Hayati Eddy Sally
Hi Michuzi,
Hii picha inatoka kwenye DVD ya filamu ya "Maangamizi the Ancient One'' ambamo Adam Mwambile a.k.a DJ Eddy Sally aliigiza kama Dr. Moshi. Ilibidi niipige picha kutoka kwenye monitor ndo maana unaona flash.
DJ Eddy Sally alifariki dunia juzi, akiwa ameacha nyuma kumbukumbu kama DJ bora aliyepata kutokea Bongo toka enzi za mwanzo wa disko ya Sea View na badaye Keys Hotel ya mtaa wa Uhuru akiwa na DJ Sweet Francis.
Da'Chemi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2009

    Eddy sally kwa mnao mjua kijujuu ndio hivyo dj kabla ya hapo alikuwa drummer boy au mpiga drums wa bendi ya tonics moja ya bendi maarufu za miaka ya70 mungu amlaze mahala pema amen

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2009

    Hakuwa tu drummer boy bali alikuwa anapiga drums na kuimba. Baada ya ya Eddy Sally singer-cum-drummer boy aliyefuatia alikuwa somebody Mhuto Chezimba Band.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2009

    Charles Muhuto ~ CHEZIMBA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2009

    Nakumbuka Khadija Mwanamboka kuna siku alishinda kucheza muziki katika mashindano ya disko la watoto ambapo DJ alikuwa Marehemu Eddy Sally.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 31, 2009

    sura inanijia sana ila nyumbani siku nyingi sijarudi, ama kweli mungu amlaze mahali pema peponi, wote tunaelekea huko huko.

    ReplyDelete
  6. - Mungu amlaze pema peponi Gwiji DJ Eddy Sally, ninamkumbuka in the Early 80s, akiwa DJ wa Club moja maarufu sana then in downtown Lusaka, Zambia kwa jina Studio 22.

    - Kama kawaida ya taifa letu, hatuwezi hata siku moja kuwaenzi wasanii maana in our old rugged screwed up English mentality DJ kama wapiga muziki na comedians, ni wahuni unless tu kama angekuwa mcheza mpira wa miguu.

    - People kama Eddy walipaswa kuwa celebreted nationally kutokana na kazi kubwa ya kisanii waliyoifanya wa-Tanzania tukiwa tunaishi katika mazingara magumu sana kisiasa, atleast waliweza kutu-entertain na kutusahaulisha machungu tuliyokuwa tukiyaishi enzi hizo za miezi 18 ya kufunga mkanda, yaani ya kutouziwa hata mafuta ya gari weekends.

    - Kina Eddy, wako wengi sana Tanzania, wangepatiwa nafasi wangekua kina Dr. Dre na P. Didy wa bongo, lakini wapi na no body cares! Well some of us tulikuwepo na tuliyaona, na we will always talk about it, may God rest and bless his soul, DJ Eddy Sally.

    Respect.

    FMEs!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...