


SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF) PAMOJA NA WADAU WOTE WA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA TUMEPOKEA KWA FURAHA KUBWA KWA MTANZANIA MWENZETU HASHEEM THABEET KWA KUCHAGULIWA KWAKE KUWA MCHEZAJI NAMBA MBILI KATI YA WACHEZAJI THELATHINI KATIKA RAUNDI YA KWANZA KUCHEZEA TIMU YA MEMPHIS GLIZZLIES.
HAKIKA JANA SAA MOJA NA DAKIKA THELATHINI NA TISA ITAKUA IMEWEKA HISTORIA KWA HASHEM NA WATANZANIA WOTE BAADA YA KAMISHNA MKUU WA NBA DAVID STERN KUMTANGAZA HASHEEM KUWA NDIO CHAGUO LA PILI AKITANGULIWA NA BLAKE GRIFFIN AMBAYE AMEENDA LA CLIPPERS NA KUWAPITA KWA MBALI WASHINDANI WAKE WALIOPEWA NAFASI ZA JUU WAKATI WA MCHAKATO DE JUAN BLAIR (37) AMBAYE AMEENDA SAN ANTONIO SPURS NA RICKY RUBIO (5) AMBAYE AMEENDA MINNESOTA.
TBF INAWAPONGEZA WOTE WALIOWEZESHA MAFANIKIO YA KIJANA WETU AMBAYE ATATULETEA SIFA NA KUITANGAZA TANZANIA, RASI WA JAMHURI WA TANZANIA KIPEKEE KWA KUMSHAURI NA KUMPA MOYO KILA WAKATI, CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU CHA MKOA WA DAR ES SALAAM, MAMA HASHEEM NA NDUGU ZAKE PAMOJA NA UBALOZI WA MAREKANI KWA KUTUTAARIFU MARA KWA MARA NA KUFUATILIA MAENDELEO YAKE NA KUTUPA MOYO.
MUNGU MBARIKI HASHEEM
MUNGU IBARIKI TANZANIA
LAURENCE CHEYO
KATIBU MKUU- TANZANIA BASKETBALL FEDERATION
kaka michuzi kwenye picha ya pili huy si mmiliki wa glizzles ila ni commissioner wa NBA au unaweza kumuita mwenyekiti kwa lugha nyingine
ReplyDeleteacheni umbeya TBF huyo Hasheem hamkumsaidia hata kiduchu kufikia alipofikia ni jitihada zake!shame on you !
ReplyDeleteJe uraia wa nchi mbili upo hau haupo JK? Kwa sababu ya kodi lazima atakuwa Mwamerika soon
ReplyDeleteHONGERA HASHEEM, HUO UREFU SIDHANI KAMA UNA HAJA YA KURUKA WE UNANYOOSHA MKONO TU KITU NA BOX.
ReplyDeletehiyo picha ya pili, huyo siyo owner wa Grizzlies, ni NBA Commissioner David Stern
ReplyDeletehongera sana hasheem! ni furaha kwetu watanzania kwa kutuwakilisha! we support u! hureeeeeeeeee hasheeem!
ReplyDeleteAisee!,hawa jamaa ni warefu,maana kama wanaringanaringana na hashimmu hivi!
ReplyDeleteWadau, mie nina swali, hivi tumezoe kwenye soka, mchezaji akijiunga na timu fulani, basi kunakuwa na kitita anapewa aidha wewe mwenyewe au kupitia wakala, sasa mimi sijui utaratibu wa mpira wa kikapu, hasa NBA, Je huyu Hasheem Thabit amelipwa pesa zozote au ni ujiko wa kujiunga na timu tu ikiambatana na mshahara?, naomba kuuliza
ReplyDeletemkuu huyo anayesalimiana naye hapo sio bosi wake wa memphis grizzlies ila ni commissioner wa NBA David Stern. Na hao alionao sio tano bora, katika hao kwenye tano bora yuko yeye na Blake Griffin tu (kulia kabisa).
