anko nanihii akimpongeza Lugazo Semdili, mume wa mdau wa Milioni 6 wa Globu ya Jamii, Fatma Shefa, aliyempokelea mkewe zawadi ya dola 1000 kupitia huduma ya M-Pesa leo
Anko nanihii akimshukuru Rukia Mtingwa wa Vodacom baada ya kampuni hiyo inayoongoza ya simu za mkononi kutimiza ahadi yake ya kumdhamini mdau wa milioni 6 kwa kumzawadia dola 1000
simu ya Lugaza Semdili ikionesha kupokewa kwa zwadai hiyo ya mdau wa milioni 6 wa Globu ya Jamii kupitia huduma kabambe ya M-Pesa
simu ya mume wa mdau wa milioni 6 ya Globu ya jamii ikionesha salio lake kupitia huduma ya kisasa na bora ya kutuma pesa ya M-Pesa. Picha na Moiz Husein

Mdau wa Millioni 6 wa Globu ya Jamii, Fatuma Shefa, anayekula nondozzz katika Chuo Kikuu cha Coventry University Uingereza, hatimaye amekabidhiwa leo kitita chake cha dola 1000 kupitia huduma makini ya M-Pesa ya Vodacom

KWA KUTUMIA HUDUMA BORA YA KUTUMA PESA, HATIMAYE MDAU FATUMA SHEFA WA CHUO KIKUU CHA COVENTRY UNIVERSITY CHA UK AMEPATA KITITA CHAKE CHA DOLA 1000 (TSHS 1,300,0000) BAADA YA KUIBUKA MDAU WA MILIONI 6 WA GLOBU YA JAMII.

PESA HIZO AMEZIPATA LEO KWA KUPITIA MWAKILISHI WAKE BW. LUGAZO SEMDILI AMBAYE NI MUME WA MDAU FATMA SHEFA AMBAYE ALIKUWA MDAU ALIYEIBUKA WA MILIONI 6 KATIKA MTANANGE HUO.

ANKO NANIHII ALIKUWEPO WAKATI WA KUKABIDHIWA MSHIKO HUO WA NGUVU KUPITIA HUDUMA INAYOONGOZA YA KUTUMA PESA YA M-PESA YA VODACOM TANZANIA AMBAPO AFISA WA KAMPUNI HIYO YA SIMU RUKIA MTINGWA ALISIMAMIA MAKABIDHIANO HAYO LEO KWENYE MAKAO MAKUU YA VODACOM.
GLOBU YA JAMII INATOA HONGERA KWA MSHINDI NA PIA SHUKRANI ZA DHATI KWA VODACOM TANZANIA KWA KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUDHAMINI MDAU WA MILIONI 6.

JINSI HUDUMA YA M-PESA ILIVYOWEZA KUFANIKISHA CHAPA-CHAP MAKABIDHIANO HAYO, GLOBU YA JAMII INATOA MWITO KWA WADAU KWAMBA KATIKA MASUALA YA KUTUMA PESA M-PESA NI KIBOKO YAO KWANI IMEWEZA KUTEKELEZA AHADI YA VODACOM TANZANIA KWA MUDA USIOZIDI SEKUNDE 90. HIVYO WADAU MNAOTAKA KUTUMA PESA MSIPATE TAABU, M-PESA IPO KWA AJILI YENU.





















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2009

    mmmmh mimi nina wasi wasi nadhani kaka michuzi utakua umepanga kumpa huyu dada! naomba contact zake nimpongeze nami nina kizawadi changu nataka nimzawadie!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2009

    MMmmm, jamani hebu tupe kahistoria ka zawadi hizi, wakwanza alikuwa nani na alitoka wapi, nk kama hutojali

    ReplyDelete
  3. mama aishaJuly 16, 2009

    ha ha ha nimefurahi kumuona shem wangu hapa nimemmiss sana mpe salam nyingi bi lufana hongera ziwafikie voda kwa kutimiza ahadi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2009

    Heee, Fatma mbona hatuambianiamambo mazuri hayooo?hongera sana dadangu na Mungu akubariki umalize shule salama. Rena-Ireland

    ReplyDelete
  5. baba AishaJuly 16, 2009

    HONGERA BI FATMA SHEFA LUGAZO. BWANA LUGAZO MWENYEWE YUKO MBALI NIPASIE MIE HATAKAJIALFU MOJA SHILINGI NAMI NIENDE KAVOKATION HAHAHA.
    MDAU STOCKHOLM

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2009

    Mashallah mama Lufa! Siamini macho yangu kama ni wewe! Hongera sana, kismati kilioje! kiraks

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2009

    wacheni mambo ya kupekenyuwa pekenyuwa zawadi zimesha tolewa na washindi ndio mshajulishwa .

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2009

    Mmmh mama UK baba kachukuz mzigo TZ - mh iyo ya mzee kala bingo - Hongera sana bi Fatma.

    ReplyDelete
  9. lakini mbona hizi zawadi kila mara wanapata watu wa england tu?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 16, 2009

    Duh, kumbe Fatuma uliolewa!!! good, hongera zana, sikujua kama siku hizi uko ughaibuni unasoma, wale ndugu zako wengine nao wako wapi siku hizi? Nimewasahau majina kuna mmoja mweupe alikuwa bomba sana,ok usimsahau Mr. Shefa wa Mbagala kama namuona muda huu na miwani yake.
    Mdau wa Mkwakwani Sec. School miaka hiyooooooo!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 16, 2009

    nampa hongera nyingi sana mdau mama Lufa, namuona hapa baba lufa akipokea kitita ila namwambia asikitumie ampe mwenyewe mkewe maana si unajua tena kila siku matatizo bongo hayaishi.
    mdau Netherland

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 16, 2009

    ...Which word is most appropriate to express my happiness to you Fatma Lugazo, Congrats Love for this!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 17, 2009

    Fatma mimi bado siamini, kuwa ushindi wako ulikuwa fair. Naamini kabisa ulitegesha kaprogram fulani hivi kukamata numba 6,000,000 kwenye counter.

    Kwa nini hukuweka mambo hadharani kuwa UK unasomea nini hasa?, Sasa si unajua mambo yatu pale nanihii, usiporudi na degree nzuri tutajua ulikuwa unapotezea muda mwingi kwenye blogu.

    Halafu Michu shindano la mdau wa 6,100,000 mshindi anapata zawadi gani vile?. Nataka kujirisha na mchezo wenyewe. Najua kama dau ni $2000 Fatuma lazima ashinde tena Hahahahahah.

    Mdau mwenzi hapa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...