JE NI KWANINI TUZITUMIE POSTA,
BANDARI NA AIRPORT ZA TANZANIA?
Siku chache zilizopita, kumekuwepo na malalamiko ya kutosha kuhusiana na Airport, Posta pamoja na Bandari ya Dar. Na kusema kweli, hali ya hizi idara zinatisha kiasi kwamba tunaonelea ni vyema tuukane uraia wa kitanzania na kubakia ughaibuni, au tutumie eapoti za Nairobi na Bandari ya Mombasa.
Inasikitisha sana, baada ya kuangaika na kujinyima nchi za nje kutafuta riziki ili kuendeleza ujenzi wa nchi yetu kwa michango yetu midogo, mara tunapotua nchini kwetu, kuanzia kwenye kaunta za Immigration unakuta ni aibu tupu.
Unaposogea kwenye customs, unakutana na watu wenye vitambi wenye macho ya tamaa, kwenye mizigo yetu ni wale manyang’au wanaoiiba bila kujali kana kwamba hawana akili nzuri.
Nimekuwa nikiishi hapa Ujerumani kwa miaka 14 sasa. Kwa sabau ya kukosa makaratasi nilishindwa kurudi nyumbani hadi mwaka 2004. Lakini ingawa nilikuwa sirudi nyumbani, kila mara nilikuwa natuma mizigo midogo midogo pamoja na fedha kusaidia ndugu zangu nyumbani. Mwaka 2006 nilinunua gari lililotumika la mwaka 2001 kwa $3,800 pamoja na usafiri Ikafikia $4,800 nakutima nyumbani pamoja na nyaraka zote original.
Gari ilipofika, ufisadi ulianzia TRA, TSCAN nk.. hadi kuitoa gari bandarini, nililipa kiasi cha $7,000 Inatia hasira sana, kuona kwamba kumnyima mtu rushwa inamfanya nakuhadhibu.
Watu wa TRA waliponyimwa Rushwa walipandisha thamani ya gari, hapo hapo wakaanza kunifanyia mambo yawe magumu, inspection certificates wakadai ni feki, kwa hiyo TSCAN ikabidi wafanye inspection mpya na kunichaji zaidi ya $900.
Niliporudi nyumbani mwaka 2007 February, kwenye msiba, hapo hapo kipawa, nilikuta mzigo wangu umefunguka, lakini sikufatilia sana kujua ni kipi hakipo ndani ya begi. Nikapitia kwa watu wa customs ambao walichomoa Camera wakasema nilipie ushuru, na thamni yake wakaiweka millioni mbili, kwa maana hiyo walitaka nilipe VAT, na 25% kwa hiyo ni kama 55% ya millioni mbili nilikataa, wakaniambia basi hawawezi kunisaidia. Ikabidi nihonge $50 ili nipewe Camera yangu ambayo nilinunua Euro 150.
Kufika nyumbani, saa niliyoweka kwenye begi na viatu vipya sikuvikuta. Baada ya hapo niliamua kutokutumia Airport ya Dar es salaam tena. Natumia Nairobi na sijawahi kupata tatizo tena..
Vile vile nilipotuma gari aina ya Pick-up niliyonunua toka Japan, niliituma kupitia bandari ya Mombasa, na wala haikuchukua siku mbili kuitoa bandarini na gharama zilikuwa chini mno. Kuelekea Bukoba ilibidi nitumie mpaka wa Tarime ambako sikupata bugudha.
Licha ya yote, nimetuma vifurishi vingi tu kupitia posta ya Tanzania, lakini mpaka leo havijafika, ingawa vilisajiliwa sehemu zinazotoka. Unapouliza nchi za watu wanakuthibitishia kwamba bidhaa ulizotuma zilifika Tanzania, matokeo yake unanyamaza kimya.
Kwa nini hawa wezi wazidi kuachwa kufanya kazi shemu kama hizi ambapo wanawaibia na kuwanyanyasa hata wageni wanaoleta fedha za kigeni? Swali langu, je ni faida gani kuwa raia wa Tanzania, kuzitumia na kupata kero tunazozipata tukirudi nchini kwetu au tunapotuma kitu ambacho kina manufaa kwa nchi yetu.
Kuna kosa gani tunapotumia Airport ya Nairobi ambayo haina bugdha au Bandari ya Mombasa isiyokuwa na Urasimu?
Kwa nini watanzania wawe ni watu wa ajabu kiasi hiki, mengine vitambi vinazidi kuwa vikubwa kwa kuwaibia wanchi wakati ni shuguli zao kuwalinda?
Mdau Benjamin M.. Ryayemamu
Berlin,
Germany

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2009

    Yaani Airport ya Bongo na Bandari mmh! sina hamu nao!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2009

    Viongozi wahusika wanjifanya viziwi lakini ukweli ni kwamba option ya Mombasa kwa wananaonunua magari ughaibuni imekuwa ndio chaguo la wengi. Inasikitisha mno kwamba mimi mtanzania ninunue gari halafu nilishushie mombasa wakati hata nyumbani kuna bandari!
    AIRPORT pale ni ufisadi mtupu kweli yaani nitoke zangu notoke zangu huku ughaibuni eti nishukie Jomo Kenyatta kwa sababu JNIA kuna wadokozi. Jamani hiyo ni Somalia, serikali gani hii isiyo sikia vilio vya wananchi wake!
    Tutaongea mpaka mtusikie! Hao wadokozi, mafisadi waondolewe hizo sehemu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2009