ReplyDeleteWe huyo nanihii sio bosi wa timu ya Memphis ni kamishna wa chama cha NBA anaitwa David Joel Stern na pia ni Lawyer kutoka Columbia University School of Law. Kucheza mpira ni muhimu na kusoma ni muhimu.Michael Heisley ndio majority owner wa Grizleis ya Mpemphis.
ReplyDeleteKaka Michuzi waliokupa hizi picha hawajakupa "caption" kamilifu, hiyo picha ya pili sio mmiliki wa Memphis, ni Kamishna wa shirikisho la kikapu la Marekani (NBA Commissioner) David Stein. Na hao sio 5 bora wenzie, hapo tano bora yupo Blake Griffin tu, wengine hawakuchaguliwa katika tano bora.
ReplyDeleteMichael E. Heisley is an American businessman who is the majority owner of the Memphis Grizzlies. He orchestrated the move of the team from Vancouver in 2001, after promising to keep the franchise in Vancouver when he purchased it in 2000. Heisley regularly appears on the Forbes 400 Richest Americans list.
ReplyDeleteHeisley is also involved in multiple business ventures, such as:
Heico Holding, Inc.
The Heico Companies, LLC
Heico Acquisitions
Stony Lane Partners
Heisley was born in Washington, D.C., grew up in Alexandria, Virginia, and lives in Chicago, Illinois. He graduated from Georgetown University. Heisley is the director of the Heisley Family Foundation.
Mdau Anonymous wa Tarehe Fri Jun 26, 02:17:00 PM kukujibu swali lako ni hivi atapata kitu inaitwa Rookie Season Salary na itakuwa US $4,458,840 yaani dola za kimarekani milioni nne,mia nne na hmsini na nane eflu,mia nane na arobaini.
ReplyDeleteKwa habari zaidi fuata hii link
http://hoopshype.com/draft.htm
kikwete kasimama au amekaa,
ReplyDeleteVideo kwa waliokosa kuona draft live hii hapa
ReplyDeletehttp://nukta77.blogspot.com/2009/06/congratulation-to-hasheem-thabeet.html
SASA MHESHIMIWA RAIS JK,TUNAOMBA MSAADA WA KUKUZA MCHEZO HUU WA BASKETBALL NCHINI..KAMA ULIVYOTIA NGUVU KWENYE FOOTBALL,..TANZANIA INA NAFASI YA KUTOA AKINA HASHEEM WENGI TUU..we now need serious basketball Programs and Scholarships for our Kids..A NEW MODERN BASKETBALL ARENA WILL BE A GOOD START..KBC*
ReplyDeletesasa na nyie mliomkomalia mithupu..oooh sio boss mwenyekiti
ReplyDeleteiweje???annon alotoa mwongozo mwanzo anatosha nyie vihere vya nini kwamba tujueje?ovyoooooooo
go boy go...hongera sana...ila naskia ana asili ya rwanda imekaaje apo???ufafanuzi
yan ao wooote wafupi????
Mi-gravy uungwana huwa ni kuwa ukisahihishwa una acknowledge kuwa ulichemka na kufanya masasahisho lakini siyo kufanya masasahihisho kimya nakufanya wadau wanamakengeza. Wadau waliona hiyo ingekuwa kwenye paper ulichofanya ni kudesa ambacho ni aibu kwa mwandishi mzoefu kama wewe. Najuautaibania tu hii lakini ujumbe utakuwa umekufikia.
ReplyDeleteKwa anony wa june 26 12:46 umesema kweli tu hawa jamaa wanajua kupongeza tu hebu watuambie mchango wao kwake nini? Na hata sasa njia imefunguliwa ukiwauliza wana mkakati gani kuinua vipaji watatoa mimacho tu.
Anon wa Fri Jun 26, 02:17:00 PM ni kwamba NBA hakuna transfer au purchase fees, kuna mkataba wa kucheza NBA ambao una-negotiate na timu inayokuchukua. Kama alivyosema mdau hapo juu huo ndo mshahara wake wa mkataba wa mwanzo. Akimaliza huo mkataba wa kwanza (rookie) anaweza kupanda au kushuka chati ikitegemea performance yake uwanjani.
