Ndugu Michuzi,ninakusalimu sana wewe pamoja na kikosi kizima cha blog yetu hii ya jamii. Kwa niaba ya kamati nzima ya wachungaji wa makanisa mbali mbali yaliyopo hapa Dallas Metroplex ninapenda kuwakaribisha watu wote katika semina kubwa ya neno la Mungu.
Watumishi wa Mungu Apostle VERNON FERNANDES na mke wake Pastor ANN kutoka Tanzania ndio wasemaji wa semina hii.Hii ni semina ya kwanza kuandaliwa na wachungaji kutoka mataifa mbali mbali kwa ajili ya watumishi kutoka Tanzania.
Tunaomba kila mtu atakae soma tangazo hili amjulishe mwenzake.Semina hii itafanyika kuanzia tarehe 21 mpaka 23 mwezi wa nane. kwa wale ambao wanahitaji malazi naomba wawasiliane nasi kwa namba hizi hapa;
Pastor Emmy; DaySpring International Bible Church; 214 868 5151
Pastor ; Nosa Arise&Shine Church; 214 448 3135
Pastor Pastor Amen; Dayspring International Bible Church; 214 545 8488
Evangelist Julius; All Nations Church; 214 226 8249
Pastor Absalom Nasuwa; Umoja church;214 554 7381.
Katika kufanikisha semina hii, jumuia ya watanzania waishio Dallas imeandaa chakula maalumu kwa ajili ya kuchangia mkutano huu siku ya ijumaa tarehe 11 mwezi huu.Unaweza kuwasiliana na Dada Jesca au Pastor Absalom kwa maelezo zaidi kwa namba hizi;
972 506 7780, 214 554 7381

Karibuni sana.
Pastor Absalom Nasuwa
Umoja Church
12727 Hillcrest Road
Dallas Tx 75230.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2009

    Je Absalom Nasua ni mchungaji kutoka Babati.Ni kama hili jina nalifahamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...