JK akiteta jambo na Mufti wa Tanzania Shekhe Shaaban bin Simba pamoja na Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Musa Salum wakati wa Hitma ya kumuombea marehemu Shekhe Selemani Gorogosi aliyefariki hivi karibuni kwa ajali ya gari huko Lindi. Hitma hii ilifanyika katika msikiti wa BAKWATA Kinondoni Muslim jijini Dar jana jioni. Mufti Mkuu inabidi akae kitini kutokana na sababu za kiafya
JK akisalimiana na baadhi ya waumini walioshiriki katika Hitma maalumu ya kumuombea Marehemu Sheikh Selemani Gorogosi iliyofanyika katika katika Msikiti wa BAKWATA Kinondoni Muslim jana jioni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2009

    INAONEKANA HAPO KWENYE PICHA YA KWANZA,MUFTI AKIMNONG'ONEZA MUUNGWANA,hala hala na mahakama ya kadhi.....

    ReplyDelete
  2. Anon wa 11:09AM na MUUNGWANA pia anamnong'oneza Mufti, hala hala waislam msitishie kutonichagua 2010. Mkinichagua tu kabla sijamaliza muda wangu nawapata mahakama ya Kadhi. Sasa hivi nimeshikwa pabaya nikiwapa upande ule nao watatishia kutonichagua. Sasa sheikh wangu jifanye hujui, nikishinda tu 2010 wallah, mahakama ya kadhi nawapatia. Takbir

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2009

    ebwanaeeeeeeee hii imetulia.

    ReplyDelete
  4. JK: Sasa nani atakuwa mrithi wako baada ya huyu uliyekuwa unamuandaa kuwa mufti kufariki?
    Mufti: Ngoja nitamuuliza Shekh Yahaya

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2009

    anonymous wa kwanza na KIPILI wabaguzi wa dini

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2009

    Kikwete: Waislamu wenzangu kukaa katika jumba lile jeupe mizengwe ni mingi sana. Lakini msijali swala la mahakama ya kadhi nalifanyia kazi. Tupo pamoja.

    Mufti Simba: Nakuaminia mtu mzima. Usijali kura zote za waislamu unazo mwaka ujao. Lakini tupe haki yetu waislamu. Ni haki yetu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2009

    MPENI RAISI UHURU WA KUABUDU. KILA RAISI ALIYEPITA ALIFANYA MAMBO YA KIDINI KWA WAKATI WAKE NA MAMBO YA SERIKALI KWA WAKATI WAKE.RAISI HASIUDHURIE IBADA YA DINI YAKE KISA KUWAOGOPA UPANDE WA PILI, TUKIENDELEA NA UPUMBAVU HUO KILA RAISI TUTAMCHANGANYA NA DINI , ALIPITA MKAPA HIVYO HIVYO. TUACHE USTUPID ESPECIAALY WATU WA NJE.KAMA MAHAKAMA YA KADHI ITADILI NA MIRATHI NA NDOA ZA KIISLAMU WEWE UTAHUMIA NA NINI.NI SAWA NA WAKRISTO WALIVYOTETEA KULA NGURUWE KUWA NI HAKI YAO.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2009

    ANACHOFANYA MHESHIMIWA NI KUTEKELEZA TU AMRI YA DIN INAYOMTAKA MUISLAM YEYOTE KUMHESHIM AALIM WA DINI, YAANI HAPO MHE. HANA UNJANJA LAZIMA ATULIZE BOLI, MUFTI SI MCHEZO, HAO NDO WARITHI WA MTUME WETU ( SAW)

    MZEE WA BUNJU

    ReplyDelete
  9. Jambo lingine ambalo Mufti anamnong'oneza mheshimiwa "RAHISI" ni Mzee ulikumbuka kuja na ndizi mbivu pamoja na kamfuko ka rambo.Unajua tena ktk sherehe kama hizi mpunga hautashuka kisawa sawa bila ya kuwa na japo ndizi mbivu moja.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 09, 2009

    R.I.P Gorogosi

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 09, 2009

    Mahakama ya Kadhi imetolewa na serikali ya uingereza kwa waislam ambao ni asilimia mbili tu.

    kiongozi wa kanisa anglikana ameunga mkono kwa waislam wa UK kuwa na mahakama ya kadhi na inafanya kazi kwa support ya serikali ya UK.