ReplyDeletevilevile anaweza kupata endorsements nyingi kutoka makampuni mbalimbali, lakini kunakuwa na sharing scheme ya image rights kati yake na NBA....
ongera sn kaka......japo na cie watz tupate mtu wa kumshangilia ktk ligi za kimataifa
ReplyDeleteMPIRA WA WAPI HUO MCHEZAJI ANAPEWA PESA, LABDA HUKO BONGO, MCHEZAJI ATAKACHOPATA NI MSHAHARA TU NA MAPOSHO MENGINE ATAKAPOANZA KUCHEZA,KAMA VILE MATANGAZO YA BIASHARA % FULANI AMBAYO YEYE ATASHIRIKI NA HII INATEGEMEANA NA WAKALA WAKE ATAKAVYO-NEGOTIATE MKATABA AKIZUBAA HATA PIA ANAWEZA AKAKATWA PANGA KWENYE ADVERTS, WANAOPATA PESA NI MAWAKALA TU WANAMUUZA MCHEZAJI, KWANI KILA MCHEZAJI HUO NA WAKALA NA MENEJA WAKE, KATIKA MCHANGANUO WA KUNUNUA NA KUUZA HAPATI HATA SENTI TANO, ATAKACHOPATA NI MSHAHARA AKIANZA NGOZI.
ReplyDeleteHongera HASHEEM, Dah Mdau hapo juu asante US $4,458,840 sio mchezo, Yaani hata kwenye Ndoto ni ngumu kuiota... Kutoka Sinza mpaka NBA kwa mshahara huo!??? Mungu Mkubwa... Im so Happy kwa Hasheem na Familia yake nzima...
ReplyDeleteSasa ukatulie ucheze kikapu cha kueleweka tukuenzi kama D.Mutombo na wengineo wanaowakilisha bara letu la africa, sio ulewe sifa uishie kuwa kama Lile huni la Bulls zamani D.Rodman...###
NB: JEZI YAKO IKITOKA TU NANUNUA, Ntaivaa kila kona kupeperusha chata...
get more for Thabeet
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=u_NKlU5iMqc&NR=1
TBF sasa muache kuzurura ovyo na vi semina kibao visivyokuwa na maaana tena mfungo midomo yenu kuhusu Hasheem, tunajua vyema alikosota na hadi aliposikia...hakuna mkono wenu humo msijipendekeze...nendeni usukumani au umasaaani mkatafute akina Hasheem wengine siyo kujifanya mnalo mnalo lijua kuhusu dogo na juhudi zake binafsi.
ReplyDeleteWakati anasoma makongo mlikuwa mnamuona ka fala fulani, msitake tuboe yote nyie ni watu wazima nyie kina Cheyo...naaawambia fungeni domo wacha dogo afanye mambo na akamate mshiko labda baadaye ndiey tutamchagua rais hapo TBF ala....@@$$%%##%^^TBF
nawaomba wanasiasa waache kumfuata fuata huyu dogo. mwacheni acheze basketball.
ReplyDeleteVICHECHE VYA KIBONGO HAPA MAREKANI KAMA NAVIONA VILE VITAKAVYOANZA KUJIPENDEKEZA MAANA NAONA WENGINE WATAJINYIMA KILA KITU ILI WAENDE KWENYE MECHI
ReplyDeleteHASHIM KUWA MAKINI SANA ASILIMIA KUBWA YA KINADADA HAPA USA NI MAGOLD DIGGER
TBF safirini na hiyo momentum kuimarisha mchezo huo bongo. Tengenezeni na kutekeleza mikakati ya kuinua mchezo, tusiishie kupongezana tu kwa kumwomba Mungu mwenzetu afanikiwe.