    Bw.Rweyemamu,
    Pole sana kwa yote, na wewe si wa kwanza kukumbwa na na mabaraha haya,kwa kweli tuna safari ndefu sana,na hauatwezi kujisafisha nafsi zetu,uchafu huu wa nafsi ndio adui mkubwa wa maendeleo yetu,katika tahasisi kama Posta,TRA,Airport,Bandari,kumejaa watu wavivu walio na wivu wa kujituma,na kwa kuwa wapo pale na wanalindwa na baadhi ya vivuli vya mabosi wao walio na tabia kama wao,kichaka cha uchafu wakuficha rushwa na mengineyo bado unaendelea.
    Tabia kama hizi basi si kwa walio watumishi wa umma walio nyumbani tu,bali pengine unaweza kukutana na watu kama hao,hapo hapo Berlin katika ubalozi wa Tanzania ,badala kuhudumiwa unageuzwa kuwa msaliti kwa kosa la kuondoka nchini kwenu na kuwaacha nduguzo wakilimwa na jua.Kwa kweli inasikitisha sana sana kuona mzalendo kama wewe unanyasika katika ardhi uliyozaliwa!

    ReplyDelete
  4. engineer canadaJuly 29, 2009

    hii inarudi kwenye kitu nilisema hapo mwanzo. Tanzania tunazawadia watu wahalifu. Tanzania hatujajenga tabia ya uwajibishwaji. Mi nashauri kutimua watu kazi, kitengo kizima kifukuzwe kazi (reason, guilty by association..or there is no way you did't know about this and you havedone nothing to stop it) kuna watu maelfu wanatafuta kazi tanzania. uwanja wwa ndege wenyewe wachakaa kila siku lakini hakuna mtu anawajibishwa. aibu aibu aibu!! Ushauri kwa watanzania wote mnaotumia huo uwanja funga begi na kufuli. Kisha tumia zile plastic wrap. mara nyingi wizi hufanywa kwa sababi ni rahisi kuiba.

    Pia sitakaa nisahau siku nimerudi nyumbani, nilipofika DIA harufu nzito ya mkojo ilikuwa inapanda ngazi.

    ReplyDelete
  5. Anko nanihii tunaomba umwambie joni mashaka au shayo waandike atiko ya kuhamasisha watu ili tuweze kuzisusa posta, bandari na eapoti
    tukifanya hivi hawa jamaa watkosa mapato na watakoma adabu. Wanatunyanyasa sana wezi wakunwa sana. Wee mashaka na shayo, Kama nyie mnataka kuwa rais wa Tanzania ni lazima muwateteee wanyonge waoteswa na mafisadi wa tra na eapoti

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2009

    Nachukua fursa hii kuweza pia kuzungumzia juu ya suala la uongezaji wa thamani kwa mfano ya magari,wote tunajua kuwa kuna sheria za kibiashara ambazo nchi zote huzifuata na sheria hizi zimekubalika vilevile kwa maana hakuna nchi inayoweza kuwa na sheria zake hususani katika nyanja za kibiashara,mfano mzuri ni kwamba ukokotoaji ili kupata hela ya kulipia ushuru utokana na thamani halisi ya manunuzi kujumlisha na gharama za usafirishaji kwa lugha nyingine CIF ,lakini jambo la kusikitisha sana ni kwamba kwa mfumo wa Tanzania inashangaza kuona jambo hili halipewi umuhimu sana maana kuna wakati TRA huweza kuongeza thamani hata kama una risiti za benki kuonyesha malipo yalivyokwenda,mfano mzuri nilipata kagari kwa bei nzuri kwa $ 2700 za kimarekani lakini cha ajabu ni kwamba ofisa aliyehusika alipandisha thamani mpaka $3700 hivi bila hata kuuliza kwa nini gari hili lilipatikana kwa $2700.Jambo hili kwa kweli inatia mashaka sana kwa maana sina uhakika kama hawa ndugu wanajua maana ya CIF.na cha kusikitisha zaidi walikataa hata na risiti ambazo zimetafsiriwa katika kingereza hii kwa kweli nahisi yaweza kuwa pengine kiburi au ufahamu mdogo wa sheria za biashara za kimataifa kwa maana hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kufanya hivi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2009

    Kwa kweli kama Posta ni weyi sana!
    Nilituma mzigo toka Ujerumani, wao wakamdai niliyemtumia hela kibao wakidai kuwa mimi sikuulipia hela za kutosha. "Can you believe this" yaani Wjerumani wakubali kukupelekea mzigo bila kuulipia heal ya kutosha.
    Najua wantumia risiti za feki ukulipia hanbazo haziko kwenye record za ofisi. "Big Thiefs"

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2009

    Dawa ni maandamano hadi ikulu. Tumechoka na TRA. Kuna mama mmoja mjaluo mama apolo ambaye ni Kama nyang'au yaani hataki hela mdogo. Ukiwa na contena ya milioni 10 anataka rushwa ya millioni 5 ili ulipe laki moja wakati anajenga majumba na majumba magari na magari. Ana roho mbya kaa shetani. Anaye mwane pale londoni ambaye anatanua na fedha zetu wajongo tuamkeni

