anko nanihii akipeana mikono na mwana wa mfalme wa mambo ya globu ndesanjo macha septemba 8, 2005 kwenye ukumbi wa finlandia hall huko helsinki, finland, hii ikiwa ni taswira ya kwanza ya toka kuanzishwa kwa globu ya jamii ambapoo jumamosi baada ya hii ijayonitatimiza miaka mitano kesh! (vekesheni zilianza kitambo ati!!)
kunradhi wadau lakini naomba niseme wazi kwamba kama si ndesanjo macha hapangekuwa na libeneke na anko nanihii wala asingekuwa nanihii unayemjua leo.
kwa lugha ingine huyu ndiye aliyefanikisha kila kitu katika mambo haya. mtembelee uone vitu vyake kwa kubofya
HAPA na HAPA na HAPA.
ukishamtembelea kote huko utajua ni kwa nini nammaindi sana ndesanjo macha ambaye kwangu mimi ndio kama mama na baba wa libeneke. vile vile ukimsoma ndesanjo macha kwa makini utapata jibu la ufanyeje kuanzisha libeneke la globu pamoja na mambo mengine. huyu mwana wa mfalme wa libeneke hana uchoyo, anapenda kila mmoja wetu aendeleze libeneke...
endapo kama mambo yataenda kama anko nanihii alivyopanga basi kutaandaliwa bash la ubwete kusherehekea hepi besdei ya miaka mitano ya globu ya jamii. kama vipi angalau wadau walitambue hilo, kwamba globu hii inajihisi ina deni kubwa kutoka kwa wadau walioifikisha hapa ilipo.
si jambo dogo ama la masikhara kwani miaka mitano ya libeneke ni umri tosha wa mdau, na kama inavyoeleweka angekuwa mtu basi saa hizi angekuwa darasa la kwanza. na ndivyo globu ya jamii ianavyojisikia kwa sasa. yaani ndio kwanza safari imeanza, na miaka mitano ni cha mtoto.
siku ya siku ikiwadia ya hepi besdei anko nanihii atatoa hutba rasmi, lakini kwa sasa si vibaya kuwashukuru wadau wote kwa kampani yao muda wote huu, kwani safari ina mabonde, miteremko na kashkash kibao ambazo kama una roho ndogo unaweza kuachia bodi.
nawashukuru sana wadau wanaoendeleza libeneke kwa kutuma taswira ama lolote lile ili tushee nao kwenye globu ya jamii. na hapa anko nanihii anaomba kwa unyenyekevu kuweka jambo moja wazi. globu ya jamii haibaugui na wala haichagui. kama mdau una lako jambo ambalo hakichafui hali ya hewa basi litabandikwa tu. likitupwa kapuni ujue umenoa stepu.
halii hiyo ya kutochagua ama kutobagua inalenga sehemu zoteza itikadi iwe dini, siasa, jinsia na hata libeneke la kufurahisha baraza tu. nasema hivi kwa sababu kuna minongóngo kwamba globu hii inapendelea chama fulani tu cha siasa ama imani fulani tu ya dini.
naomba nikanushe tuhuma hizo nzito na kukazia kwamba endapo hao wanaoona hawapewi kipaumbele na globu ya jamii hawaleti taswira na khabari zao kifanyike nini????
hapa kwa ufafanuzi ni kwamba kila jamii iko huru kuleta wakitakacho kwa kutumia
na kisha endapo kama kitaminywa (na hapa kiwe hakichafui hali ya hewa) ndipo mdau ama muosha kinywa ulalame.
ANGALIZO: globu ya jamii haibagui itikadi ya dini ama siasa, jinsia, aman mada ama libeneke lolote lile lisilochafua hali ya hewa. hivyo endapo wewe ni Mkristo, Mwislamu, Mpagani, CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, TLP na kadhalika lete tutaswira na khabari tuendeleze libeneke. Ila usilalamike wakati wenzio wanaleta wewe unakaa navyo huko uliko.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2009

    Freddy Macha ninamkumbuka sana maana miaka ya '80 alichapisha kitabu kiitwacho "Twe'zetu Ulaya". Nilikinunua nikiwa shule ya msingi na tokea hapo ndoto zangu zilikuwa ulaya na sasa nipo Ulaya!Potelea mbali usiulize ninfanya nini!
    Big-up Freddy!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2009

    Uliyoyasema Michuzi tunayapata lakini!!ujue kwamba haya unayaandika baada ya watu weengi kuona na kulalamika kwamba umeanza kubagua watu flanikutokana na misimamo yao,.kwa mfano wewe ukisha tundika maswala ya mikutano ya CCM badae wadau waanze kuchangia akioneka mdau ambae ni tofauti na anayetoka au anayesifia chama cha CCM unabana maoni yake sio fleshi tunahudhunika sana.Mzungu anasema kwamba kila kitu kina upinzani wake,na bila upinzani hakidumu,kwasababu hakuna wakukosoa makosa mbalimbali ndani yake.Sasa wewe ukishaanza kutuletea maswala ya kutundika chama cha watu wanaotuliza uwanja wa ndege wa kwetu na mababu zetu! eti CCM UK haina faida wala sio maendeleo bali na ufisadi tu .najua ni hii unabana tu.ila uyajue yote hayo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2009