ReplyDeleteYAANI UMASKINI NDIO CHANZO CHA KILA KITU WAZEE,UKIANGALIA JINSI MITAA HII YA KWA OBAMA KULIVYO NA VIWANJA VYA BASKET,FBALL/SOCCER,TENNIS,SWIMMING POOL ETC YAANI MTU UWEZI KUSHINDWA KUCHEZA MCHEZO FLANI,YAANI KI UKWELI NINGEZALIWA HUKU AU KUJA HUKU TANGU UTOTONI,AMSURE KWA SASA NINGEKUWA ANOTHER NUMBER,BONGO MNATUCHOMESHA MAINDI SANA YAANI,WE LOST OUR REAL TALENTS KIRAISI TU!!HASHIM HILO NI ZALI MZEYA WE KAMUA ACHA UTANI!!
ReplyDeletehongera hasheeem, your success story thrills from internet cafe dar es salaam to NBA (mephis) huenda cafe ulisubiria foleni bila kukata tamaaa (JITIHADA BINAFSI).... kweli dream to reality we have seen ur ONLINE STORE hope tutanunua 2 hizo vitu
ReplyDeletehis online store linkhttp://www.cafepress.com/HasheemThabeet/6767950
Hongera Hasheem
ReplyDeleteWekeza nyumbani Usijali lolote zaidi ya kufuata moyo na unapokuwa na nafasi basi unawasaidia watoto ambao wanahitaji msaada kwa watu kama wewe.
Umeweka historia pekee :) BONGO JUU BWANA.kAMA OBAMA vile.
That's my boy!!
ReplyDeleteMHESHIMIWA KIKWETE DUAL CITIZENSHIP INAKUWAJE?
ReplyDeleteDogo fuata nyoyo za wachezaji wengine kutoka africa kama Mutombo kutoka congo jamaa akuendekeza anasa au totoz badala yake amesaidia sana congo kahiyo kijana be careful we dondosha vitu kwenye nyavu tunataka tukuone kama most valuable player katika NBA
ReplyDeleteJamani, suala la uraia wa nchi mbili ni pana. Tulijadili kwa makini na tahadhari kubwa. Wengi tunaunga mkono kuwa ni kitu kizuri kwa WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA TANZANIA ila isiwe sababu ya watu wenye kupeperusha bendera yetu kubeba za wengine.
ReplyDeleteNyumbani ni nyumbani
mtanzania sii mtanzania?????????
ReplyDeletetupeni profile yake apa
HAMUELEWIIIII
Ongera Hashim T.Ingawa hu ndio mwanzo tu na safari ngumu na pevu kuthibitisha huwezo wake NBA inakuja.
ReplyDeleteIt is time now for TBF to find best utilazation of this opportnity.Example, Using Hashim to connect with Tanzanian best basket ball players and to have special NBA Agent who is a Tanzanian.Kwa njia hii tunaweza kuwa na wachezaji wengi hapo baadye katika ligi ya NBA.
Finally mlango umefunguliwa.
Hasheem tuwakilishe wenzio. Naona box lako litalipa kweli.
ReplyDeleteNdio mkome wabongo kila kukicha mwalia turudi nyumbani. Mnaona Box la Hasheem litalipa $ ngapi.
Huku tuliko juhudi na determination zako kidogo tu una win. Bongo utasota weeeeee mafisadi na watoto wao wanakuja kusooma kidogo tu wakirudi nyumbani mara wamekua maboss wanakupita weeee na kijimaster chako cha mlimani kila kukicha unaonekana kama mjinga vile....mwishowe unaambiwa hujui kuchacharikia maisha...kumbe hamna anayekupa cheo au kuona kazi zako unazozifanya. Ndio maana watu maofisini bongo hawawajibiki ipasavyo kabisa. manake watu wanajua hamna reward yeyote na no matter what atakuja mwingine atapewa kazi na cheo zaidi so why bother
Sio utani wazee, Bongo hoyeeee!Ila Memphis wana kazi nzito inabidi wafanye trades za nguvu. vinginevyo watakuwa wanashika mkia.
ReplyDelete