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2009

    Ukiachilia mbali airport, bandari na posta, pia kuna tatizo la benk za Tanzania pamoja na vituo maalum vya kuchukulia esa kama vile Western Union na Moneygram. Wat hawa wa Western Union na Moneygram nao ni wezi. Siku k=moja nilituma pesa kupitia benk ya exim tawi la Mbeya, wafanyakazi wakaichukua pesa na kuitumia. Nilipomwambia mdogo wangu aende kuchukua pesa hizo, walimwambia kuwa pesa ilitolewa Dar es Salaam nkwa mtu asiyejulikana. Mdogo wangu alihangaishana nao mpaka akawatishia kwenda kuwashtaki kwa meneja wa benki ndipo walipoamua kmchangia pesa hiyo toka mifukoni mwao na kumpatia. Ilijulikana wazi kuwa pesa walikuwa nayo ila walitaka kuila. Watanzania wanaofanya kazi katika sekta za pesa wote wamelaniwa.

    ReplyDelete
  10. Mwenda MpalikozoJuly 29, 2009

    Watanzania ni watu wasio na uzalendo kabisa...kuanzia ngazi za juu mpaka chini ni wizi mtupu...hayo ya bandarini, eapoti na posta ni ncha ya barafu tu...wizi unaanza na wabunge,mawaziri, mameneja wa makampuni na mashirika ya serikali, wizara na kila idara ya nchi yetu. Ni aibu sana kuona jinsi watu walivyo na tamaa na kutokuwa na miiko ya kazi. Wenzetu wakenya pamoja na ukabila wao lakini wamejaaliwa na uzalendo na akili ya biashara na utayaona haya pale unapovuka mpaka. Ofisi zao na uhamiaji ni bora mara elfu za kwetu, watu wanajuwa kazi zao na rasilimali zao wanazifaidi zaidi kuliko sisi tuliojaaliwa kila kitu lakini tumekuwa ombaomba wa kutupwa. Pole kaka Rweyemamu na wewe si peke yako yanayokusibu haya maradhi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 29, 2009

    Mr. Ryayemamu, Kwanza ninakutakia pole kwa dhoruba ulilopitia. Mwaka 89 hao walafi waliuza gari la marehemu baba yangu walipogundua amefariki kabla ya kuli-clear. Pamoja na majina yake kuandikwa kwenye vioo(We have a very unique sir name) aliuziwa mtu mbele yetu. Lakini usikatetamaa watu wanavyozidi ku-share their personal nightmares hatua zitachukuliwa...
    Mdau wa Unyamwezini..

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 30, 2009

    Bongo watu wameshazoea maisha ya mkato mkato huku wakiendelea kufanya wizi na ufisadi. Sidhani kama viongozi wa nchi na hizo sehemu husika wanaona umuhimu wa kuajiri watu waaminifu kwa sababu wenyewe pia ni wezi na wakati mwingine wanakatiwa kitu na kidogo ili wasifanye mabadiliko yeyote. Sidhani kama nchi yetu itaendelea ikiwa mambo kama haya yanaendelea kushamiri na matatizo haya yanawafanya watu wasiwe wazalendo na kuondoa mapenzi kabisa na nchi yao.

    Ukweli siku zote hufichwa Tanzania na kama kuna jambo lolote linaloonyesha lawama kwa Serikali na Viongozi wake basi hata vyombo vya habari huwa hata hawaripoti, hata hapa Globuni kwa wadau, mtu ukiandika kitu kuikosoa Serikali au CCM basi ujue Michuzi ataweka maelezo yako kapuni. Mungu atawahukumu tu siku moja kwa kuwanyanyasa watanzania, najua mko mnatunisha vitambi na kutanua mkivuta pumzi kwa furaha huku mkiwanyonya na kuwanyanyasa walalahoi na wananchi wengine, lakini kumbukeni itafika siku moja hiyo hewa ya kuvuta pumzi haitokuwepo ndipo hapo utakapoona joto ya ardhi ikoje.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 30, 2009

    Kwa mchongo huu wa kibwegebwege namna hii, basi kumbe wa-zanzibari wana kila haki ya kudai nchi yao. Fikiria kama wewe ni mzanzibari na unakumbwa na dhoruba kama hili la Rweyemamu, wakati unajua kabisa kwamba kama bandari ya unguja ingekuwa inaendelea kufanya kazi kimataifa upumbavu huu usingekupata. Lazima ungetaka kudai nchi yako.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 30, 2009

    1. Tatizo ni system ya Tanzania kumuajiri mtoto wa fulani.

    2. Ni system yenyewe ni ngumu usipotoa rushwa akaifuata system lazima utaumia.

    3. Roho mbaya ya kwa nini?

    4. System ya Tz usipoiba halafu ukastaafu bila kitu unaonekana ulichezea madaraka, aliyeiba na kula rushwa ndio anathamanishwa, uongo?

    Tuendeleeni tu hivyohivyo, uzalendo wa nini? Watunga sheria wenyewe si wazalendo.

