HABARI KAMILIFU
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MAJINA ya watu sita waliokufa maji katika ajali ya meli ya mizigo ya mv Fatih yametambuliwa.
Meli hiyo ilipinduka na kuzama usiku wa kuamkia juzi katika Bandari ya Malindi muda mfupi baada ya kuwasili ikitokea Dar es Salaam. Watu wengine 27 waliokolewa.
Kwa mujibu wa Dkt.Mariamu Ahmed wa Hospitali ya Mnazi mmoja ya mjini hapa, waliokufa ni Yusuf Ali Omari(10)na Awena Nassoro Ali (40), wote wa familia moja, wakazi wa
Mwanakwerekwe maili nne, Zanzibar.
Wengine ni Bi. Ashura Suleiman Mtega(40),Ali Haroub Mohamed (3) na Mukrim Mohamed(6) ambao ni ndugu, wakazi wa Mtopepo, Zanzibar . Mwingine ni Bi.Neema Meshack(19) mkazi wa Dodoma ambaye alisafirishwa jana kwenda kwao.
Wakati huo huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kuagiza chombo cha kusaidia kuopoa meli hiyo ambayo bado imezama bandarini hapo baada ya juhudi za kuitoa kwa kutumia
upepo, kukwama.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Bw. Hamza Hassan Juma, alipokuwa akizungumza na waandishi wahabari katika eneo la tukio muda mfupi baada yakikao cha
Kamati ya Maafa kumalizika kujadili suala hilo.
Waziri Hamza, alisema kwamba Serikali imeamua kuagiza kifaa cha kuongozea meli (tagi) ili kusaidia kuopoa meli hiyo ambayo imezama ikiwa na shehena ya mizigo na abiria.
Alifafanua kuwa awali meli hiyo ilikuwa itolewe kwa kujazwa upepo kwa kutumia mashine maalumu, lakini ilishindikana baada ya upepo kutoka kila wataalamu walipokuwa wakiujaza.
"Tatizo hilo lilisababishwa na matobo matatu yaliyogundulikakatika meli hiyo na kulazimika kuzibwa kwa kutumia 'welding'(mashine ya kuchomelea vyuma) lakini bado imeshindwa kuja juu,"alisema Bw.Hamza.
Akizunumgumzia mkasa huo, alisema ripoti inaeleza kwamba meli hiyo baada ya kufikia eneo la Chumbe ikiwa umbali mfupi kutoka Bandari ya Zanzibar, ilianza kuingiza maji na mabahari walichukua hatua ya kumwaga maji hayo kwa kutumia pampu huku wakiendelea na safari .
"Nahodha aliwasiliana na watu wa bandari na wao wakamshauri afunge gati katika Bandari ya Malindi lakini chanzo cha kupinduka meli bado hatujakipata na tunaendelea na uchunguzi zaidi", alisema.
Hata hivyo alisema kwamba kumbukumbu zinaonesha chombo hicho kilikaguliwa hivi karibuni na kupasishwa ingawa kinaoneka kina matobo chini lakini hilo litategemea ripoti za wataalamu wanaochunguza ajali hiyo.
Aidha alisema idadi ya abiria waliokuwemo katika chombo hicho imeelezwa walikuwa 35 na
mabaharia 13, lakini waliookolewa ni 27 jambo ambalo linaonesha meli hiyo ilikuwa na watu wengi zaidi ya waliotajwa.
"Ukweli utapatikana baada ya chombo kuopolewa na kama kuna vitendo vya ukiukwaji wa sheria hatua zitachukuliwa kulingana na uzito wa kosa lenyewe", alieleza.
Bw. Hamza alisema Kamati imetenga sh.milioni 20, kushughulikia tatizo hilo na kuwataka wananchi ambao hawajawaona ndugu zao, watoe ripoti kwa kamati hiyo ambayo imeanza kupokea matatizo hayo kupitia ofisi yake ya muda iliyofunguliwa bandarini hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Bw. Bakari Khatib Shaaban, amesema juhudi zinaendelea za vikosi vya uokoaji lakini hakuna maiti zilizopatikana zaidi ya tano.
