Home
Unlabelled
uchochoro wa palm beach
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Well njia rahisi zaidi nafikiri ni kutumia tunnel mfano...Unaingia www.vtunnel.com utakutana na msg kama hii "Enter a URL below to browse the internet securely!" hapo ingiza URL ya Blog ya Jamii then begin browsing na utakuwa ndani ya blog ya jamii kama hao Wachina wame-block blogs!
ReplyDeleteUnaruka majivu unakanyaga moto
ReplyDeletewako wapi?
ReplyDeletewafenyeje sasa!
wavunje majengo mangapi dar?
Suala la mipango miji kwa hapa Bongo ni sawa na kumpigia mbuzi gita, ni kitu ambacho "waheshimiwa" hawakijui kabisa, wako bize na ufisadi! Angalia mfano wa "majiji" ya Mwanza, Mbeya, Tanga, Arusha na Dar es Salaam kwenyewe, ni wapi ambapo pametengwa (bustani) kwa ajili ya wananchi kwenda kukaa na kumpumzika kwa utulivu? Vurugu tupu, Kila mhusika yuko bize na maslai binafsi.
ReplyDeleteDah, kile ki border kipo?
ReplyDeleteUkifika barabara kubwa (Mwinyi)lazima uende toward Salender (huwezi kukata kulia kuelekea mjini.) Ni bora usiingie hilo border congested uende kwa nyuma moja kwa moja mpaka United Nations road (ubalozi wa Korea) ukate kulia uje kutokea taa za Italian Club(sijui bado ipo?). Utakuwa umekwepa taa za Palm Beach Hotel (ipo?).
Isitoshe hiki ki blind alley ndio Gibson Mwaikambo alifia mitaa hiyo. Hakijulikani kama ni one-way ama vipi. Nuksi.
mipango mji tupooo....ndiyo tupooo te teh teh teeeeeeehhhhhhhhhh
ReplyDeleteBONGO kuna watu wa mipango MIJI? labda kimalipo sio kikazi.
ReplyDeletenimependa hiyo www.vtunnel.com, though am not in china! tthanx
ReplyDeleteam just dreaming in the year 2070.. serikali ya awamu ya kumi itajenga lidaraja limoja safi linalocross bahari Hindi hadi kaunda street, mataa ya salendar tunawaachia waendao migo na kwengineko.. the he he the.. bongo ya 2070 itakuwa tambararee. I'll be loong dead though .. my 2 cents.
ReplyDelete--Proud Tanzanian
Sir why people dont comment the flag area thats my country's Ambassy Burundi Ambassy au residence kama sijakosea !!!means kuna kinjia huko pembeni nilikuwa sijawahi kukiona maana nimetembelea mda mrefu bongo ila nadhani ni yneyewe maana last time was in 2002 ,your Bdian fan from Scandinavia B.
ReplyDeleteHii picha inaonesha moja ya uozo uliopo ndani ya Serikali ya Tanzania.
ReplyDelete1: Ndani ya Serikali ya Tanzania pamoja na ofisi zake hakuna mtu ata mmoja ambaye anayeipenda nchi hii, Kuanzia Rais mpaka raia wa kawaida wote wana mawazo ya kuweza kujipatia utajiri na hakuna mtu mwenye kujari na kujiuliza je kizazi kijacho kitafanyaje?.
2: Kutokana na kwamba hakuna mtu anaye weza kujari kuhusu nchi au kizazi kijacho cha Tanzania ndio maana mapato na matumizi ya Serikali na ofisi zake hazina muelekeo ktk kuleta maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla, hapo ndio utakapo kuja kuona hakuna barabara zikijengwa na ata zikijengwa basi hazina uimara wa kudumu.
3: Kutokana na kipengere cha (2) ndio maana nchi haina maendeleo yoyote miaka yote hii, watu wapo tayari wafanye sherehe za uhuru na kupoteza mabilioni ya Pesa na kuzidisha umasikini badala ya kufanya sherehe ndogo na kuongeza nguvu za kuleta maendeleo. Kutokana na ili nchi ya Tanzania inakuwa kama Congo Drc ambapo mwenye nguvu uvuna na kwenda zake na kumpisha mwingine...
4: Ni aibu kwa Rais wa nchi, mawaziri, Wabunge, Wasomi, Wanasiasa na raia wa Tanzania kushindwa kuwa na uchungu wa nchi hii na kuiacha ikiteketea na kuzidi kuwa masikini. Viongozi hawa hawa ndio wale wale wanao kuwa na maekalu, magari, pesa za wizi na kusomesha watoto wao nje za nchi, n.k
5: Tanzania ni nchi tajiri yenye kuweza na kuwa na maendeleo makubwa sana, Ni sisi wenyewe kujiwekea mipangilio katika maisha yetu ya kila siku, kuheshimu sheria, kuhacha wizi, na kuwa wakweli ktk kuendesha maisha yetu.
6: Tunahitaji raia wenye mawazo mema, elimu kwa wote, uongozi ulio safi na mipangilio mirefu iliyo kwenda shule, Raia wote kuhacha na kutopenda rushwa, kuheshimu sheria na kuwa na uchungu wa nchi yetu Tanzania kwa pamoja.
