Rukia Mtingwa, Meneja wa Libeneke (Matukio) na Promoshani wa Vodacom Tanzania akiongea kuhusu kumalizika kwa programu ya Tuzo Milionea ambapo ngwe ya pili itaishia wiki hii wakati mdau mmoja atatangazwa mshindi na kuvuta milioni 100 kesh!

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imetanganza mwisho wa program yake ya Tuzo Milionea iliofanyika kwa muda wa miezi miwili sasa.

Rukia Mtingwa, Meneja wa Matukio na Promoshani wa Vodacom alisema, “programu ya Tuzo Draw ilikuwa na ngwe mbili, ya kwanza ilikua kianzia mwezi wa nne 2008 na kuisha mwezi wa tatu 2009 iliojulikana kama TUZO DRAW.

Wakati ngwe ya pili ya TUZO MILIONEA ilianza mwezi wa nne (Aprilli) mwaka huu na itaisha wiki hii wakati mshindi mmoja atakapojinyakulia jumla ya shilingi Milioni miamoja taslimu”.

Katika ngwe ya pili ya Tuzo Milionea Vodacom Tanzania imewazawadia jumla ya washindi 59 muda wa maongezi cha shilingi laki moja moja. Washindi hawa walipatikana katika droo zilizoendeshwa kila siku chini usmamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha.


Hadi sasa Vodacom Tanzania imeshatoa zawadi ya zaidi ya biliioni moja fedha taslim kwa wateja wake kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.

“Kwa kuwa tunaelekea mwisho wa programu hii na droo kubwa kuchezeshwa Ijumaa wiki hii tarehe 18 Juni, Live katika kituo cha televisheni cha TBC1 saa tatu usiku, natoa wito kwa wateja wa Vodacom kujisajili ili waweza kupata nafasi ya kuwa mshindi kwani muda bado upo" alisema Rukia.

Aliendelea kusema, “Vodacom Tanzania mapema mwezi Machi mwaka jana ilianzisha programu ya uaminifu ya tuzo pointi/Droo lengo likiwa ni kuwashukuru wateja wa Vodacom Tanzania kwa kuufanya mtandao wa Vodacom Tanzania kuongoza hapa Tanzania”.

“Kwa kweli Programu hii imesaidia kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi, waliobahatika kushinda ndani ya familia yetu kubwa ya Vodacom Tanzania wameboresha maisha yao,”.

Kwa niaba ya Vodacom ningependa kuwashukuru wateja wetu wote,na kuwahakikishia kwamba kampuni yao ya Vodacom inayotoa huduma bora na yenye mtandao unaoongoza hapa Tanzania tupo pamoja nanyi daima na kila la kheri kwa mshindi ataejinyakulia shilingi milioni mia moja wiki hii", alimalizia Meneja huyo wa Libeneke na promosheni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2009

    RUKIA MTINGWA NAMKUMBUKA AKIWA ITV HAPO ZAMANI. HILO SHAVU MWANANGU, UTADHANI MTOTO WA MIAKA 12. NINI SIRI YAKE DADA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...