Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unatarajiwa kufanyika Sharm El Sheikh, Misri tarehe 15 hadi 16 Julai, 2009. Huu ni mkutano wa kawaida wa NAM ambao hufayika kila baada ya miaka mitatu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano huo.

Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za NAM unaofanyika tarehe 13 na 14 Julai, 2009.

Maudhui ya mkutano huo ni pamoja na Mtikisiko wa Kiuchumi Duniani; Mageuzi katika Vyombo vya Fedha Duniani; Mageuzi katika Umoja wa Mataifa na Migogoro ya Kisiasa Duniani.
Aidha, mkutano huo unategemewa kupitisha maazimio mbalimbali yaliyopendekezwa na mkutano wa Mawaziri huko Tehran, Iran mwaka 2008 na ule wa Havana, Cuba mwezi Mei, 2009.

Mhe. Waziri Membe ataambatana na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga Na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe. Ali Shauri Haji.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YANJE NAUSHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
13 JULAI, 2009

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2009

    ...angalau hili amewakilishwa na Membe...

    maana khaaaa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2009

    angalau, du...ingekuwa ulaya angekwenda mwenyewe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2009

    jamani, jamani hizi nchi maskini bado zinaendekeza siasa zilizokwishapitwa na wakati alimradi tu wafuje pesa za walipa kodi wao walio maskini. hii biashara ay kutofungamana na siasa ya upande wo wote ina maana gani baada ya vita baridi kuisha? ninaomba kuelimishwa kama kuna mdau aliye na welewa wo wote!

    ReplyDelete
  4. David VillaJuly 15, 2009

    Na mimi nakubaliana na waliochangia hapo juu namba 1 na 2,maana mmmhhhh......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...