



FAMILIA YA BALOZI MOHAMED MAHARAGE JUMA INACHUKUA FURSA HII KUWASHUKURU WOTE AMBAO WALIOWEZA KUSHIRIKI KATIKA MAZISHI NA KUIFARIJI FAMILIA KWA KUFIWA NA BINTI YAO MPENDWA FATUAI BINTI MOHAMED ALYEFARIKI JULAI 08, 2009 NA KUZIKWA SIKU HIYO HIYO.
FAMILIA INATHAMINI FADHILA HII KUBWA YA UPENDO KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU NA INAWAOMBEA NYOTE KHERI NA AMANI NA FAMILIA ZENU.
INA LILAHI WA INA ILAHI RAJOOON
MOHAMED MAHARAGE JUMA
jamani mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi amina..jamani dada mzuri huyuuu!!halafu mdogo mungu wangu eheeeee poleni jamani wafiwa
ReplyDeleteInna lillahi wa inna ilayhir rajiun, Poleni sana wafiwa.
ReplyDeleteInna Lilah wa Inna Ilaihi raajiuun.
ReplyDeletemungu amlaze roho yake mahala pema peponi,imekuaje jamani ajali ama ni nini mbona mapema sana jamani kifo hichiiiiii yesu wanguuuuu
ReplyDeleteHili janga jamani lipo na linaua kwelikweli tujihadharini. ni janga la dunia na halijapata ufumbuzi bado
ReplyDeletePole mno na familia yako yote MMJ.
ReplyDeleteTulimpenda lakini muumba alimpenda zaidi. Tunaamini yuko kwenye maisha mema uko aliko. Amin Mdau Ottawa. CA
Pole sana ndugu yangu kwa kuondokewa na binti yako, Mwenyezi Mungu alilaze roho yake mahala pema peponi. bll
ReplyDeleteSi vyema kabisa anapofariki mtu kumsema kwa ubaya kadhalika kumtajia siri zake au kumvumizia usiokuwa na uhakika nayo, ndugu yetu mtowa maoni wa tano nakukusudia wewe hasa, si uungwana na sio mila zetu hizo, utanufaika na nini na uliyosema zaidi ya kuwazidishia maumivu wafiwa hata kama usemayo ni kweli kulikuwa na haja ya ulimwengu kujua hususan sasa ameshaondoka ulimwenguni? jamani na tuwe wastaarabu:
ReplyDeleteSalaam wote napenda kuweka bayana kwamba marehemu alipata food poisoning baada ya kula nyama choma (sehemu jina nalihifadhi kwa kuzingatia sheria) akiwa na nduguze na marafiki vijana zaidi ya kumi katika birthday party 14Juni 2009,yeye na wengine zaidi ya sita walitapika na kuharisha kwa zaidi ya siku tano,wenzake hali ilirejea kawaida ila yeye utumbo ulijipinda na kujaa nyongo tumboni na kutoboka hali iliyosababisha operesheni tatu Hindu Mandal na Muhimbili za kukata na kuunga utumbo mdogo na mkubwa, aidha maini na mafigo yake yaliharibika sana kwa sumu. Wataalamu wanasema kilicho sabisha mauti ni SEPTIC SHOCK kutokana na majeraha ya ndani na nje. Mohamed Maharage Juma, Mzazi wa marehemu ahsante
ReplyDeletewewe unajijua utaondoka vipi ama, ni kunyamaza tu naokuomba khatima yako iwe ya salama, na tuendako five second ijayo hujui nini kitakutokea,
ReplyDeletehuyu msichana amefariki baada ya kula samaki pale kawe club inahofiwa alikuwa na poison either alivuliwa kwa njia isiyohalali au alikuwa ameharibika; wenzie waliharisha na kutapika yeye hakutapika wala kuharisha after few days akaumwa tumbo kumbe kaoza utumbo akafanyiwa operation pale hindumandal akakatwa kipande cha utumbo kilicho haribika after few days tumbo likavimba tena so they had to rush her muhimbili haikuwa rizki mungu akachukua kiumbe wake, so hapo aliyepelekea kifo chake ni kawe club na samaki wao au hindu mandal walikomkosea operation? i t doesnt matter now ndio tumeshampoteza masikini.
