
Mbunge wa viti maaalum, Al-Shymaa Kwegyir, akipita jukwaani na vazi la ubunifu, wakati wa onyesho hilo,
PINDA AASA WANANCHI KUTUMIA M- PESA
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amewaasa wananchi na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia huduma ya M-pesa inayotolewa na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania na kuwataka wabunge na Watanzania kuitumia huduma hiyo kwa kutuma na kuchukua fedha ili kuokoa muda wanaoupoteza wanapokwenda kupata huduma hiyo sehemu nyingine na kuwaomba wabunge kuwaelimisha wananchi majimboni mwao.
Pinda alitoa wito huo Ijumaa usiku alipokuwa kwenye hafla ya 'Meet and Greet' ambapo kampuni ya simu ya vodacom ilichukua furusa hiyo kwa ajili ya kuelezea huduma za M-pesa pamoja na zoezi la usajili wa laini za simu.
PINDA AASA WANANCHI KUTUMIA M- PESA
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amewaasa wananchi na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutumia huduma ya M-pesa inayotolewa na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania na kuwataka wabunge na Watanzania kuitumia huduma hiyo kwa kutuma na kuchukua fedha ili kuokoa muda wanaoupoteza wanapokwenda kupata huduma hiyo sehemu nyingine na kuwaomba wabunge kuwaelimisha wananchi majimboni mwao.
Pinda alitoa wito huo Ijumaa usiku alipokuwa kwenye hafla ya 'Meet and Greet' ambapo kampuni ya simu ya vodacom ilichukua furusa hiyo kwa ajili ya kuelezea huduma za M-pesa pamoja na zoezi la usajili wa laini za simu.
Usiku huo ulipambwa na onesho la mitindo ya mavazi ambapo wabunifu kadhaa walionesha kazi zao, mamodo wakiwa baadhi ya waheshimwa wabunge. Bendi ya muziki ya Les Capitale 'Wazee Sugu' chini King Kikii ilitumbuiza.
Waziri mkuu alisema M-pesa ni huduma bora kwa kuwa humfanya mtu kutokwenda kupanga foleni ya kutuma, kupokea au kuchukua fedha katika taasisi zinazojihusiha na fedha pia ni huduma inayoweza kumsaidia mtanzania kununua Luku,kulipa bili ya maji Dawasco na kupokea mishahara yao kupitia njia hii kiurahisi zaidi.
“Hawa jamaa (Vodacom) walipokuja kunieleza huduma hii, niliwaambia ni vema habari hii wakaifikisha kwa wabunge kwa kuwa wao wanaweza kuifikisha vizuri zaidi kwa wananchi” alisema Pinda
Pinda alisemaa kutokanaa na kuhamasishwa huko hata yeye ataanza kuitumia huduma ya M-pesa pamoja na kusajili laini ya simu yake ili aweze kwenda na mabadiliko ya teknolojia.
“Kesho na mimi nitakwenda kusajili simu yangu, nimeelezwa hapa bungeni kuna vibanda vinatoa huduma hiyo” alisema Mh. Pinda.
Naye meneja wa Vodacom Innocent Ephraim, ambae ni mtaalamu wa huduma ya M-pesa alisema ni huduma nzuri kwa kuwa haimfanyi mtu kutembea na fedha nyingi lakini pia hurahisisha zoezi la kutuma na kupokea fedha.
Alisema zoezi hilo lina manufaa zaidi kwa kuwa hata maeneo ya vijijini yasiyo na taasisi za kifedha huweza kunufaika na mfumo huo uliobuniwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya mtumiaji wa mtandao huo.
Aidha kuhusu zoezi la usajili wa simu, alisema mawakala mbalimbali wa mkoani hapa wanatoa huduma hiyo ili mradi mtu awe na vitambulisho vinaavyotakiwa.
“zoezi la usajili wa laini si lazima uende Dar es salaam au sehemu nyinginezo kwa kuwa hata mawakala wa hapa wanatoa huduma hiyo” alisema mtaalamu huyo
Mzee wetu Bwana Pinda inabidi atafute mtu wa kumsaidia kupanga mavazi yake. Huo mchanganyiko hapo hata siuelewi-elewi.
ReplyDeleteKazi yake nadhani anajitahidi.
Yani niliifurahia hii show kweli. Tungeomba waandae kipindi maalumu kwaajili ya kuonyesha show hii. Kwa hakika mitindo ni mizuri hasa aliyevaa vazi la kijani mwwaaa limependeza sana. Hiyo ndiyo mitindo ya kiafrika bwana na inayotakiwa kuvaliwa na waafrika.