Nilikuwa nje Ya Tanzania kwa muda, nikarudi nyumbani kidogo haya ndio niliyo yaona:
a: Kila sehemu niliyo kwenda ni rushwa, Kuanzia Uwanja wa ndege, polisi, mawakili, Viongozi, wanasiasa, raia, n.k
b: Kutokana na hali ngumu ya Maisha umalaya umeongezeka na kurudisha nyuma maendeleo. Ukimwi umeongezeka.
c: Hakuna kilicho endelea, kila kitu kile kile kama nilipo acha zamani.
d: Idadi kubwa haina kazi wala elimu - Hiki ndicho kinacho niogopesha, kizazi hiki kisicho kuwa na kazi kitakwenda wapi na kufanya nini??? Wachache ni matajiri sana na hakuna ukweli wa utajiri wao, gap ya masikini na matajiri ni kubwa sana na ina ogopesha!!!
e: Kila kitu kinachofanyika ni kama hakuna mawazo yaliyo kwenda shule, kuanzia serikali, n.k. Ukiangalia utadhani nchi haina Uongozi.
f: zaidi ya 80% ya viongozi, wanasiasa, wafanyakazi wa serikali na binafsi wanapokea na kutoa rushwa, kuibia serikali, nchi au waajiri wao, n.k Hakuna mtu mwenye uchungu wa nchi na kwa jinsi inavyo onekana wanaweza kuuza nchi au kufanya chochote kibaya, kupindua nchi kutokana na pesa, kujitafutia utajiri, madaraka, n.k
g: Wachina wameleta vitu feki kila kona, hakuna anae onekana akifanya lolote sio serikali wala ofisi za Serikali, hii inaonesha wame ridhishwa na hali halisi, sio kwamba hawajui bali wamefumba macho kwakuwa wanapata 10%
Unaweza uka feki kila kitu, chochote unachotaka...inatia uchungu na uruma sana, uwezi kujua kipi cha kweli kipi feki.
Nilibaki kusikia uchungu sana, nilishindwa jinsi ya kuishi, kwakuwa nilizoea kupata mahitaji yangu muhimu na haki zangu bila ya kutoa rushwa, niligandisha kila kona kwakuwa sikutoa rushwa!!!
Jamii yenye mafanikio ni ile inayo fundishwa toka ikiwa changa nini maana ya maendeleo kwa ujumla, madhara ya rushwa, umuhimu wa amani, kuipenda nchi, n.k cha kushangaza sikuona Tangazo lolote eidha ktk radio, tv, au magazeti ikizungumzia yoyote kati ya haya kwa kipindi chote cha mapumziko yangu.
Hapa nilipo, kila siku ni lazima nione moja ya Tangazo yakielimisha jamii, hapo ndipo jamii inapokuwa na upendo wa nchi na kuweza kuleta maendeleo.
Nina amini Tanzania ni nchi tajiri, ila hatuna uongozi na raia wenye kuweza au kuwa na mawazo ya maendeleo. Lakini sitokata tamaa, ipo siku nitakuja kuona maendeleo.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Habari za leo.tunaandika sana comment zetu kwa uzuri tu. sijui kama kweli zinawafikia wahusika na kufanyiwa kazi. labda michuzi unaweza thibitisha hilo. Ushauri wa bure kwenye mipango miji. Tukiangalia sababu ya kuwa na foleni sana Dar na baadhi ya miji ni short term plan ya mambo bila kufikiria kuna swala ya mji kupanuka. Tunaona ujenzi wa Magorofa Posta mfano Exim tower;Nssf etc yao yakiisha yanaitaji watu kujakufanya kazi na wote wanakuja na public transport na wengine Private, Isitoshe wanakwenda upande moja na kwa njia moja asubuhi na jioni wanarudi upande ule ule. Swali langu kwa nini Magorofa yasiendeleze tegeta. mwenge na nje ya Posta kupunguza msongamano, Pili kwa nini wizara ziliondolewe posta ziende nje ya posta. Na pia foleni hata kwenye maofisi km POSTA mtu anatoka tegeta na private kuja posta kupost barua .kwa nini posta isipatikane huduma nje ya MJI. Tuje kwenye Longterm plan. kwa nini Watu wa miundo mbinu na barabara wasifikirie kwamba barabara za mitaani zipinge lami(kutengenezwa)kupunguza foleni. Tatu long term plan. Lazima ujumuishe na soko huria ,kwamba watu wanauhuru wa kununua magari na kila siku yanaingia mapya barabarani,(Let say minimum magari 20 kwa siku)yanaingia kwenye barabara ile ile ya mwenge-posta tunategemea nini? tukifanya ujenzi lazima tujue hii barabara ni kwa miaka 50 mpk 100 ijayo kama wenzetu wazungu. sasa Ushauri unaoitajika sasa nikuanzisha Tramps sehemu mbali mbali kwani zinakwenda speed, zitasaidia foleni kupungua au kuisha kabisa na watu kupark magari yao.
ReplyDeleteTuache Kelele nyingi jamani,tujiulize kila mtu kwa binafsi yake anafanya nini kurekebisha matatizo tulionayo?Mengi ya matatizo yaliyopo yanatokana na ubinafsi,ulafi,ujinga, na uvivu wetu katika kufikiri na kutenda.Hakika kama kweli tunataka kuondokana na matatizo haya ni tufanye vitendo badala kupiga domo kaya.
ReplyDelete