    Mtoto wa fisadi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 30, 2009

    RWEYEMAMU MANENO YAKO YA KWELI KABISA.
    TANZANIA HIVI SASA NI AIBU NA INAJULIKANA HATA KATIKA MITANDAO YA KITALII INAYOTAMBULISHA NCHI KWA KIFUPI KWAMBA NI NCHI ILIYOJAA RUSHWA KUANZIA VIONGOZI WA JUU HADI WA CHINI.
    DAWA YA KUVUNJA RUSHWA NI KUTOKUWEPO KKWA HIZI IDARA ZA TRA AU MAMBO YA KULIPA USHURU WA GARI BONGO.
    KAMA SERIKALI INATAKA KUPATA FEDHA ZA USHURU WA MAGARI AU MIZIGO INAYOTUMMWA TOKA NJE YA NCHI, ADA ZILIPWE KWA MAWAKALA WA MIZIGO WALIO NJE YA NCHI AMBAO WATAINGIZA FEDHA KUPITIA KWENYE AKAUNTI MAALUM YA SERIKALI NA RISITI KUAMBATANISHWA NA CHETI CHA USAFIRISHAJI KAMA UTHIBITISHO WA MALIPO.
    WATUMAJI MAGARI LAZIMA WATAMBULIKE AU WAJIANDIKISHE KWENYE WIZARA HUSIKA ILI KUEPUSHA HUU UNYONYAJI WA NCHI UNAOFANYWA NA WAZALENDO.
    VINGINEVYO HAKUNA KITAKACHOLIPWA KWANI FEDHA ZINAISHIA KWA WALEVI.
    KIKWETE ALIDAI ANA MAJINA YA WATU WOTE WANALKULWA RUSHWA. MBONA HAWATAJI KAMA ALIVYODAI AWALI?
    IKISHINDIKANA SERIKALI ITAFUTE WAFANYAKAZI WAZUNGU KUHAKIKISHA MALIPO YA KODI YANAPATIKANA NA WATU WANACHAJIWA KIHALALI. NDIYO BORA IWE HIVYO KWANI WABONGO NI WANYONYAJI WAKUBWA WA NCHI KULIKO WAZUNGU WALIOKUWA WAKINHYONYA NA KUPULIZA! WEZI NYIE...
    WEZI HAOOO, WEZI HAOOO, WEZI HAOO...YUPO WAPI...KAMATA PIGA UA HUYO...NYAMAFU WEZI WAKUBWA HAMNA HATA HAYA.
    LEO MNADAI MATIBABU BURE, ELIMU BURE HUKU KODI ZINAISHIA KWENYE PUBS...WEZI HAOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 30, 2009

    Mr Rweyemamu pole kwa yote,mimi naishi canada na matatizo kama hayo yameshanitokea hata sikumbuki ni mara ngapi,nimekuwa nje ya tanzania kwa miaka 9 sasa kwa mara ya kwanza nilirudi nyumbani 2007 nikitumia passport ya canada kwa kweli sikupata matatizo yoyote.February 2009 nilikuja tena nyumbani kuitembelea family cha ajabu wakati wa kuondoka walinizuia na kusema kuwa passport yangu ilikuwa fake na wakataka niwape kitu kidogo ambapo nilipinga cha ajabu ni kwamba passport yangu ina visa zaidi ya moja ya bongo baada ya kuwatishia kupiga simu kwenye ubalozi wa canada waliamua kuniachia.kuhusu kupoteza vitu kwenye mabegi hili ni jambo la kawaida na tabia ya jamaa kuombaomba imezidi mpaka inachefua kwa kweli.kwa kweli nakumiss home lakini nikifikiria misukosuko yake wacha nitulie huku tu.....godbless tanzania.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 30, 2009

    Nakubaliana nanyi ila "NANI WA KUMFUNGA PAKA KENGELE"

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 30, 2009

    ole wenu hapo JNIA ninazawadi ya Rais ila siwaambi yupi wa ZNZ or Bara, nakuja mwezi October 2009 kumletea, ole wenu mkichomoa kwenye Begi, vibarua mtakuosa na mtanyea Keko, ndege BA, mtajuuuuta kuiba. thanks

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 30, 2009

    poleni wenzangu kwa matatizo mliyoyapata kutokana na nchi yetu yenye AMANI NA UTULIVU,HATUPIGANI HATUNA VITA ILA HALI YA NCHI YETU SI NZURI ,RUSHWA IMEOTA MIZIZI KILA KONA.WEZI KILA MAHALI.inatia aibu,HAMJIULIZI KWA NINI PIA WATALII WENGI WANAPITIA KENYA KUINGILIA TANZANIA??SABABU KENYA NI RAHISI ZAIDI NA HAKUNA LONGO LONGO.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 30, 2009

    ole wenu nyie mnaowaibia watu kutoka ughaibuni kwa maana arobaini yenu imekaribia, maana watu hawa wanaposegeza karibu karibu ujumbe huu na vilio vyao ili utufikie sisi wizara nyeti, mtanyea Keko.
    na huko mtasema hakika tunajuuuuuta kuiba kwenye mabegi yao vitu vingi, na mawakili wenu watawalia fedha zenu bure huku wakiwapa matumani ya bure na kuwalia fedha zenu pia na majina yenu kubakia kwenye Magazeti, TV, Radio, wabunge, mawaziri na Rais.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 30, 2009

    Nakuunga mkono Bwana Mwenda, nikweli wabongo hatuna uzalendo kwa watu walioko ughaibuni wanalitambua hili, nalaiti kama tungekuwa tunaweka uzalendo mbele hata ufisadi usingeendelea kuchanua kiasi hichi. kila idara serikalini kumeoza, yanii ukikaa chini ukifikiria unapata jibu kuwa Bongo inamilikiwa na wajanja wachache, sijashangaa pale JK aliposema kwamba 30% ya pesa za bajeti zinakwenda mikononi mwa wajanja. sijui hao wajukuu watakuta nini.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 30, 2009

