RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ameteua Majaji Wapya Kumi (10) wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Uteuzi huo ulianza Juni 26, mwaka huu, 2009.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo Jumatatu Ikulu, Dar es Salaam imewataja majaji hao kuwa ni Bwana Ferdinand Leons Katipwa Wambali, aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani; Bibi Eliamnani Godfrey Mbise, aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu na Bibi Sekela Cyril Moshi, aliyekuwa Mkurugenzi Mahakama za Wilaya hadi Rufani.

Wengine ni Bibi Fatuma Hamisi Masengi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mahakama za Mwanzo, Bwana Sivangilwa Mwangesi, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama ya Rufani; Bibi Pellagia Barnabas Khaday, aliyekuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Bwana Moses Gunga Mzuna, aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Iringa.

Taarifa hiyo iliwataja Majaji wengine wapya wa Mahakama Kuu kuwa ni Bibi Hamisa Hamisi Kalombola, aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Mbeya; Bibi Fredrica William Mgaya, aliyekuwa Msajili Wilaya Mahakama Kuu, Mwanza na Profesa Ibrahim Hamisi Juma aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2009

    Mhe. Jaji Sekela nakupa pole kwa kufiwea na mmeo na hatimaye kuzikwa wend iliyopita-roho ya marehemu ipumzike kwa amani-Amina.

    Pia hongera kwa kuteuliwa kuwa Jaji.

    Kila la heri katika kazi yako.

    Mwanafamilia!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2009

    Jamani naomba wale wanaofahamu tusaidiane mawazo.
    Hivi Rais huteua majaji kwa hulka yake tu au kuna utaratibu maalum wa kiuweledi??!
    Je Kuna tume maalum ambayo hutoa mapendekezo kwa Raisi kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ambavyo pengine Bunge limeviainisha?
    Je Mahakama ya Rufaa kazi yake ni nini? Je ina idadi maalum kikatiba?
    Tuelimishane jamani maana karibu tunafika 50 tumekua.
    Mzawa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...