ReplyDeleteHaipendezi tunakuwa tunaiga tuu mavazi ya kizungu wakati tunamavazi yetu. Ikiwa wanigeria wameweza kwanini sisi tushindwe.
Katika maigizo tunatakiwa tuwakilishe mavazi yetu.
Nawapa hongera wabunge kwa kubuni hili.
mwana wa mkulima atoka na ze bellon (fulanazzz!)..michu unaukumbuka msamiati wa bellon?..na 'bizbo'..hebu wadau tupeni misamiati mingine ya enzi za nineteen kweusi!..
ReplyDelete"AWAASA" HILI NENO NAONA LIMETUMIKA VIBAYA KUTOKANA NA HABARI YENYEWE.
ReplyDeleteNAAMINI "KUASA" NI WARN (KWA KIINGEREZA) NAAMINI MOJA YA MANENO MBADALA YALIYOPASWA KUTUMIKA HAPA NI "AHIMIZA"
ANYWAY, I COULD ALSO POSSIBLY BE WRONG
Kweli ndio maana Obama anasema tuletewe Mbegu tu Africa. Hii mambo ya kuletewa misaa ya chakula ianatufanya tunakua tunakua hatuna la kufanya.
ReplyDeleteYaani bunge limegeuga kuwa catwalk
Duh! Waende kwenye majimbo yao kufanya kazi .....I am speechless...
Muheshimiwa Pinda anahitaji up date ya jinsi ya kuvaa, kwani kila avaacho kinaonekana kimechoka. be up to date baba. mdau UK
ReplyDeletewatanzania hatuna wasi wasi kila kitu ni poa tuna muda wa kupoteza kwa mambo yasio na maana, kama viongozi wetu wanavyodhihirisha, kuna mambo tele ya kupewa lipa umbele zaidi ya hili lakini wao wanaona hili ni muhimu zaidi.
ReplyDeleteAti, mamodo?! Viongozi wetu sasa zea not serious!
ReplyDeletehahahahah ama kweli bongo tambarare, yaani kabisa wabunge wamefanya shoo ya mavazi bungeni. hahaha yaani hapa nacheka sina mbavu. haki ya mungu ni vichekesho duh!
ReplyDeleteWatanzania wenzangu!
ReplyDeleteNaona hao waheshimiwa wetu na watunga saheria wetu wamekosa kazi wakati ni wazi kuwa majimbo yao yanadidimmia na wananchi wengi wanashinda na kulala na njaa.
Naomba JK akemee hiki kitendo na awasihi mara moja wasije kugeuza kakawa kamchezo! Si munajuwa tena mbongo ukimuacha aegemee atasinzia na ukimuasha utakuwa ugomvi.
wabunge ni binadamu kama binadamu wengine na hivyo wanahitaji muda wa kujiburudisha. hii ilikuwa ni mojawapo ya burudani na sioni tatizo. burudani ni mahitaji ya msingi kama malazi, chakula, mavazi, na hata ngono. pengine kutokana na hafla kama hii tunaweza kuanza kuona kuwa watanzania tunaweza kubuni staili ya mavazi yetu ambayo yanaweza kushindana na staili za 'wenzetu'. si mmeona waghana hususan rais wao wakati wa mapokezi ya obama, hakuna cha suti ya ulaya wala ya china!!!
ReplyDeleteThis is totally and uttery rubish...
ReplyDeleteLaw makers doing a catwalk???? Gosh..save this nation...otherwise 2we're doomed to fail".
Ohhh wabunge ni binadamu kumbe. Leo catwalking, kesho kula nyama mnadani, kesho kutwa, kucheza twanga pepeta.
ReplyDeleteYule aliyesema we are doomed to fail, he/she is right.
Jamani this can't be, hawa wabunge wanasoma vitabu saa ngapi?
Completely BS
Inasikitisha sana, hawa wanaojiita waheshimiwa "what sort of message are they trying to send out to wananchi if not the world, this is utterly disgrace" Hivi bunge letu huwa linakaa kwa muda gani hasa? manaake mimi nimetoka nyumbani muda kidogo hivyo naomba radhi. kwa nini wasifanye haya mambo wakati likizo zao zinapoanza?? kwa nini lakini?? natamani kulia jamani.Inatia uzuni sana jamani sisi waafrika. Watanzania tuamke jamani hawa wabunge tumewachagua sisi kwa hiyo hawapaswi kufanya wanavyo taka wao.