    Kikwete unaposisitiza watanzania walio nje wawekeze nyumbani usikie kilio cha watu

    Na ni pigo kwa taifa kwakuwa tunapitishia mizigo Mombasa na ni easy and cheap

    Do something Mr. President
    Please please please do
    Futa dhuluma na mateso ya makusudi ya wananchi.
    Tunalia tunaumizwa Tumechokaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 30, 2009

    Mdau Rweyemamu, Shumaramu waitu, mpola bhojo! kwata amashaija!
    Kama watu wanakuwa wapumbavu kiasi hicho basi si vibaya kutumia njia mbadala za Mombasa na kwingineko! Mimi mwenyewe nilituma picha kwenye box kubwa na mpaka sasa hivi halijafika! hiyo ndio Tanzania, posta na Bandarini! Hawa watu wanahitaji hatua kali sana! They should get fired!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 30, 2009

    yaani nashukuru sana kwa kuongelea swala hili kwani tumechoshwa na tabia hii kabisa sio siri mpaka tunaogopa kutuma chochote. mim nilimtumia ndugu vitu tena nina kila kumbukumbu lakini vimepotea kimaajabu ukienda kuuliza unaambiwa havijafika mapaka sasaivi nimeshakata tamaa kama sina hera ya kutumia dhl bora nikae nao kama nikipata mtu anakuja bongo aje nao unajua kaka michuzi inafaa utufikishie ujumbe kwa vyombo vinavyousika kwani tunaumia sana kwa watu wachache wenye wivu na wasiopenda kujituma na tunanyanyasika sana na hivyo vitengo vilivyoorodheshwa.

    ReplyDelete
  25. Mi kila leo nasema hapa, nchi hii imeshaoza kuanzia juu hadi chini. Dawa ni moja tu, apatikane mtawala wa kijeshi, na sio eti mwanajeshi mstaafu, bali mjeshi wa ukweli, hapo ndo watu watatia akili. Yaani imekua too much. Watu hawana imani ya dini hata chembe, kazi kujirimbikizia mapesa tu kwa migongo ya walal hoi. Ukiishi huku nchi za watu hadi mtu unaona raha, hakuna upuuzi upuuzi, kila kitu kinafata system.
    Kama asemavyo rwey, mi mwenyewe niliingiza gari wakadai eti hiyo bei sio, nimefoji document, ilmradi tu niwape rushwa, na mi nikasema rushwa siwapi, bora pesa iingie kwenye mfuko wa taifa! WIZI MTUPU!! Moto wa jehanam unawasubiri kwa hamu, na hawa ndo watakao kuwa kuni za motoni!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 30, 2009

    mh jaman hiyo bandari ya bongo ndio uozoo kabsaa
    bora tuhamie mombasa wajameni
    sylvester wa nbc ebu wasimulie wadau yaliyokutokea!!! aibu jamani yaan wizi mtupuuuu
    jk

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 30, 2009

    Kama kuna makampuni yanakera na yamejaa watu wasio na huruma wa mali ya wanyonge ni pamoja na posta, bandarini huko, tanesco,TRA na mengineyo.
    Sababu kubwa ni kuwa ukichunguza sana utaona wengi walioajiriwa hapo kwenye vyeo nyeti ni watoto wa wakubwa.
    Siku moja nilikutana na jamaa ambaye namfahamu, form six yake alidunda ziro, akaniambia yupo tiaraei, na muda huo alikuwa anajiandaa kwenda ng'ambo kusoma! Jamaa huyu namfahamu sana, ana-akili za kutafuta hela kwa njia za mkato, ajabu kabisa. Sasa hao wapo wengi na wengi mnawajua, na wengine wamezamia kwenye siasa, mwisho wa siku mnawapa kula!
    Ukienda tanesico, huko nakumbuka nilivyotaabishwa kupata umeme, nilitumia vishoka,ambao ndio kazi yao ukikwama kupata umeme, bili zinakuja za ajabuajabu, umeme wenyewe ni mwendo wa mgao.
    Posta huko ndio kabisa,kila nikitumiwa kizawadi,najiuliza mara mbili, jinsi ya kukikomboa , na je kweli nitakipata! Poleni sana wabeba maboksi mnatujali kwa vizawadi,lakini mjue zawadi hizo inabidi tugawane na hawa jamaa,au watuzulumu kabisaaa!
    Kwa ujumla, system yetu ni mbovu, sehemu nyingi, kwasababu watu waliajiriwa kiudugu, na wengi ni watoto wa wakubwa. Inahitajika mabadiliko, na mabadiliko hayo hayawezi kuja kama zawadi. Ni wewe na mimi, tuwasomeshe watoto wetu hadi ngazi za juu, ingawaje ni kwa shida, manake, wenzetu wameshawahi, kila shule nzuri ya pesa wamewekeza huko, watoto wao ndipo walipo,na hao ndio taifa la kesho.MMMh, tunasafari ndefu.
    Elifu mbili na kumi inakuja, najua bado hatuwezi kugeuza misimamo yetu, lakini hapo ni sehemu ya kuonyesha kuwa tumechoka,au bado tutaendelea. Nawaombeni nyie mlioko nje muwe changamoto la kueleimisha nini maana ya vyama vingi na faida yake ni nini. Nilitegemea kuwa nyie mtatoa changamoto, lakini mmmh,kila siku matawi yanafunguliwa, je ni nani wakusaidia upinzani. Kwasababu upinzani sio vita au dhambi, ni jinsi ya kujikwamua na kurekebisha pale mwenzako alipokosea, sasa ni nani wa kumkosoa mzee mzima, kivitendo, hayeni, kufa hatufi lakini chamoto tutakiona!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 30, 2009