"Juhudi za kuopoa chombo zinaendelea lakini mpaka sasa sina jipya zaidi ya watu watano waliopatikana na wale 27 waliokolewa awali," alieleza Kamanda huyo.
Meli hiyo ilizama katika Bandari ya Malindi ikiwa na shehena ya mbao, mchele, unga wa ngano na soda, ambapo hadi jana baadhi ya vitu vilikuwa vikiokolewa huku ulinzi ukiimarishwa bandarini hapo baada ya vibaka kuanza kuzamia baharini na kubeba vitu hivyo eneo la Forodhani.
Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeimarisha ulinzi katika maeneo ya kuingia na kutoka bandarini hapo lakini kumekuwepo huku likizuia mtu
yeyote kuingia zaidi ya wafanyakazi wa bandari na abiria.


siamini!!
ReplyDeleteyan adi leo bado kuna abiria umo?afu ndo mwawaza kuleta ilo tagi sijui??
tobaaa,sijui tuote mbawa!!
Tunaomba Mungu awarehemu na awape Subra wafiwa na wale wote waliojeruhiwa.
ReplyDeletejamani Meli imezama sababu ya uzembe wa serikali. watu wa tower wamejulishwa toka chumbe meli haifiki wakalazimisa iletwe bandarini. meli imefika wanaombwa walete tagi izuwie wamedharau eti wanasema captain kapakia magendo na amezowea kutaka kupaki meli anapotaka. Kisa last month ilipata tatizo la stering akapaki kwa lazima mkokotoni kuokoa maisha ya watu.
EBU FIKIRI NA SERIKALI IKAZUWIA LESENI YAKE NA KUCHARGE KUMPUNI FINE YA MILI 30.
ANGELAZIMISHA KWA SERIKALI ZETU YULE ANGEFUNGWA NA LESENI YAKE INGEZUIWA MAISHA.............
KAMA SERIKALI SI ZEMBE, KWA NINI WACHINA WAMETAKA KUOKOA WATU WAKAZUIWA? WAZAMIAJI KIBAO WAMEJITOLEA WAKAZUIWA? FIRE, POLICE, WALIFIKA BANDARI KABLA HATA MELI HAIJAFUNGWA WALIJUAJE KUNA HATARI KAMA CAPTAIN HAKUTOA TAARIFA.
Huo ni uzembe wa serikali bwanaaaaaaaaaaaaaa.
wanauwa watu kupunguza kura makusudi. kwanza tunasikia mke wa Karume ana shea katika hiyo meli, so they only think about the boat not people.
Watu wa tower ni wazembe.
Captatin kaonewa atolewe ndani. mbona watu wa tower wako town wanakula raha?
Kafanya kazi yake sahihi, mlitaka ashindane na serikali? Jamani serikali yetu haina sheria, wa2 wanatunga wenyewe.
mie hizi coments zinanichanganya!.
ReplyDeletenadhani wale MGAMBO au baadhi ya WANAJESHI wangekuwa TRAINED...kufanya shughuli kama hizi za kuokoa watu badala ya kwenda kuwaharass wamama wa watu wanaojitafutia riziki zao.
however,nadhani vyombo vyote vinavyotumika kusafirisha watu,viwe vinakaguliwa kila mwaka kama vinafaa kutumika kwa kazi hio..in this way watu watakuwa na confidence kuwa vyombo hivyo ni salama.
ajali naturally haziwezi kuepukika,ila tukiwa na utaratibu wa kukagua vyombo vyote vya usafiri....then vyombo vile vimekwisha,vibovu...vibovu vinaweza kuondolewa kny system na hivyo kupunguza ajali!
HEAVYPENALITIES kwa wale WAMILIKI..wanaokwepa kupeleka vyombo vyao kukaguliwa...looooooolz!!!
nadhani pia wamiliki wawe subjected kulipa some form of tax/insurance...ili kucompesante watu kukiwa na ajali,na pia kusimamia GHARAMA za uokoaji!
ALTERNATIVE ni kuwa na plane/CHEAP FLIGHTS btn the places!
michuzi hata sijui nandika nini hapa leo...aaagh ila hivyo hivyo.