Mambo Michuzi,
Kwanza naomba nikufahamishe kwamba mie ndio nimesharudi nyumbani na nimeshaanza kuseto. Libeneke sio kali sana kama nilivyokuwa nahofia. Ukiondoa wadau kuwa slow slow katika kila kitu, mambo bado ni mswano. Bongo tamu bwana, asikwambie mtu...Nikikumbuka nilivyokuwa naota kibyongo kwa boxi na sasa mambo tambarare tu. summer time mwaka mzima!

Waama baada ya salamu, leo naomba tukumbushane tulikotoka ambapo kabla ya kuletewa mifuko ya plastiki tulikuwa tukitumia vifungashi kama hili PAKACHA kufungia bidhaa zetu bila kuathiri mazingira yetu. Lakini siki hizi, dah! bila fuko la 'Rambo...'

Mdau Lilly

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2009

    WTF? Sijaukuelewa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2009

    WELCOME BONGO LAND UKITAKA MIWA HIPO UTAKAMULIWA NA MAJI UTAKUNYWA ILA USIKOSE KUPITA KAZI MZUMBWI KULEE NDIO KWETUU.MADAFU KWA SANA TUU UAMENYWA UTAVUNJIWA NA MAJI UTAKUNYWA ........KARIBU NDUGU YANGU
    ILA SISI BADO TUKO TUNAVUTA MDA TUJIUNGE NAWE NDANI YA BONGO LAND

    ReplyDelete
  3. Anita (Lisbon)July 14, 2009

    Hongera kwa kuitikia wito wa dr shayo
    ila swali, yeye anarudi lini? manake tunamuhesabia siku!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2009

    kumbe huyu dada Lily alikuwa serious kurudi Bongo oohh hongera zako,sie wacha tumalizie huu mwaka kwanza. haha

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2009

    Hongera mwanzetu. Sisi bado kidogo. Kila mwaka tunasema mwaka kesho. Ila mwaka ujao lazima nitie time huko bongo. Salamu kwa wadau wote wa Mwanza Sekondari 1992 na Tabora Boys 1995. Milima haikutani ila binadamu hukutana. Nyumbani ni nyumbani tu!!! C ya soon....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2009

    ...maisha yamekushinda tuu huna lolote,states ndio mwisho wa mambo,inaonekana hukusoma ulikuja kucheza cheza tuu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2009

    We annon Tue Jul 14 04:09:00Am
    acha hizo, mtu kaamua kujirudia nyumba badala ya kumwambia hongera nakutakia kila la heri, nyumbani ni nyumbani mama ni mama, wewe unaanza eti heee states ndo mambo, kwani kakosea nini?

    Lilly nakutakia kila la heri!

    P.E.D

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2009

    Karibu nyumbani mwaya! kwani nyumbani ni nyumbani na mkataa kwao mtumwa. Pia mcheza kwao hutuzwa na heri pako pabovu kuliko kwa mwenzio pazuri. Ah nisiseme sana. KARIBU MWE!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2009

    kilamtu akipewa pakacha kwa bidhazake si minazi yote itateketea sasa nani mharibu mazingira mwenye rambo bag au pakacha??
    fikiri kabla huja ropoka kumbuka hilo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2009

    Mdau hapo juu anony 07:57:00 PM umenifurahisha;)mwishowe watakuja kutuambia tusipikie umeme tutumie kuni ili kulinda mazingira.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2009

    Dada umefulia dada usitudanganye. Kaka Obama kawabania sasa mnajidai bongo tambarare, wewe jichanganye tuu acha sifa za kijinga, wewe unataka kulinganisha kwa Obama na JK land? acha hizo kabisa, box zimekushinda kubeba, kwahiyo we cheki na TMK kama wanavyosema 3 bila.Yaani kipindi chote ulikuwa hujui bongo summer time the whole year? you must be trying to please yourself, everyone know that, the financial crisis has made you to loose your cheap labour so the only way is to comeback and say bongo tambarare. Mwanzoni utasema maji ya madafu matamu,nyama unatupa baadaye mambo yakibana utakula mpaka mbata acha nyama ya dafu.
    But all in all, we have our swahili phrase which says ng'ombe akivunjika mguu anarudi zizini na kama wewe Mkristu kuna kifungu kinasema yule mtumishi alifuja mali zake akaenda kujichanganya halafu hali ilipokuwa mbaya akaamua kurudi kwa baba yake na baba yake akamfanyia sherehe kubwa, kwahiyo welcome back home
    EAST OR WEST HOME IS THE BEST BABY

    Cheers
    Mdau wa chanika- madafu growers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...