    Tanzania imekuwa sehemu ya wizi na uonevu. Watu hawana aibu kuomba rushwa na kunyanganya. Mtu anatafuta kazi sehemu ambazo ataweza kudhulumu na kuiba na kwa kuwa viongozi wote wana tabia hiyo basi hamna anaeweza kumkataza mwenzake. Inashangaza kuona mtu kaanza kazi miezi sita ilopita leo ana magari 2 nyumba kubwa ya kifahari na anaishi maisha mazuri. Swali Kwa mshahara gani? ni wizi mtupu na imani zetu zimeshuka ndio maana vijana wengi wamekimbia ugahibuni na walo baki wanajiingiza kwenye siasa sio kusaidia noooo ili na wao wapate kuiba, maana kuanzia juu mpaka chini wote ni wezi.

    Sasa nini tufanye, Obama kasema maendeleo ya africa ni kwa wa africa wenyewe, sasa jee tutaendelea au ndio tunaibiana tu.

    Mimi sina imani na nchi hii kwa lolote na sina mpango wa kurudi maana kitakachobaki watanifukuza kazi maana sitokubali kuona mtu anaiba....

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 30, 2009

    Ndugu wana globu. Matatizo ya aina hii pia yanapatikana katika usafirishaji wa fedha kutoka nje kwenda Tanzania. Mimi binafsi nimetuma pesa na nimekaa wiki bili bila kuingia katika account niliyotuma. Nilipokwenda kwenye bank niliyotuma wakanihakikishia kuwa fedha hizo zimeingia siku ile ile niliyotuma na NBC wamehakikisha kupokea pesa hizo. Unajiuliza kwa nini ichukue siku 13 za ziada ndio pesa ziingizwe katika account. Tena hapo ni baada ya kufuatilia na kutumiwa ujumbe kuulizwa kwa nini hizo pesa hazijaingizwa katika account husika. Ningaliomba globu ya michuzi akatufikishia kero hizi kwa watu wa NBC kama alivyofanya kwa ile ya airpot.

    Mdau kutoka Sweden

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 30, 2009

    tahadhari kabla ya ajali...........
    ni bora kuweka vitu vya thamani katika hand luggage.vitu kama simu ,laptop,camera,video games,saa n.k maana kila wakati unakua navyo mwenyewe na hao wezi hawatapata chance ya kuiba.ukikosea step ukatia kwenye mzigo mkubwa watakuumiza tu....

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 30, 2009

    mie ni mombasa tu hata kama watanidai rushwa at least mzigo wangu nitaupata salama. Tanzania inanuka! i hate it with my whole heart! I wish I was born in Kenya! viongozi wuet hovyo! ni kwenye maparty tu

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 30, 2009

    We Michuzi, ninavyoamini mimi wewe ni mwana habari na popote pale unaingia na kukubalika,unapopublish maoni ya watu,hivi unayatoa tu ili watu wasome au na wewe mwenyewe unayafanyia kazi kuisaidia jamii?????!! au unatoa tu ili mradi watu wamesoma inatosha, nyinyi wenyewe mnatusema wabeba mabox life yetu ni ngumu ni bora aliyeko nyumbani, ni kweli pengine twahangaika sana nakutafuta maisha huku ugenini, japo pengine si wote, sasa kwa nini watu wanapojinyima na kutuma vitu walivyopata kwa ajili ya huo ubebaji mabox ambao mnatuponda nao hapo nyumabani nyie tena ndio mnakua wa kwanza kukwapua vilivyotumwa au vilivyo ndani ya mabegi ya watu?? tuachieni vitu vyetu tulivyopata kutokana na jasho la ubebaji mabox, nyie mlio na maisha bora na kazi bora,tafuteni vya kwenu vinavyolingana na hadhi zenu, NAWE MICHUZI, KAMA KWELI NI MTOA RIPOTI MZURI ILI JAMII IRIDHIKE NA KAZI YAKO NA KUONA KWELI WEWE NI MWANAHABARI ULIYEKAMILIKA, HIVI VILIO VYOTE NA MALALAMIKO YA WATU HUMU NDANI TUNAKUOMBA UENDE KATIKA IDARA HUSIKA NA KUONANA NA WAKUBWA WA IDARA UKIWAONYESHA HAYA MALALAMIKO NA KUWAFANYIA INTERVIEW AMBAYO UTAIRECORD NA KUTULETEA HAPA ILI TUONE HASA WANACHOFIKIRIA AU KUONGELEA JUU YA ADHA HII, ILI SULUHISHO LIPATIKANE, NA KWA KUMALIZIA MJULISHE NA HUYO JK WENU, HALI HALISI YA WATENDAKAZI WAKE, NA AFAHAMU NI KWA NINI WATZ WALIOKO NJE WANAUKANA UTZ WAO, ILI ANAPOKUA KATIKA ZIARA ZAKE ZA NJE AACHE KUWAAMBIA WATZ ETI WARUDI NYUMBANI KUWEKEZA, AJUE NINI AU KITU GANI KINAWAFANYA WATZ HAWATAKI KURUDI HOME, kuna watz wengi huku wasomi ambao wamekabidhiwa au kuaminiwa kupewa kazi za maana sana huku nje watu kama hao wangekua nyumbani wangeliendeleza guruduma la maendeleo vizuri sana, hakuna mtu asiependa kwao au kuchukia kwao, lakini mambo kama hayo ndio yanafanya watu wanagoma kurudi.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 30, 2009

    jamani kama ukitaka kutuma gari,ni bora kabisa ukatumia bandari ya ZANZIBAR,angalau utaikuta na redio na vifaa vyake vingine,na hata usumbufu sio mkubwa.DAr port ni kichaa.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 30, 2009

