hapa ni kijiweni kwa Dj mkongwe Young Kim Magomelo (aliyeshika fegi) mtaa wa mkwepu street dar, ambako wadau toka vijiwe mbalimbali huwa huwa tunakutana kubadilishana mawazo haya na yale, hususan mstakabali mzima wa maisha ya bandari salama. hapa huwa haliharibikagi jambo hapa. na lisilojulikana hapa halistahili kujulikana.
Dj Young Kim ndiye muasisi wa shindano la kwanza la kucheza disko enzi zake za Moon dust discoteque la Motel Villa de Tanzanie ya Mwananyamala ambapo fainali zake mshindi alikuwa marehemu Mussa Simba a.k.a Black Moses na mshindi wa pili akiwa Ommy Sydney. Kwa kina dada nakumbuka mshindi alikuwa Salama Kajela, ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Ilala enzi hizo, Mh Jenerali Ulimwengu.
Dj Young Kim pia aliasisi mashindano ya Yo Rap Bonanza kushindanisha marapa wakati muziki wa kizazi kipya unaibuka. Mshindi alikuwa Saleh Jabir

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2009

    Na huyu wa kwanza kabisa kulia mwenye miwani huwa mnakaa naye kijiweni?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2009

    mimi nauliza huo mfiniko ndio ulishapitiwa na wale jamaa wa vyuma chakavu ama huo wa zege ndio uliokuwepo toka mwanzo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2009

    muda wa kuwa kazini nyie mpo mitaani mnapiga domo,no hurry in africa wazungu hawakukosea!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2009

    Ndawila boy, ba-ba mpaka ITALY

    ReplyDelete
  5. Mbona Matango si muoni ukimkosa hapo , basi ujue ana dharura. hivi Sijui huwa anafanya kazi saa ngapi ..?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2009

    Swali hich kijiwe umesha fanya kitu yoyote ya maendeleo au ??? na kazi ni saa ngapi??
    time is money, hurry up !

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2009

    Dah....hivi huyu ndo KIM wa KIM AND THE BOYS???? Duh! aisee watu tumeshazeeka.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2009

    Mkuu,

    Shindano la kwanza la disco Tanzania lilikuwa Discomesha / Discommecial ambalo liliishia hewani. Au nimekosea?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2009

    Baba wa Taifa shati ya Pink tano toka kulia Duh huyu jamaa hakui huyu miaka nenda rudi haya bana labda utabadilika, Anamjua kila mtu na anajua kila jambo. We unayesema watu waende kazini hapo kila mtu anakazi zake peleka deal uone!! big up brodaz

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2009

    jaman yu wapi mohamed bajabir a.k.a jazzie b??jamaa yule ni noma

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2009

    alievaa raba nyeupe sio othman Kazi kweli huyu?

    ReplyDelete
  12. nipatie namba ya kim nimsalimie.duuh amekuwa kibabu sasa.lakini powa tuu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 10, 2009

    Ha ha ha ha ha ha ha ha ha,umenikumbusha mbali sana bro Michuzi.
    YO RAP BONANZA,DJ KIM AND THE BOYZ!ha ha ha ha ha ha.Tangazo lake lilikua linatoka kwenye gazeti la mfanyakazi kila jumamosi,kuna dogo mmoja kauinua mguu juu,kaushika,halafu mwingine kanyoosha juuu,halafu kwa mbali kuna disco light zinawaka waka.Ha ha ha ha ha!

    Mkulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 11, 2009

    ALIYEKAA CHINI WA KWANZA KUSHOTO AITWA KAZI SELEMANI KITUNDU ! KAKIMBILIA BUNJU SIKU HIZI.ANA KIJIWE CHAKE KINGINE HUKO DUUU ! JAMAA AKUI.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 12, 2009

    YAKUBU TARATIBU NYAMA CHACHE!!!

    UNAFIKIRI KUNA MTU WA KUBAKI, BA BA MANENO ITALY KWA NASSA!!!!

    MDAU MBITA!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...