ReplyDeleteInasikitisha sana kuona kuna wadau humu wanadiriki kusifia mambo yaha, tusipokemea jambo hili "soon" tutaona nyama ambazo wanakula pale sijui panaitwa mnadani zitaanza kuchomwa kwenye viwanja vya bunge kwa kisingizio waheshimiwa wanajiburudisha baada ya kazi. Nina mengi yakusema lakini sitaki kuwachosha, "My fellow Tanzanians Lets sign Petition and send it to state house, No changes come to our country until we change ourselves. oh God
Acheni utimanyongo wenu .. mambo hayo yapo kila kona . kazi na burudani .. mbona wanapocheza mpira . soccer , netball hakuna comments mbaya .. ila mitindo mnaona wanafaidi ..hii ni moja ya kutukuza mavazi yetu ya asili . kitu kama hicho kingefanyika nchi za magharibi mngeshabikia ..ooh!! boy give me a break!!
ReplyDeletejamani huyo ndio hafidh ali alivyo sasa? wenzako tuliosoma darasa moja mbona hatukukonga namna ile?
ReplyDeletewala wanaotetea kuwa hawa wabungnge ni binaadamu na wanastahili kujiburudisha mumeshindwa kuona mbali. kweli sote ni binaadamu lakini unapoamua kuchagua professional fulani kuna mambo unakuwa hupaswi kufanya na kusema kweli kwa mwana siasa wa kiafrika kuwa na nafasi ya kufanya haya kunamfanya yeyote mwenye busara kujiuliza hivi kweli mudq huu wasingeliutumia kutatua jambo fulani la kitaifa?
ReplyDeletehutegemei kqtu kumuona mcheza mpira wa kulipwa akijimwaga kilabuni na kunywa chakari ilhali timu yake ina iko hatarini kushuka daraja, na infact hata kama haiko hatarini kushuka daraja, huwezi kumuona mchezaji akifanya hilo bila ya wapenzi kulaani tabia yake na kutaka aadhibiwe. yeye ni binaadamu lakini professional alochagua haikubaliani na hilo.
hukuna atakae kaa kimya pale meneja anapochukuwa likizo au kurusha bonge la pati ilhali kampuni yake iko hatarini kufilisika.
hutegemei kumuona padre au shehe dansini akila denda na kuenjoy muziki ingawa nao ni binaadamu.
kila professional ina heshima zake na wajibu wake. na wajibu wa wabunge ni kutu,ia ,uda wao mwingi kulitumikia taifa letu na hatukuwalazimisha ila wametaka wenyewe na ndio maana wanalipwa mishahara minono, hatukwapa kura zetu na hatuwalipi kufanya maonyesho ya nguo.
Watu wanaodai kwamba wabunge hawatakiwi kufanya hivyo wana chuki zao binafsi.Wabunge ni human being na wana haki ya kusocialize kama watu wengine.
ReplyDeleteMe binafsi sioni tabu kama event imefanyika Saturday night.
wewe unayedai wangekua wanasoma vitabu. we huwa jumamosi usiku unasoma vitabu????????????
Kama event ingeendeshwa jumatano asubuhi hata mimi ningemend coz hiyo ni mida ya kazi.
Wabunge jiachieni achaneni na haters hata mkitaka kuwa na disko lenu kila week end hiyo ni poa ila mradi muwe na wake zenu na waifu zenu
GOB BLESS TZ & IT'S PEOPLE!!!
Riiiiiiiiidiculous!!!!
ReplyDeleteAnon was Mon Jul 13, 12:02:00 AM Mungu akubaliki make umeelezea kinaubaga issue.
ReplyDeleteMimi nimesema nikaambiwa nina chuki binafsi, mwingine anauliza kama ninasoma vitabu J'mosi. Mimi nisome nisisome it doesn't matter ila ninachoelewa ni kwamba nafasi ya ubunge inakuja na sheria za kutojitakia.