ReplyDelete...mh
ReplyDeletembona watu mmeanza kuleta stori umu mara samaki,mara janga la dunia
nini sasa?ametangulia mbele ya hukumu na kila mtu atafika tu,swala ni kujiandaa wakati wote tengeneza na Muumba wako
ni hayo tu
Poleni sana family ya Balozi Maharage. Hawa mahayawani wanaoandika upuuzi huu na hakika hawajazaa bado, na hawajui uchungu wa kizika mtoto! Kwa wale wanazuoni iliyobaki ni kumwombea mwanetu huko alikopumzika na siyo kuanza kuandika pumba. Wote tumetoka kwa Allah na kwake ndiko tutarejea! Inshaalah Mwenyezi mungu awape tahafif na uvumilivu katika wakati huu mgumu. Sote tuko nanyi.
ReplyDeletePole Balozi wetu kwa statment hiyo uliyoitoa .. naomba hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika..
ReplyDeletePOLENI SANA NDUGU WAFIWA HIYO NDIO KAZI YA MWENYEZI HAINA MAKOSA
ReplyDeleteNAOMBA MSIJIBU HAYA YA UMU KWANI UMU KUNA VICHWA VINGI NA SIO TIMAMU ZAIDI NI KUJIPA UCHUNGU NA MAWAZO YA MPENDWA WETUU
TUNASHUKURU KWA TAARIFA HII YA MSIBA INNA LILLAH WAINNA ILAH RRAJIYN
MWANA KIJIJI FOTO BARAZA BLOG MAKINI
poleni sana wafiwa, ama hakika kwake tutarejea. Kisomo lini(40)
ReplyDeleteHakuna marehemu asiyeacha hadithi. Nawapa pole sana familia ya mahemu. Ninachomba tuu kama imesha thibitishwa marehemu alikula sumu katika chakula basi inabidi serikali ifuatilie hilo ili wengine tusije dhurika. Hapa ndio unatakiwa uonyeshwe umuhimu wa elimu ya usafi katika chakula nchi yetu ni ya joto hivyo genetation ya bacteria katika chakula ni kubwa sana. Kwaufupi tu wa ufahamu bacterial generation kwa dakika ni mara mbili ya idadi ya hao bakteri. Yaani kama kuna bakteria kumi katika chakula baada ya dakika watakua 20 na baada ya dakika mbili 40 piga hesabu baada ya saa moja. Na vyakula vya nyama na maziwa vikiwa baridi chini nyuzi joto 65 chini masaa matatu huwahavistahili kuliwa tena. Salmonera au coli bacteria wanaweza kutekteza jiji kwa muda mchache sana. Serikali inabidi iweke mkakati kwenye hilo. Balozi hili limeanzia kwako basi fanyakazi ili wengine wasije dhurika pole sana mungu atakuafu na machungu hayo wewe pamja na familia yako
ReplyDeleteThis is such a shock!!! I went to school with Fatuai at Academic International school, she was a lovely girl, young and beautiful. My heart goes to the whole family!! Inna lillahi wainna ilaihi rajiuun...I shall include her in my prayers always, being a friend and a fellow muslim.
ReplyDeleteThis is shocking news!! Fatuai was a lovely girl, young, good hearted and beautiful...I went to school with her at Academic International School. My heart goes out to the family!! Inna lillahi wa Inna ilaihi rajiuun...I shall include her in my prayers always, being a friend and a fellow muslim. Poleni sana Fatuai's family!!
ReplyDeletei loved u Fatu..but God loved you more..
ReplyDeleteil never forget our big brother moments....
My heart goes out to your whole family especially ur mum, Teddy bear and ur dad..
Inna illahi wah inna irrajiun