Limousine za kisasa zimewasili Bongo. Zina kila kitu kama yale yanayotumiwa na mastaa wa kimarekani. Ni magari ambayo yametoka kiwandani mwaka 2007. Kwa mahitaji yako ya harusi, bithday party, Dar city tour, Airport to city centre na shughuli mbalimbali,wasiliana nasi kwa namba
0713 406507,
0777193677,
0719144645.
kwa ndani na kwa ubavuni na nyuma




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Mdau - majuuJuly 13, 2009

    corrections . Michizi.. aah sorry Michuzi . Limousine ya kisasa sio za kisasa.. wakati tunaiona ni moja tu .. Anko kama unavyojiita siku hizi unapenda kukweza mambo mh!!

    ReplyDelete
  2. kalumekengeJuly 13, 2009

    INASIKITISHA SANA TENA SANA.

    ReplyDelete
  3. SAFI HIYO LAKINI SUPER CELEBS HAWATUMII KAMA HIZO! HIYO QUALITY HAIKO INLINE WITH THEIR STANDARDS.
    Angalia online ya limo ya jacko au ya bwana chris brown/ kicheche carey.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2009

    Kaka Michu
    Gari za 2007 kwa USA sio mpya,kwa sasa USA gari mpya ni zile zinazoitwa toleo la 2010(kumbuka USA ikiisha fika mwezi July hwa mwaka mpya kibiashara),kwa hiyo ndiyo kusema gari hizo zilizoletwa Dar zina miaka 3 toka zitengenezwe!
    Anyways and always Chylser huwa gari zenye A/C nzuri sana

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2009

    WATANZANIA TUSIWE MAMBUMBU WA VITU KAMA HIVI.GARI HILI HATA SPARE HUPATI BONGO
    MTU ATATAMBA KUWA NA GARI KAMA HILI WAKATI YEYE ANATUMIA CHOO CHA PASPOTI SIZE.

    ReplyDelete
  6. wee acha ushamba umetoka ukerewe jzi nini??,Limo hilo haliuzwi linakodishwa..ununue utaenda nalo wapi utapaki BReak Point ??? una raha gani mTZ wewe mpaka ulitumie wewe ???

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2009

    Kutoka Airport mpaka kwa Mtogole bei gani? 'Bei Maelewano?'

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 13, 2009

    pelekeni hayo huko magaribeipoa hatutaki magari humu kwenye blog ya jamii

    ReplyDelete
  9. kichuguu mwitaJuly 13, 2009

    Je lililipiwa ushuru kiasi gani?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 13, 2009

    wewe mtowa maoni wa tatu unamatatizo gani? hivi huoni kitu kuwa kizuri na bora mpaka kiwe kinamilikiwa na celebrity? unadhani watu wote wana akili za namna yako? jitowe katika utumwa wa kuiga ya watu!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 13, 2009

    Kweli anoni aliyesema kutumia choo cha passport size hajakosea. Mie huku TZ inaniuma mambo kama haya ya kulazimisha na watu kushabikia ujinga italeta Husda mbaya kwa watu wengine.

    SAWA NA HOSPITALI KUBWA KUWA NA MA DAKTARI 30 WOTE WANATUMIA MA PRADO WAKATI GARI YA KUCHUKULIA MGONJWA NI MOJA. AIBU TUPU. VOTE NI VYAKUPITA TU.

    TUWACHENI MAKUBWA. MZ

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 13, 2009

    UNAJUWA MAMBO MENGINE BWANA GARI KAMA HIZI TZ BARABARA HATA HAZIFAI, HUO NDIO UKWELI IKIPIGA KONA AJALI INAITA. TIZAMA WENZETU UK BORA SIO TUNA BARABARA KUBWA ILA UWENGEREZA BARABARA ZAO NYEMBAMBA ILA VITU KAMA HIVI VICHACHE SANA 1. MAFUTA 2. GARI KUBWA 4X4 SIO SANA WANAJUWA ZINAWEZA KULETA AJALI wanatengeneza ma LAND CRUISER ila yanaenda nchi kama MAREKANI NA AFRICA NA SOUTH AMERICA SABABU YA BARABARA SASA LAND CRUISER na MA PRADO TANZANIA SAWA.