    Tuulize ya nini wewe mdau wa 11:37 kubwa utakuwa unamadabo shift usiku na mchana ya kuwalaza wazee na kuwaosha. Mwaya unapata thawabu kutunza wazee sio pesa tu

    ReplyDelete
  4. Michuzi wewe ni bonge la mjanja acha tu, very smart and genious. unajua kumkaanga pweza na mafuta yake. hahahaaaaaa. kaswali kadogo je pesa za matangazo unamkatiaga nayeye?..nikizidi kuuliza sintaona mwanga wa jua.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2009

    acha upumbumbavu wewe michuzi mara ngapi tunaleta ishu zikiigusa CCM tu au zikimgusa Kikwete unazibania???!!! acha kujifaragua bwana. na hii bania kama kawaida yako.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 30, 2009

    Kwa lugha uliyotumia hata hapa tu wewe Anony wa 07:48 jul 30 ni wazi kwamba comments zako huwa zinachafua hali ya hewa...umesema hapo " acha upumbavu wewe michuzi" hiyo ni lugha kali sana kimaadili, unaweza ukapingana na mtu bila kutumia kugha kama hiyo!!! hata ingekuwa mimi nisingeruhusu lugha kama hiyo kutumika kwenye blogu yangu! kwani ni lazima usome na kuto comments zako kwenye blogu hii? kama unaona michuzi unakubania na lugha yako chafu si uende kwenye blogu nyingine? Michuzi habagui lugha na comments zenye manufaa na mtazamo mzuri kwa jamii...Acha lugha ya jazba!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 30, 2009

    Mimi mwenyewe nimetuma jana email yangu kuhusu kumbukumbu ya baba yangu cjui haijafika? au kuna watu special wanaotolewa taarifa zao haya ni hayo tu hata nikisema sana kama imebaniwa imebaniwa tu lakini mi ni mdau mkubwa wa blog yako labda mpaka tuwe maarufu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 30, 2009

    KAKA MICHUZI, uwe mkweli, nisemi tuu ili nioshe kinywa ila UKWELI una upendeleo wa kidini na mambo mengine, HUO NDIO UKWELI, nakubaliana nawe kabisa kuna lugha za kuchafua kinywa nakupongeza kwa hilo hata mimi sipendi na huwa sioonge lugha za kuchafua hali ya hewa MICHUZI JITAHIDI KUWA FARE usiegemee upande mmoja. ASANTE LIBENEKE JUUUUU

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 30, 2009

    Yanga na Simba Je?
    GJK

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 30, 2009

    Sasa mlitaka michuzi apendelee Man U wakati yeye ni bwawa la maini na blog ni yake!!! acheni hizo nyinyi anzisheni blog zenu! blog yake ndiyo maana anaiita Issamichuzi.blogspot.com...kuna vitu michuzi lazima avipendelee...comments za kuikashifu au kuicheka Liverpool inapopewa kibano haziwezikuwekwa humu...never!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 30, 2009

    Hongera sana michuzi ila naomaba huache ubaguzi watu wengine tunakutumia utuwekee matangazo yetu kwenye blog yako lakini matokeo yake tunasubiri uweke au utupe jibu lakini ua unaamua kukaa kimya mbona watu wengine unawawekea mtangazo yao hao wanatoa kitu kidogo? tujulishane bwana ni hayo tu mze wa libeneke mambo mengine mswano

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 30, 2009

    aku ka michu sa nyingine unabania hata msaada tutani.sasa sijui hiyo hali ya hewa imechafuliwa vp kumtafuta rafiki au ndugu mliyepotezana miaka miiingi.I was sure kwa kuleta ombi dogo tu la msaada tutani ningelimpata shogangu.Please-

    ReplyDelete
  13. bantugbroJuly 30, 2009

    Mamboz,

    ndugu mtoa maoni wa kwanza kabisa, huyu bwana sio Freddy bali ni Ndesanjo yeye ni mdogo wa Freddy Macha.

    Kwakweli Ndesanjo ni mtu ambaye hana uchoyo katika kuliendeleza libeneke lolote liwe la kiblogu ama jambo lolote lile lenye manufaa ya kijamii.

    Namfahamu Ndesanjo kwa miaka mingi sasa tukiwa ughaibuni na pia nyumbani ingawaje tumepotezana kidogo katika mihangaiko ya kimaisha hivi karibuni. Kwakweli nimefurahi sana kuona Michuzi ukitoa ushuhuda wako.

    Amani baba Ukweli.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  14. HEPI BASDAY BROOOO!!!WE NDO STELIING, SALUTE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...