Mkuuwa mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela (kushoto) akikabidhiwa simu za mkononi pamoja na fulana zilizotolewa na Kampuni ya Simu ya Tigo ikiwa ni sehemu ya mchango wao wa sh. milioni 50 kwa Chama cha Wakulima Tanzania (TASO) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kuanza Agosti Mosi mjini Dodoma. Anayekabidhi mchango huo ni Meneja Uhusiano wa Tigo, Bw. Jackson Mmbando
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela (kushoto) akikabidhiwa fulana zilizotolewa na Kampuni ya Simu ya Tigo ikiwa ni sehemu ya mchango wao wa sh. milioni 50 kwa Chama cha Wakulima Tanzania (TASO) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kuanza Agosti Mosi mjini Dodoma. Anayekabidhi mchango huo ni Meneja Uhusiano wa Tigo, Bw. Jackson Mmbando

Mkuuwa mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela (kati) akifurahia baada ya kukabidhiwa simu za mkononi pamoja na fulana zilizotolewa na Kampuni ya Simu ya Tigo ikiwa ni sehemu ya mchango wao wa sh. milioni 50 kwa Chama cha Wakulima Tanzania (TASO) kwa ajili ya maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kuanza Agosti Mosi mjini Dodoma. Kulia meneja husiano wa Tigo, Bw. Jackson Mmbando anayekabidhi mzigo huo
TIGO KUDHAMINI
MAWASILIANO YA MAONYESHO YA KILIMO KITAIFA DODOMA.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetangaza azma ya kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo katika kila mkoa hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Tigo Bw Jackson Mmbando jana mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kuitambulisha Tigo kuwa mdhamini mkuu katika eneo la mawasiliano wakati wa maonyesho ya kilimo maarufu nane nane ambayo mwaka huu yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.

Bw Mmbando alisema kuwa Tigo ni wadhamini wakuu wa mawasiliano katika maadhimisho ya maonyesho ya Nane Nane 2009 na kwamba wanategemea kujifunza mambo mengi ambayo kwa hakika ni changamoto ndani ya kilimo nchini.

Amesema Tigo itaitumia fursa ya kuwa mau katika maoneysho hayo ili kujifunza na kuzijua changamoto zinazoikabili kilimo Tigo na kutafuta mbinu za jinsi ya kupambana nazo lengo likiwa ni kuimarsiha kilimo na kufanikisha azma ya seriklai kupitia kauli mbiu ya kilimo kwanza.
"Kwa sasa Tigo inaendelea kushirikiana na wadau wa Kilimo - TASO kuhakikisha kila mkoa unakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo kwa kujifunza mbinu mpya za kilimo ili kila mmoja aweze kujipatia chakula chake mwenyewe tukiwa na dhumuni la kuunga mkono kauli ya mwaka huu ya KILIMO KWANZA"Alisema Mmbando.

Aidha katika kuyafanikisha maoneysho haya hasa kimawasiliano ambayo tunaamini ni moja ya nguzo muhimu katika kuharakisha shughuli mbalimbali na kuongoza ufaniksi katika uwajibikaji wa kila siku wakati wote wa maonyesho Tigo tutatoa ushirikiano kuwezesha wadau wa kilimo kwa kutoa vitu vifuatavyo:-

Directors phone 7,
Exhibition officials phones 13,
Airtime of Directors 10 days 7,
Airtime of officials 10 days 13,
T shirts with Nane Nane logo (POLO) 250,
T shirts with Nane Nane logo (Round neck) 500,
Caps with Nane Nane (Logo) 250,
Public address system for 10 days,
Banners Main Gate/stage/in all main areas,
Radio/TV advertisements,
Printing of promotional brochures 10,000,
Build 3 water tanks in the Nane Nane ground.

Katika kuhakikisha wakulima wanakabiliana na changamoto za kilimo bora tunaamini watahitaji mawasiliano bora na gharama nafuu, hivyo huduma zetu za mawasiliano zitaendelea kubakia zile zele ambapo mteja atakaepiga simu ya Tigo kwenda Tigo atalipia shilingi 1 kwa kila sekunde atakayopiga simu siku za kawaida saa ishirini na nne kwa simu zitakazopigwa na mteja wa Tigo.

Mbali na gharama hizi nafuu bado Tigo tutaendelea na promosheni zetu ambazo kwa uhakikika zinasaidia kupunguza gharama na ukali wa maisha na kuwaongeza tija wakulima na wateja wengine kufanya mawasiliano mazuri ya kibiashara kwa muda mrefu kwa kujiunga na huduma yetu ya XTREME SMS, USIPIME, AU TIGO LIFE".

Mmbando alisema "Kwa unafuu wa gharama wakulima na wadau wengine wa kilimo watakaoshiriki maonyesho haya na hata ambao hawatoshiriki watakuwa na uhakika wa kufanya mawasiliano ya kupanua masoko,kutangaza mazao na huduma wanazozitoa bila ya kuwa na hofu huku wakiwa na uwezo wa kuokoa kiwango kikubwa cha fedha wanazoweza kuzielekeza katika matumizi ya shughuli nyingine".

Mwisho tunawaomba wadau wote wa kilimo kutumia fursa ya maonyesho haya kama njia muhimu ya kujitangaza na kuboresha shughuli zao ili kujiimarisha kiuchumi na hatimae kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la taifa hasa tukizingatia kwamba Kilimo bado kina nafasi kubwa katika pato taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2009

    Sijui sana kiswahili fasaha, lakini naadhani neno sahihi hapa ni MAONESHO, ambalo mzizi wake ni onesha. Na si MAONYESHO, kwani mzizi wa neno maonyesho ni ONYA.

    Mdau chiggs, Deslam

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2009

    Mimi hawa Tigo nawapendea kitu kimoja,mnawajali sana walala hoi, nyie ni wenzetu, manake Tigo kwa Tigo mnaongea basi tena, ole wako upige Tigo kwenda upande mwingine...

    ReplyDelete
  3. habari kaka michuzi pole na kazi za kila siku ningependa kuchangia kiswahili sahihi ambacho wanahabari wengi tunakosea ukweli ni kwamba sio maonyesho bali ni MAONESHO neno ambalo kama mdau mwenzangu aliesema linatokana na neno ONA lakini onyesha ni neno ambalo linatokana na neno ONYA. kazi njema.Tina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...