Mambo Michuzi,
Kwanza naomba nikufahamishe kwamba mie ndio nimesharudi nyumbani na nimeshaanza kuseto. Libeneke sio kali sana kama nilivyokuwa nahofia. Ukiondoa wadau kuwa slow slow katika kila kitu, mambo bado ni mswano. Bongo tamu bwana, asikwambie mtu...Nikikumbuka nilivyokuwa naota kibyongo kwa boxi na sasa mambo tambarare tu. summer time mwaka mzima!
Waama baada ya salamu, leo naomba tukumbushane tulikotoka ambapo kabla ya kuletewa mifuko ya plastiki tulikuwa tukitumia vifungashi kama hili PAKACHA kufungia bidhaa zetu bila kuathiri mazingira yetu. Lakini siki hizi, dah! bila fuko la 'Rambo...'
Mdau Lilly
WTF? Sijaukuelewa.
ReplyDeleteWELCOME BONGO LAND UKITAKA MIWA HIPO UTAKAMULIWA NA MAJI UTAKUNYWA ILA USIKOSE KUPITA KAZI MZUMBWI KULEE NDIO KWETUU.MADAFU KWA SANA TUU UAMENYWA UTAVUNJIWA NA MAJI UTAKUNYWA ........KARIBU NDUGU YANGU
ReplyDeleteILA SISI BADO TUKO TUNAVUTA MDA TUJIUNGE NAWE NDANI YA BONGO LAND
Hongera kwa kuitikia wito wa dr shayo
ReplyDeleteila swali, yeye anarudi lini? manake tunamuhesabia siku!
kumbe huyu dada Lily alikuwa serious kurudi Bongo oohh hongera zako,sie wacha tumalizie huu mwaka kwanza. haha
ReplyDeleteHongera mwanzetu. Sisi bado kidogo. Kila mwaka tunasema mwaka kesho. Ila mwaka ujao lazima nitie time huko bongo. Salamu kwa wadau wote wa Mwanza Sekondari 1992 na Tabora Boys 1995. Milima haikutani ila binadamu hukutana. Nyumbani ni nyumbani tu!!! C ya soon....
ReplyDelete...maisha yamekushinda tuu huna lolote,states ndio mwisho wa mambo,inaonekana hukusoma ulikuja kucheza cheza tuu
ReplyDeleteWe annon Tue Jul 14 04:09:00Am
ReplyDeleteacha hizo, mtu kaamua kujirudia nyumba badala ya kumwambia hongera nakutakia kila la heri, nyumbani ni nyumbani mama ni mama, wewe unaanza eti heee states ndo mambo, kwani kakosea nini?
Lilly nakutakia kila la heri!
P.E.D
Karibu nyumbani mwaya! kwani nyumbani ni nyumbani na mkataa kwao mtumwa. Pia mcheza kwao hutuzwa na heri pako pabovu kuliko kwa mwenzio pazuri. Ah nisiseme sana. KARIBU MWE!
ReplyDeletekilamtu akipewa pakacha kwa bidhazake si minazi yote itateketea sasa nani mharibu mazingira mwenye rambo bag au pakacha??
ReplyDeletefikiri kabla huja ropoka kumbuka hilo
Mdau hapo juu anony 07:57:00 PM umenifurahisha;)mwishowe watakuja kutuambia tusipikie umeme tutumie kuni ili kulinda mazingira.
ReplyDeleteDada umefulia dada usitudanganye. Kaka Obama kawabania sasa mnajidai bongo tambarare, wewe jichanganye tuu acha sifa za kijinga, wewe unataka kulinganisha kwa Obama na JK land? acha hizo kabisa, box zimekushinda kubeba, kwahiyo we cheki na TMK kama wanavyosema 3 bila.Yaani kipindi chote ulikuwa hujui bongo summer time the whole year? you must be trying to please yourself, everyone know that, the financial crisis has made you to loose your cheap labour so the only way is to comeback and say bongo tambarare. Mwanzoni utasema maji ya madafu matamu,nyama unatupa baadaye mambo yakibana utakula mpaka mbata acha nyama ya dafu.
ReplyDeleteBut all in all, we have our swahili phrase which says ng'ombe akivunjika mguu anarudi zizini na kama wewe Mkristu kuna kifungu kinasema yule mtumishi alifuja mali zake akaenda kujichanganya halafu hali ilipokuwa mbaya akaamua kurudi kwa baba yake na baba yake akamfanyia sherehe kubwa, kwahiyo welcome back home
EAST OR WEST HOME IS THE BEST BABY
Cheers
Mdau wa chanika- madafu growers