    Inatia hasira.Haya yote malalamiko ya watu uongozi upo wapi? aibu tu.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 30, 2009

    posta na sehemu hizo kweli wizi umeshamiri na udokozi. mimi mwenyewe kipindi bado nikiwa tanzanianiliwahi kutumiwa mzigo kutoka USA na rafiki yangu,sasa posta walipo uona ule mzigo sijui walidhani kuna electronics ndani,wakaufungua cha ajabu walipokuta ni vitabu tu vimejaa tena vya kidini wakachoka,nilivikuta lakini mzigo ulikuwa umefumuliwa na kupekuliwa uko hovyohovyo.
    pia nikatumiwa pesa usd 2000 kupitia western union, nilipofika posta,badala ya kuniambia tangu mwanzo pesa hazipo,wakasubiri hadi najaza info zangu zote,kisha ndo wanasema aah samahani pesa hapa haipo labda ujaribu tawi jingine au uje jioni. NIKAJUA HAPA WANANILENGESHA ILI NIPORWE KISHA WAGAWANE DOLA ZANGU 2000. nikatoweka kama mshale nilipozichukulia najua mwenyewe na kwa muda gani.
    watu wamejaa tamaa sana! wakiona kitu kilichovujiwa jasho na mtu wanataka mgawane utadhani walikuwa wanakusaidia kutafuta.
    najiandaa kuingiza gari yangu na vifaa kadhaa vya electronics, mtu aviguse aone cha moto,mimi wala sikukawizeni nyambafffff zenu!

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 30, 2009

    WIZI MTUPU...RAFIKI YANGU ALI IMPORT GARI NDOGO YA THAMAN YA $2,200 GARI IMEKAA MIEZI 3 CUSTOMS/BANDARINI, NA MIMI NINA KAGARI KANGU NILINUNUA $6,200 JAPAN WAKA UPLIFT HADI $10,500, NIKATUMIA WIKI MBILI KUJIBIZANA NA TSCAN NDIPO WALIPOPUNGUZA HADI $8,500, NIKASHINDWA KUITOA, NIKAAMUA KUIPELEKA BONDED WARE HOUSE ILI NIJIPANGE UPYA, PROCESS YA KUIPELEKA BONDED WARE HOUSE NIMETUMIA MWEZI MZIMA NA BADO IKO PORT, SASA SWALI KAMA NILISHINDWA KULIPA USHURU WOTE WANAOUTAKA, HIYO STORAGE CHARGE NITAWEZA? WIZI MTUPU WALAANIWE....SWALI LA PILI HAWA TICTS/KARAMAGI WAMEGOMA SIKU MBILI, SERIKALI IMEINGIA HASARA YA BIL. 2, KUMBE HIYO KAMPUNI INAINGIZA BIL. NGAPI KWA SIKU 2? JE TANZANIA PORT AU SERIKALI HAIKUWA NA UWEZO WA KUAGIZA HIZO CRANE ILI MAPATO YANAYOTOKANA NA KUPAKUA MAKONTENA NA STORAGE YA MAKONTENA IKAENDA SERIKALINI? NAWASILISHA.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 30, 2009

    Kila nikiamka, nashukuru nimeondoka na shida za Tanzania kuja hapa ulaya. Naamka na umeme wangu na maji safi. Wizi kupita kiasi Bongo, halafu kinachonisikitisha zaidi utaona wadau wanawapigia makofi sana viongozi wabovu kwa kufungua ofisi za CCM nje. Hata ukinilipa dola elfu 10, sitaenda kupoteza muda wangu.

    ReplyDelete
  38. Culture of silence na kuogopa kulipiziwa kisasi ndiyo vinatafuna TZ. Rais anaogopa, waziri mkuu anaogopa, waziri anaogopa, katibu mkuu anaogopa, mkurugenzi anaogopa, mkuu wa mkoa anaogopa, mkuu wa wilaya anaogopa, mfanyakazi wa chini anaogopa, polisi anaogopa, MWANANCHI WA KAWAIDA NDIYO KUNGURU kabisa. Sasa nani abadilishe huu utamaduni wa woga?. Jibu ni rais wa nchi aanze huko huko juu, kila mtu ataogopa kuwa asipomwajibisha wa chini yake atawajibishwa yeye. Yaani hii ni "Domino effect" Rais akianza tu ngoma inashuka chini.

    Mh! Rais fukuza kazi wakurugenzi wote wanaolalamikiwa na kuthibitika kweli wamelala. Mbona nchi yetu leo ina nguvu kazi kubwa tu zinazurura mitaani kwa kukosa nafasi za kazi ili wajenge nchi yao?. Kama ulimtimua Mnali basi nina hakika bandari na TRA na DIA hapakushindi.