    LORD CHIEF JUSTICE WA UINGEREZA NAYE AME SUPPORT MAHAKAMA YA KADHI KWA WAISLAM WACHACHE WA UINGEREZA.

    MKUU WA WANASHERIA WA UK NAE AMESEMA KUWA MAHAKAMA YA KADHI NI LAZIMA KWA WAISLAM KWANI SHERIA ILIYOPO HAINA MBADALA WAKE.

    SASA CHIKAWE NI MKRISTU ZAIDI KULIKO WAINGEREZA AU MKUU WA KANISA LA KIANGLIKANA?

    WAISLAM WAPEWE MAHAKAMA YA KADHI NA TANZANIA IJIUNGE NA OIC KAMA ILIVYOFANYA KWA WAKRISTU KWA KUIJUNGA NA VATICAN AMBAYO NI TAASISI YA KIDINI.

    ReplyDelete
  12. LAZIMA TUKUBALI KWAMBA KUNA WAISLAM AMBAO NI ELOMU DUNIA SANA NA WENGINE NI ELIMU AHERA SANA . SASA HAPO SHULE ZINAPINGANA NA HATA KAMA MAHAKAMA YA KADHI IKIANZISHWA WENGINE HASA WALE ELIMU DUNIA HAWATAIPELEKEA KESI ZAO. TUTABANANA TU KISUTU.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 09, 2009

    anon 4:58Pm naona unachanganya kati ya Tanzania na Wakristo.Aya yako ya mwisho nanukuu
    "WAISLAM WAPEWE MAHAKAMA YA KADHI NA TANZANIA IJIUNGE NA OIC KAMA ILIVYOFANYA KWA WAKRISTU KWA KUJIUNGA NA VATICAN AMBAYO NI TAASISI YA KIDINI"
    Kwanza ujue sio wakristo wote wanafungamana na VATICAN ni wakatoliki peke yao.
    Pili-Umesema Tanzania ijiunge na OIC ukichukulia kigezo cha wakristo blah blah.Tanzania kama nchi haifungamani na dini yeyote na kila dini ina uhuru sawa mbele ya katiba ya nchi.Kwa hivyo sasa kinachotakiwa kufanyika ni kwa Waislamu kujiunga na OIC kama wakristo(ulivyosema ww) walivyojiunga na VATICAN.
    Tatu-Kila nchi ina mwenendo na katiba zake.Kama UK imekubali kutambua mahakama ya kadhi haina maana kila nchi ibadili sababu UK wamekubali.UK inatambua haki za mashoga na ndoa za mashoga ina maana Tanzania nayo ifuate Mkumbo wa UK?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2009

    Mkuu Jumanne (7:15PM)! Unachosema ni sawa. Lakini kuwepo kwa mahakam ya kadhi hakumlazimishi muislamu kutokwenda mahakama nyingine kutafuta haki kama anaona inafaa. Na kwa yule anayeona mahakama ya kadhi inafaa asilazimishwe kwenda sehemu isiyomfaa.
    Nitakupa mfano mmoja. Serikali iliombwa na waislamu iruhusu hijab kwa wanafunzi wa kike wa kiislamu na ikafanya hivyo (ingawa watu wa dini nyingine walipinga sana hilo kule bungeni wakati wa BWM). Je umeona wanafunzi (wa kike) wote wa kiislamu wanavaa hijab?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 09, 2009

    ninarudia kusema kwamba hizi tamaduni za 'wenzetu' - wazungu na waarabu, tulizoletewa na kuzipokea kwa roho nzuri (sifa mojawapo nzuri ya mwafrika ni mtu asiyembishi sana) ZINAELEKEA KUTUPELEKA PABAYA.