    LIMO TANZANIA KIDOGO KAMAH IYO IPO CHINI SANA NA NDEFU HATA HAZIFAI NA VIFAA HAKUNA. BORA INDIA WAPO NA TATA ZAO NA VIBAJAJI. PAZI

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 13, 2009

    kila kitu lazima watu wajaribu, walioponda hapo juu wote ni wavivu wa kujaribu, na ndo masenene, haijarishi kuwa gari lina miaka mitatu,lakini huyu kajaribu, na anaongeza hadhi ya mji. ni mara ngapi watawala wenu wanafikiri huku tunaishi juu ya miti , na wakikuta magari mazuri kuliko wanayoendesha kwao, wanashangaa.
    kwa wanaojifunza, hawaogopi kujaribu, wanaotaka kupendezesha harusi zao, msisite kumuunga mkono mdau hapo juu, achaneni na wabebao box hao wasio na maisha wala mtazamo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 13, 2009

    Ndugu yetu JANGUO ameleta nyingine tena?
    Aaa huyu bwana hatumuwezi. Ameshafika mbali sana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 13, 2009

    Sasa litapita wapi? Au limejengwa kwa barabara za Tabata na Sinza pia? Hii ni ajabu. Kwa sababu mastaa marekani wanapanda magari ya namna hii na sisi lazima tuwe na gari za namna hii? Kwa nini usipeleke pesa zako kule kijijini kulima mahindi na mchele ambao watanzania wengi wangekushukuru? Kumbuka yale "mabasi ya ghorofa" yaliyoletwa Tanzania kwa sababu tulitaka tuwe kama London, yako wapi. Huyo mtu aliyekutengenezea business plan kweli anahitaji kuwekwa kiti moto!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 13, 2009

    hii gari tayari ni USED. we angalia taili tu zilivyo vipara!!! kashata za tairi zimekwisha halafu unatuambia ni mpya!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 13, 2009

    Aaaa..!!!, maharusi na ma-star wa bongo watazitumia, wala msikonde. Mabo swafiii, bongo tambarare

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 13, 2009

    mambo yeto ni piki piki tu mliona wedding ya last week? acheni na mambo ya limosins ebo!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 13, 2009

    UTAKUTA MTOTO WA FISADI KAULIZWA NA BABA "NIKUFUNGULIE BIASHARA GANI MWANANGU" MTOTO KAJIBU " NATAKA BIASHARA YA MA LIMO BABA".KWAHIO MTOTO NDIO KALETEWA BIASHARA HIO ASHINDWE MWENYEWE SASA.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 13, 2009

    swimming pool limo humo ndani?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 13, 2009

    Self drive inaruhusiwa kwenye hii pipe?Nina Manzi yangu kijenge ya juu ameshanizoea na Landrover na Cruiser natamani nimtokee na pipe kama hii maana manzi ana wenge la hatari ila nikimtokea na hichi kitu lazima anielewe.
    Pili je huu UZI naweza kwenda nao Porini(Mererani)nikipigiwa simu shimo linatowa?
    Hii ni MANDO ya ukweli.

    Mdau A.city

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 13, 2009

    Vitu kama hivi ni kwa wale wanaotaka mabadiliko tu.
    Nyie ambao bado mna matatizo ya vyoo vya passport size hii si size yenu, jengeni kwanza hivyo vyoo vyenu sisi wengine tulishahangaika zamani tukajenga vyoo vya kisasa na huu ni wakati wetu wa kuendelea mbele na kuleta chachu ya mabadiliko.
    We need more Limousines hata kama ni za beattle!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 14, 2009

    wewe Anony wa Mon Jul 13, 02:32:00 PM akili yako inakutu. Unawaza shamba, kushukuliwa na wakulima-Kweli we mwanasiasa ama mganga wa kienyeji maana hizo akili hazina kipya wala kizuri

    All in all big up bro. Natamani sana kujenga ukumbi kama MGM na mataa ya kutisha kama mbinguni.

    Mungu aliumba paradise watu wajirushe na wafurahi na sio shamba, kulima, kijiji. Thats bush politics na ugonjwa wa ujamaa na kutegemeana

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 14, 2009

    wenye roho maskini-Litapita wapi? la zamani! Tusiige kama ulaya! Baya! sio kama la maiko jakison

    Acheni ushamba. Mko majuu bado akili za Nsungu Manda ama Nansio ukelewe. Badilikeni

    Guys do more and more ili bongo iwe NY watu tusherekee
    Toeni akili za zamani ingizeni mpya

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 14, 2009

    Positive. Goood. Super. One step up. Hongera sana wakubwa.

