KWA KUTUMIA HUDUMA BORA YA KUTUMA PESA, HATIMAYE MDAU FATUMA SHEFA WA CHUO KIKUU CHA COVENTRY UNIVERSITY CHA UK AMEPATA KITITA CHAKE CHA DOLA 1000 (TSHS 1,300,0000) BAADA YA KUIBUKA MDAU WA MILIONI 6 WA GLOBU YA JAMII.
PESA HIZO AMEZIPATA LEO KWA KUPITIA MWAKILISHI WAKE BW. LUGAZO SEMDILI AMBAYE NI MUME WA MDAU FATMA SHEFA AMBAYE ALIKUWA MDAU ALIYEIBUKA WA MILIONI 6 KATIKA MTANANGE HUO.
ANKO NANIHII ALIKUWEPO WAKATI WA KUKABIDHIWA MSHIKO HUO WA NGUVU KUPITIA HUDUMA INAYOONGOZA YA KUTUMA PESA YA M-PESA YA VODACOM TANZANIA AMBAPO AFISA WA KAMPUNI HIYO YA SIMU RUKIA MTINGWA ALISIMAMIA MAKABIDHIANO HAYO LEO KWENYE MAKAO MAKUU YA VODACOM.
GLOBU YA JAMII INATOA HONGERA KWA MSHINDI NA PIA SHUKRANI ZA DHATI KWA VODACOM TANZANIA KWA KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUDHAMINI MDAU WA MILIONI 6.
JINSI HUDUMA YA M-PESA ILIVYOWEZA KUFANIKISHA CHAPA-CHAP MAKABIDHIANO HAYO, GLOBU YA JAMII INATOA MWITO KWA WADAU KWAMBA KATIKA MASUALA YA KUTUMA PESA M-PESA NI KIBOKO YAO KWANI IMEWEZA KUTEKELEZA AHADI YA VODACOM TANZANIA KWA MUDA USIOZIDI SEKUNDE 90. HIVYO WADAU MNAOTAKA KUTUMA PESA MSIPATE TAABU, M-PESA IPO KWA AJILI YENU.
mmmmh mimi nina wasi wasi nadhani kaka michuzi utakua umepanga kumpa huyu dada! naomba contact zake nimpongeze nami nina kizawadi changu nataka nimzawadie!
ReplyDeleteMMmmm, jamani hebu tupe kahistoria ka zawadi hizi, wakwanza alikuwa nani na alitoka wapi, nk kama hutojali
ReplyDeleteHongera sana Fatma.
ReplyDeleteha ha ha nimefurahi kumuona shem wangu hapa nimemmiss sana mpe salam nyingi bi lufana hongera ziwafikie voda kwa kutimiza ahadi.
ReplyDeleteHeee, Fatma mbona hatuambianiamambo mazuri hayooo?hongera sana dadangu na Mungu akubariki umalize shule salama. Rena-Ireland
ReplyDeleteHONGERA BI FATMA SHEFA LUGAZO. BWANA LUGAZO MWENYEWE YUKO MBALI NIPASIE MIE HATAKAJIALFU MOJA SHILINGI NAMI NIENDE KAVOKATION HAHAHA.
ReplyDeleteMDAU STOCKHOLM
Mashallah mama Lufa! Siamini macho yangu kama ni wewe! Hongera sana, kismati kilioje! kiraks
ReplyDeletewacheni mambo ya kupekenyuwa pekenyuwa zawadi zimesha tolewa na washindi ndio mshajulishwa .
ReplyDeleteMmmh mama UK baba kachukuz mzigo TZ - mh iyo ya mzee kala bingo - Hongera sana bi Fatma.
ReplyDeletelakini mbona hizi zawadi kila mara wanapata watu wa england tu?
ReplyDeleteDuh, kumbe Fatuma uliolewa!!! good, hongera zana, sikujua kama siku hizi uko ughaibuni unasoma, wale ndugu zako wengine nao wako wapi siku hizi? Nimewasahau majina kuna mmoja mweupe alikuwa bomba sana,ok usimsahau Mr. Shefa wa Mbagala kama namuona muda huu na miwani yake.
ReplyDeleteMdau wa Mkwakwani Sec. School miaka hiyooooooo!!!!!
nampa hongera nyingi sana mdau mama Lufa, namuona hapa baba lufa akipokea kitita ila namwambia asikitumie ampe mwenyewe mkewe maana si unajua tena kila siku matatizo bongo hayaishi.
ReplyDeletemdau Netherland
...Which word is most appropriate to express my happiness to you Fatma Lugazo, Congrats Love for this!
ReplyDeleteFatma mimi bado siamini, kuwa ushindi wako ulikuwa fair. Naamini kabisa ulitegesha kaprogram fulani hivi kukamata numba 6,000,000 kwenye counter.
ReplyDeleteKwa nini hukuweka mambo hadharani kuwa UK unasomea nini hasa?, Sasa si unajua mambo yatu pale nanihii, usiporudi na degree nzuri tutajua ulikuwa unapotezea muda mwingi kwenye blogu.
Halafu Michu shindano la mdau wa 6,100,000 mshindi anapata zawadi gani vile?. Nataka kujirisha na mchezo wenyewe. Najua kama dau ni $2000 Fatuma lazima ashinde tena Hahahahahah.
Mdau mwenzi hapa