    Ninashindwa kuelewa kwa nini serikali isitoe ruhusa waislamu wakaanzisha mahakama ya kadhi? Je kila ibada inayofanywa na waislamu, imepitishwa na bunge? kama jibu ni hapana, kwa nini waislamu wasijitangazie kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi?????????

    sisi wapagani tunazo mahakama zetu za kalumanzila na hatuhitaji kuomba kibali kutoka serikalini.

    mpagani

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 09, 2009

    Kwanza nampongeza sana rais wetu muheshimiwa JK kwa kushiriki vyema katika shughuli za kidini inayomhusu! Tanzania ni nchi yenye uhuru wa kuabudu sioni tatizo lolote kwa waislam kupewa mahakama yao ya kadhi kama dini yao inavyotaka. Wakristu wakitaka mahama zao nao watapewa na za serikali yetu zitabaki pale pale kwa hiyo itakuwa ni chaguo la kila mmoja!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 10, 2009

    At last baba yupo home. We miss you daddy

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 10, 2009

    Anon wa 4.58pm Hivi Waingereza ndio kigezo cha Ukristo? Au ndio kipimo cha vitu mbalimbali? Nadhani unapo toa hoja yako huna sababu ya kulinganisha linganisha, badala yake ipe vigezo vya nguvu na vya msingi kuitetea.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 10, 2009

    nani anamlipa kadhi???wa mahakama iyo,haina noma wala nini kila muumini ataingiza kile imani yake inamuitaji "kutimiza ibada"

    katiba ya nchi inasemeje?apa sio wakristo wako against waislam,huu ni ujinga kabisa na kutafuta SABABU

    zao ni kuiba kura iki chama

    eti UK,vatican nk!!!

    out of senses

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 10, 2009

    ni kweli,karibu BABA home

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 10, 2009

    Hivi kwa nini katika awamu ya nne kumeibuka mijadala mingi ya dini? Nchi inaelekea kubayaaa, Baba wa Taifa alikemea huu ufa.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 10, 2009

    Nchi yetu ilitawaliwa na waingereza,bunge letu linafuata mfumo wa Uingereza.elimu yetu inafuata mfumo wa kiingereza,mfumo wa mambo yetu mnengi ni wa kiingereza,

    lugha mnayoipenda wengi wetu ni kiingereza,ndio maana nikatoa mfano wa uingereza ambako ndio chimbuko la ukristu.ningesema Malayasia au Saudia mngesema ni nchi za kiislam.

    hata mpira wengi wetu tunapenda timu za uingereza.kwa hiyo MAHAKAMA YA KADHI na OIC NI LAZIMA KWA WAISLAM LIJE JUA AU IJE MVUA.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 10, 2009

    ..mimi nna suali moja naliona muhimu sana: hivi jina lipi ndo sawa na ni kwa nini: hivi ni WAKRISTO/WAKRISTU ao WAMISHENI. Mmmnh, chiswahili chigumu! Ninamuombeni wenye kuimanya mnitongolee, tafazali.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 28, 2010

    Tatizo letu watanzania siku hizi ni udini. Tumekuwa wadini kupita kiasi. Suala likifanywa na kiongozi muislamu linapewa sura ya kejeli na chuki bila sababu.

    Wachangia tunajua wazi kwamba kikwete siyo muasisi wa hoja ya kuwepo mahakama ya kadhi bongo. Alianzisha ndugu Mrema akaungwa mkono na CCM na issue ikafika bungeni. Ilikuwa enzi za raisi mkapa. Toka hapo likaletwa rasmi katika ilani ya uchaguzi wa CCM. Maaskofu na wachungaji waliisoma lakini hamna aliyejitokeza kuikemea CCM kuwa ina udini. Hata askofu mtikila alikuwa kimya. Iweje sasa waislamu wameikubali inakuwa issue? Nini tatizo la kikwete kama siyo kukataa unafiki na kutaka kuitekeleza ajenda ya mahakama ya kadhi?


    Suluhisho ni kwa watanzania wakweli kuwapiga chini wabunge na viongozi wote wadini katika uchaguzi mkuu. Naamini mzee kikwete alikuwa serious tatizo ni hao wadini nyuma yao. Wanadhani udini utawafikisha wapi. Waislamu bado ni ndugu zao japo wanawachukia.

    Kuondoa tatizo la udini ni kuwaolwa dada zao na binti zao kwa gharama zote. Wakiwa wakwe zetu na shemeji zetu labda watatuona nasi ni watanzania kama wao. Tunahaki ya kuabdu na kuinjoi dini yetu kama wao ili mradi atuvunji sheria za nji.

    Haleluya- Allah Akbar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...