Kwamba wabunge wanatakiwa kusoma vitabu, magazeti, miswada ni obvious. Kama hawafanyi hivyo basi yule aliyesema the country is doomed is right on the money
Watu wengine ni wavivu sana wa kufikiri..hivi kuna ubaya gani mbunge kujiburudisha baada ya kazi ya wiki nzima ya kupitia bajeti za wizara mbalimbali?Ni haki ya kila binadami kupumzika na kujipa burudani baada ya kufanya kazi nzito. Mi nafikiri tuwapime hawa jamaa kwa utendaji wao na umakini wao katika kuibana serikali kwenye masuala mbalimbali yenye manufaa ya nchi na sio wanafanya nini jumamosi wakati wa mapumziko yao. Ni muhimu kwa kiongozi kuwa na maadili nje ya ofisi na asifanye mambo ya ajabu na yenye kutia aibu, lakini kushiriki kwenye maonesho ya mavazi mimi sioni kama ni kitu cha ajabu.kila kitu kina wakati wake, vitabu vina wakati wake na burudani pia zina wakati wake.Watu wanapenda sana kurukia mambo bila ufahamu wowote.Ndugu zangu nawashauri mfuatilie mijadala ya bajeti inayoendelea bungeni na muwakosoe wabunge kwa kile kinachopitishwa huko.Nina wasiwasi mkubwa watu wengi waliojifanya wanakosoa hata hawajui kama sasa hivi kuna bunge la bajeti na wala hawajui mijadala gani mizito inayoendelea bungeni, nyinyi mnasubiria vitu vya kukosoa tu. Kuna mtu alishasema watanzania tunahitaji akili zetu zioshwe na omo ili tuweze kubadili mitazamo yetu.
ReplyDeleteBUNGE:
ReplyDeleteThere are 300+ MPs katika composition ya wafanyibiashara, walimu, wakulima, wanamichezo, wanasanii, waimbaji, waandishi wa habari, wanasheria, madaktari, wanajeshi, wanausalama, wachumi, list ni ndefu sana.
Kwa hiyo basi katika wakati wao wa ziada baada ya kazi ya wiki nzima wanahaki ya kujiburudisha au kuburudishwa kama vile mimi na wewe unayesoma post hii yangu sasa hivi. Wabunge hawatokani na kundi la malaika kwamba hawawezi kufanya yale mambo wanayoyamudu ati tu ati wao ni waheshimiwa, la hasha wanahimahitaji ya kawaida kabisa kama vile alivyo binadamu mwingine yeyote.
Mwisho, kwa wale wanaohoji hii leo nadhani ni wafupi wa kumbukumbu, maswala ya maonesho ya mavazi, kutandaza soka, jogging, muziki nk hufanyika kila mara kwa wabunge.
Ninawatakia waheshimiwa wabunge letu tukufu kila heri.
Inatia kichefu chefu kabisa kuona.. ndo tuliwachagua wakafanye caltwalk huko dodoma?
ReplyDeletesawa ni binadamu lkn wafanye mambo yao kwa wakati mwengine sio kipindi kama hiki wanachotakiwa wafanye kazi.
Halaf nani aliaandaa hili zoezi zima.Nadhani si pesa za walala hoi.
Napenda niwajibu Anons wa Mon 05:40:00 AM na Mon 02:48:00 AM, Mimi nafikiri nyie ndo mmekuwa na kumbukumbu fupi au hamjafikiri implications za hivi vitu.
ReplyDeleteHakuna mtu anayesema kwamba wabunge wasi-socialize, au wabunge sio binadamu; kila mtu anajua social life is part of any human creature.
Issue ni kwamba kila professional ina limitations zake. Kwahiyo ni sawa wakienda strip clubs? Kwa sababu ni social life au?
Yule anon aneyesema tuwapime wabunge kwa uwezo wao wa kuibana serikali, hapo sasa ndo unaji-contradict. Ukweli ni kwamba hawa watu hawafanyi hivyo, wabunge wetu for the most part wanaenda Bungeni kukeshini na kurudi nyumbani. Trust me, kama wangekuwa wanafanya kazi yao inavyotakiwa watu wasingekuwa wanalalamika. Wala mimi na wewe tusingekuwa tunaandika kutokea ughaibuni.
The truth is the country is in a mess. Kama wabunge wa nchi zilizoendelea wako busy kuangalia nini kifanyike kuendeleza nchi zao nafikiri wabunge wetu they have to be twice as much...ila they are doing nothing...zero
Sorry nimeandika gazeti ila I am outraged..
AMA KWELI SASA NIMEAMINI UWEZO WA KUFIKIRI WA WATANZANIA UKO CHINI!! WABUNGE KUFANYA SOCIAL INTERRACTION KAMA HIZI NYIE MNAONA TATIZO AU NI BCOZ MNA WIVU. HATA MKITOA MAONI MAZURI HAMTAELEWEKA KUTIKANA NA MAWAZO HASI MLIYONAO.
ReplyDelete