    Tusioweza ku-saave pesa na kununua hata vicheche haki yetu kukanda.

    Hali ni mbaya na sio wote tunaweza kujaribu

    Pelekeni moja Morogoro na moja Dodoma na Arusha huko.

    Tanzania oyeeeeeeeeeee. CCM juu!

    ReplyDelete
  26. Hili ni kwa ajiri ya biashara, sio basi, kwaajili ya special occasions, acheni ujinga, ukiwa na sumni yako kodisha kwa ajili ya harusi.... hii sio taxi, watu oh barabara mbaya , hakuna spear parts zake,acheni ufinyu wa kufikiria kibiashara, mwacheni jamaa aliyeleta afanye biashara yake kwa watu watakaoweza kukodi, wewe kama huna kitu au uhitaji nyamaza.

    Acheni mambo yenu ya kukatishana tamaa na ufinyu wa mawazo, na roho za kichawi. Mdau leta nyingine zaidi ili hii serikali ya wajinga ilazimishwe kujenga barabara nzuri, badala ya kupiga domo tu na mijitu kulala wanafikiri dunia imelala kama walivyolala wao.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 14, 2009

    KAKA MICHUZI HONGERA SANA KWA KULIRUSHA HILO TANGAZO LA MDAU MWENYE LIMO! HAO WOTE WANAOMPONDA JAMAA NI WAVIVU WA KUFIKIRI NA NI WATUA AMBAO MAENDELEO KWAO NI NDOTO! HAKUNA KITU KILICHOTENGENEZWA KWA AJILI YA NEW YORK TU AU LONDON TU! KILA KITU KINAWEZEKANA AS LONG AS UKO CHINI YA HII DUNIA! WATU WAMESEMA MEEENGI WAMEPINGA SANA ETI SPARE HAKUNA ETI LIKO CHINI! HUYO MDAU SIO MJINGA MPAKA AKALILETA LAZIMA ALIFANYA RESEARCH KABLA YA KULILETA NA KUJUA KWAMBA SPARE ATAPATA WAPI HIYO NI NON OF YOUR BUSINESS!WABONGO WENGI NI WAGUMU KUBADILIKA ( KU ACCEPT CHANGE) KWAO NI NGUMU NA NDIO MAANA WENGI HUWA WANAFANYA VITU BILA KUFIKIRI, NA WENGI NI WAIGAJI TU! WABEBA MABOX UGHAIBUNI MAMBO BONGO YANABADILIKA MKAZANE KESAVE MJE MWEKEZE LA SIVYO MWAWEZA KUZEEKA NA MIBOX HIYO NA SHULE MSISOME VILEVILE IN SHORT NO FUTURE KATIKA KUBEBA BOX!
    MDAU WA KUSINI KWA MKWAWA!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 14, 2009

    HUU MTAMBO USIPIME WANAO OSHA VINYWA NI FULL JELASI BONGO SI MCHEZO NIPO KIWANJA MWENYEWE NIMEKUBALI SI MCHEZO KAMA UNAWEZA WEKA STRIP SHOW NDANI NA BAR WATU WAJIRUSHE MAISHA YENYEWE MAFUPI UKIZIPATA ZIFAIDI

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 15, 2009

    Washikaji msiogope wajinga ndio waliwa hapo kinamata ni hilo bodi tuu. Kwani hamjui kwamba Audi na Golf injini yake ni ile ile hiyo mbona hata A taun ukitaka Zinachongwa tu. Mbona mnaogopa bodi

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 17, 2009

    First of all, hongera kwa huyo mdau mwenye hiyo 300C. Its an amazing car and it brings out the presence. Ninasikitika kuona maoni ya some of wabongo maana ni balaa. Kwanini watu wanakuwa na kinyongo sana? Hii ni biashara ya mtu na kwenye biashara kuna ups and downs. Let the man do his business na acheni wivu. If you can't afford to do anything like this just sit back and shut ur mouth maana you are just wasting ur time and the government's time as well. U could be doing something productive for u and the country. So mind ur own biznes shhh.... Roho mbaya tu zinawasumbua.

    ReplyDelete
  31. You have done a great job on this article. It’s very readable and highly intelligent. You have even managed to make it understandable and easy to read. You have some real writing talent. Thank you. Hamilton Party Bus

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...