Juu na chini ni mchezaji wa kibongo Denis Geoffrey (jezi nyeupe) mwenye mpira katika majaribio nchini Puerto Rico na timu ya Carolina Cigantes

Mchezaji Denis Geoffrey ni miongoni mwa wachezaji wenye ndoto ya kucheza mpira wa kulipwa nje ya Tanzania,Denis alizaliwa Tanzania,mkoa wa Arusha miaka 24 iliyopita.sasa hizi anaishi nchini Marekani,Durham,North Carolina na anachezea timu ya Cary Clareps inayoshiriki ligi inayoitwa USL.

hii timu ipo chini ya ajenti anayeitwa Howid Goldberg anayeandaa vijana wenye vipaji kama Denis na hatimae kuwatafutia timu ya kulipwa hapa marekani na hata ulaya.

Howid Goldberg pia ni ajenti wa mchezaji Nino Gomez anayechezea Fc Porto ya Ureno.Denis anasema kutokana na yeye kua na kipande cha kijani ndio maana kwake ni vigumu kwa ajenti kumpa majaribio ulaya.

Denis alikuja huku Marekani akiwa na miaka 14 kwa kumfuata Baba yake Lepana Geoffrey na amesoma na kucheza mpira college ya Columbia,St.Louis 2005-08,mwenyewe pia anapendelea kufanya majaribio na timu ya Taifa kama atahitajika au kupata nafasi kufanya hivyo.

kwa habari zaidi za Denis unaweza kuzipata kwa kubofya www.caryclareps.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2009

    kipande cha kijani ndio nin?
    tumia lugha iliyonyooka kidogo,
    halafu mbna hiyo website hai exist? au ndo unatupiga changa la macho?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2009

    kipande cha kijani???????????

    eee jamani?

    so unajiuza timu ya maximo..aya

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2009

    nimsaidie anko michuzi kujibu swali.
    kipande cha kijani hapo nadhani alikuwa anaamanisha "green card" ile ya USA
    Mdau Kyk.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2009

    Mtoa habari amechemsha hiyo website ni www.caryclarets.com

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2009

    Kijana bado ana kazi kabla ya kuweza kuitumikia Taifa Stars. Ligi anayocheza ni ya chini ya ligi waliyoenda kina "Cannavaro". Walau angekuwa anacheza kwenye USL tungependekeza ajaribu.
    Picha zinaleta matumaini lakini. Akaze msuli aje kuwakilisha. Mafowadi wetu wengi wanaona aibu kucheka na nyavu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 15, 2009

    na kweli wabongo despereti...chochote kitanzania ughaibuni hata kama ni jiwe mtasema kipaji!!!ebu njooni kwetu Mbeya muone vipaji 'made in bongoland'

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 15, 2009

    sasa mbona kama ligi yenyewe ni ile ya mchangani???poa lakini mshikaji, keep on dreaming, one day you might pull a " Hasheem Thabeet" move, and all of us so called "haters" we'll start to kissing your a$$

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2009

    Wacha kutuyeyusha bwana, mbona wacheza baseball wengi tuu sio raia wa marekani, na wanagreen card hiyo hiyo. Hasheem mwenyewe he is still on a visa, sasa wewe usituyeyushe eti kwa sababu una greencard ndio agent asikutafutie time. you don't have to be an american citizen to be represented by an agent; the truth is kipaji chako bado hakina kiwango na sio maswala ya greencard. by the way, considering your age, you better off to start look into other career prospects kama vile nursing homes, group homes kwani soccer might not be a thing for you. in other words, jua linazama changamkia ulaji mwengine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...