HABARI TOKA DODOMA ZINASEMA TRENI MBILI ZA MIZIGO ZIMEGONGANA USO KWA USO ASUBUHI HII KARIBU NA STESHENI YA ZUZU NJE KIDOGO NAN MJI WA DODOMA KATIKA RELI YA KATI.
KWA MUJIBU WA MGANGA MKUU WA MKOA JUMLA YA MAJERUHI SABA WAMEFIKISHWA HOSPITALI KWA MATIBABU NA HADI SASA MMOJA AMESHALAZWA NA WENGINE WANAPATA VIPIMO VYA X-RAY KABLA YA KUAMULIWA KAMA WALAZWE AMA WARUHUSIWE.
HADI SASA CHANZO CHA AJALI HIYO HAKIJAFAHAMIKA. TRENI MOJA ILIKUW INATOKA DODOMA KUELEKEA TABORA NA INGINE ILIKUWA INATOKEA TABORA KUELEKEA DODOMA.
Reli yenyewe ipo moja tu, matreni yamechoka hata spidi hayana...hizo treni zinagongana vipi.!!!
ReplyDeleteNi neno moja tu naweza kusema: INASIKITISHA.
ReplyDeleteMie naongezea "UZEMBE MKUBWA" Hivi kabla treni haijaondoka kituoni wahusika wa kuiruhusu itoke huwa awajui ratiba za treni nyingine? Kwenye maonesho ya sabasaba niliingia kwenye banda la hao watu wa reli wakasema kua hua wanajua ratiba na mpangilio mzima wa njia zoooote.Sasa inakuaje?
ReplyDeleteHii inatokana upumbavu na dhana potofu ya "ajali haina kinga", na kila kitu "mungu amepanga". Mungu huyo Mungu gani anayetupangia mabalaa sisi tuu? "Station masters" wa hizi stations mbili ambapo ajali imetokea katikati ya "stations" zao lazima wajibu na wawajibishwe ipasavyo. Lakini mweeh.... hii ndo bongo bwana, kama shemeji yako Lowasa, binamu yako Kikwete, and mjomba wako Kingunge, basi tena hakuna kesi ya kujibu hapo. PUMBAF....KABISA
ReplyDeleteIMPOSSIBLE TO BILIVE.......HII ITAKUWA NI NJAMA FLANI KWA WAHUSIKA WA RELI,MACONTOLERS WAMEZEMBE MNOOOOO,STATION MASTER MZEMBE,KIKWETE FUKUZA KAZI HAWA WATU HARAKA SANA...NATABIRI SMTHNG BAD OTHERWISE{UTABIBU WA NYAKATI}
ReplyDeleteMh...huko Dodoma kuna kitu. Ajali za treni zinatokeaga huko tu kila siku.
ReplyDelete