    Achana na washauri mafisadi wanaokutisha kwa maslahi yao binafsi. Wewe huna mbia, wabia wako ni wapiga kura walikuchagua hivyo wasikilize wapiga kura fukuza hawa watendaji wabovu.

    "Yote mazuri yaliyofanyika katika utawala wangu, yalikuwa yetu, ila mabaya yote yaliyofanyika katika utawala wangu yataitwa yangu"-Mh Ali H Mwinyi.

    Hivyo basi malalamiko yote haya ya ubadhirifu nia yako Mh-Rais fukuza wote tuanze upya!

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 30, 2009

    Yaani inasikitisha sana kuona wafanyakazi wa TRA,Posta,Bandarini n.k wamekuwa ni waroho wa vitu na pesa,Mtu ukienda nyumbani basi ukishafika uwanja wa ndege tu roho inaanza kudunda, sijui kama mtu utaupata mzigo wako au la?na ukishaupata begi lako tu,sasa unafikiria ukipita pale kwa watu wa ushuru eti wanaanza kukuuliza je una zawadi yeyote?kwani wao wanafikiriaje mtu utoke mbali kweli na haujaonana na familia zako kwa muda mrefu halafu usibebe zawadi?wao wenyewe wakisafiri kwenda vijijini au mikoani tu wanarudi na zawadi kwa familia zao!Je sisi tunaotoka mbali iweje tuende mikono mitupu?Ni ufinyu wa elimu na upeo wa maisha mdogo waliokuwa nao,na kuanzia ngazi za juu hadi chini wengi wao ni wala rushwa tu!Ebu angalieni weekend ikishafika watu wanavyojazana kwenye mabaa kunywa na kula nyama choma,kwa mshahara upi waliokuwa nao ili waweze kujichana hivyo?kama siyo Rushwa na wizi ni nini?Ni aibu tupu wala haipendezi nchi nzuri kama Tanzania yenye kila Neema Mungu ameijaalia, lakini baadhi ya watetaji wake ni wabovu na hovyo kabisa!

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 30, 2009

    There is no hope in Tanzania! Look at what Tanzanians are saying!

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 30, 2009

    Ina maana wahusika haya matatizo hawayaoni jamani kama kuna vitendo vichafu na vyenye kufedhehesha Watanzania na wageni?Hii sasa imezidi watu wanajinyima kile kidogo wakipatacho kwenda kugawana umaskini na jamii zao watu wanaamua kufanya mambo ya wizi wizi tu?Tunaomba Serikali yetu tukufu ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania ichukue hatua kali na ya haraka katika kuondoa huu uozo uozo!Nakupenda kwa Moyo wote Tanzania!

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 30, 2009

    Tatizo ni kwamba Tanzania tuna institutionalized corruption. Bila kuwa mwizi hauwezi kupata kazi TRA Airport au Bandarini. Kamanda wetu hajui haya kwasababu yeye akitokaga kuzunguka dunia nzima kama kawaida yake anakuta mizigo yake inamsubiri. As long as they don't steal his stuff he doesn't care. Ama kweli Ari mpya...

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 31, 2009

    Silaha na ukombozi wa haya yote upo mikononi mwako, na si siku nyingi zimebaki 2010 ndipo utaamua mwenyewe kama kweli una uchungu utauonyesha siku hiyo lakini kama nikulogezewa endeleeni kufungua matawi! Labda nyie mnaofungua matawi hamtaibiwa,labda iwe hivyo...

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 31, 2009

    mi hata sioni wa kumlaumu zaidi yetu sisi wenyewe.hivi kweli mnadhani rais hatambui matatizo haya? yeye ni mwanasiasa kama wengine,anawaambieni mnachotaka kusikia.akiwapoza kwa hotuba,mnashangilia kama mtoto kapewa pipi.
    kwani kwenye ile ziara ya california,watu walishindwa kumuuliza maswali ya maana,wanabaki kujichekesha kwa kila neno analoongea. anyway,may be hata kama wangeuliza asingejibu chochote kama kawaida yake....
    na nyie mlio nje,msiniambie kwamba mnaweza kununua vitu vya zaidi ya $300 halafu unashindwa kukilipia $70 kwa dhl,ups au fedex ili kifike! that's how i do it!!

    ReplyDelete
  45. Ninaanzisha blog ya watu kuwaweka hadharani kwa majina (hata ukisema mama Apolo wa kijaluo inatosha!) watu wanaokla rushwa; pia watu waseme mali zao zinazojulikana!

    Dah, jamani yule mama wa customs pale sehemu ya vifurushi posta mpya ni anazitengeneza sana. hakosi milioni kadhaa per day. Yule jamaa mlemavu na kikofia chake ni msaidizi wake!

    ReplyDelete
  46. Pole sana Rweyemamu. Nami yalinikuta hayo kama yako pale Bandarini. Waliniibia vitu karibu robo tatu. Hivi sasa nikituma container natumia Mombasa.
    Tena walivyo wajinga hawaelewi kuwa jinsi tunavyokimbia bandari ya Dar es salaam kupitishia mizigo yetu ndio na wao ajira zao ziko hatarini. Maana sasa hadi wamalawi, wazambia na wote wanaopitishia mizigo yao Dar wanaamua kuhama.

    Taifa linakoseshwa mapato na wajinga wachache

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...