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA TANZANIA ila isiwe sababu ya watu wenye kupeperusha bendera yetu kubeba za wengine.

    Nyumbani ni nyumbani

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 27, 2009

    mtanzania sii mtanzania?????????

    tupeni profile yake apa

    HAMUELEWIIIII

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 27, 2009

    Ongera Hashim T.Ingawa hu ndio mwanzo tu na safari ngumu na pevu kuthibitisha huwezo wake NBA inakuja.

    It is time now for TBF to find best utilazation of this opportnity.Example, Using Hashim to connect with Tanzanian best basket ball players and to have special NBA Agent who is a Tanzanian.Kwa njia hii tunaweza kuwa na wachezaji wengi hapo baadye katika ligi ya NBA.

    Finally mlango umefunguliwa.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 28, 2009

    Hasheem tuwakilishe wenzio. Naona box lako litalipa kweli.

    Ndio mkome wabongo kila kukicha mwalia turudi nyumbani. Mnaona Box la Hasheem litalipa $ ngapi.

    Huku tuliko juhudi na determination zako kidogo tu una win. Bongo utasota weeeeee mafisadi na watoto wao wanakuja kusooma kidogo tu wakirudi nyumbani mara wamekua maboss wanakupita weeee na kijimaster chako cha mlimani kila kukicha unaonekana kama mjinga vile....mwishowe unaambiwa hujui kuchacharikia maisha...kumbe hamna anayekupa cheo au kuona kazi zako unazozifanya. Ndio maana watu maofisini bongo hawawajibiki ipasavyo kabisa. manake watu wanajua hamna reward yeyote na no matter what atakuja mwingine atapewa kazi na cheo zaidi so why bother

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 28, 2009

    Sio utani wazee, Bongo hoyeeee!Ila Memphis wana kazi nzito inabidi wafanye trades za nguvu. vinginevyo watakuwa wanashika mkia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...