Waziri Mkuu mstaafu Mh Edward Lowassa yuko alikuwa Bonn, Ujerumani, kwa matibabu ya macho ambapo amefanyiwa upasuaji wa jicho lake la kushoto na anaendelea vyema. Anatarajia kurejea nyumbani wiki ijayo.
Pichani mdau Aboubakar Liongo wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio DW alipokwenda kumjulia hali hotelini kwake akiwa benet na mai waifu wake Mama Regina Lowassa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2009

    Wanaongoza nchi yanawashinda, hawawezi kuleta huduma kwa wananchi, wao wakihitaji huduma wanaenda Ujerumani, hawana uchungu na mtu wa hali ya chini, aibu.

    ReplyDelete
  2. NautiakasiJuly 08, 2009

    Hata aende wapi muda ukifika atarudisha namba tu...!Wako walojaribu hata kupumulia mashine na haikuwa kitu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2009

    HIVI MIMI NINA MATATIZO GANI? MAANA NILIPOISOMA TU HII HABARI NIMEJIKUTA NAPANDISHA HASIRA NA SIJISIKII TENA KUSOMA HABARI ZILIZOMO NDANI YA HII BLOG, JAMANI NAOMBA MNIOMBEE ROHO YA HASIRA INITOKE

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2009

    Mamaa nimezikubali strategies zako.....ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO...USITEME MATE NDANI YA BUS.....dakika moja ni nyingi sana kwa bidhaa adimu kama hiyo uliyokomaa nayo....BIG UP MAMAA!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2009

    Naona Mama Lowassa amependeza sana kwenye Blaus na Jinsi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2009

    mdau 8:22am

    hauko peke yako mbona tunafanana?yan ghafla hal ya hewa imebadilika apa!!

    ...ithink hii hali ni kawaida asa unapoona nchi inaliwa na watu wachache bila HURUMA.poa tu kuna sehemu noja tu ya kutoa hukumu ya milele

    suruali zinakuhusu nini wewe!!

    "##@@$5***<:&**

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2009

    Nautiakasi, hata wewe utarudisha namba tu, wote safari moja, isikose ukawahi wewe. Mwenye hasira na hii habari avimbe mpaka apasuke, chuki za kishabiki zisizo na kichwa wala mguu. Kama unaishi tanzania, ndiyo unajua kwamba serikali sasa inammiss huyu jamaa. Tunakuombea upone haraka baba, wananchi wa Tanzania bado wanategemea mchango wako sana, usikate tamaa na wapuuzi wachache.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 08, 2009

    Jamani tuacheni chuki na wivu, Dunia Nzima kuna tofauti kati ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mwananchi wa kawaida, Hata ungekuwa wewe Mmatumbi ndio waziri mkuu mstaafu ungetibiwa huko, Na Yesu alisema " Asiye na dhambi na awe wa kwanza kumpiga kwa mawe mdhinifu" watu wote wakatimua,
    Nawasilisha

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 08, 2009

    Ugua pole mzee wetu, na mama Pamela pole kwa kuuguza. Mungu awabariki na kupata nafuu na pia safari ya kurudi nyumbani.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 08, 2009

    Mie huwa naona raha sana kuwaona Mr & Mrs pamoja iwe ni kwenye furaha au ugonjwa i just like that despite of ll that went through

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2009

    nani analipia hizo gharama za hospitali?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 08, 2009

    USIJALI YOTE MAISHA MAMA NI MWENDO WA KUDUNDA KWA MMOJAMMOJA,HUKU IKTOLEWA NA BWANA YESU NDIYO BINADAMU ANAELEWA MAANA YA MAISHA WHAT IS MONEY BY THE WAY WHEN YOUR GOING TO BE BURIED IN A MIN BABY KILA MMEA HUOTA KUNAWIRI NA KUSINYAA.
    K'ZOO CONCORDE MABONDE KWINAMA

    ReplyDelete
  13. PhatlorenzoJuly 09, 2009

    Shutuma nyingine ni very low na zinasikitisha. Hivi jamani huyu mzee pamoja na weakness zake tunataka kusema hawezi kujilipia nauli na gharama ya kutibwa macho Ujerumani? Simtetei Mh. Lowassa lakini naona hatumtendei haki. I have known this guy since akiwa Mkurugenzi wa AICC, na baada ya hapo ameshika nyadhifa nyingi tu serikalini, na vile vile ana connections nyingi tu na marafiki wenye influence ndani na nje ya nchi. Kwa nini tunakuwa wepesi wa kutupa mawe wakati sisi wenyewe tunaishi kwenye nyumba ya kioo? Kwa jinsi ninavyoelewa mimi...procedures ambayo yeyote ya upasuaji unayofanyiwa hospitalini halafu madaktari wakakuruhusu kurudi nyumbani kwa jina lingine (Same Day Surgery)...sio complicated na huwa hazi cost gharama kubwa kama zile za mgonjwa kulazwa Hospitalini (inpatient). Hii picha hapa inaonyesha kwamba Mzee Lowassa yuko hotelini kwake...Hivi kwa mfano kama ameenda kufanya lasik eye surgery procedure ambayo ni very reasonable plus room and board Ujerumani na tiketi ya ndege kwa former PM. Tunataka kusema Lowassa hana hiyo hela ya kulipia hizo gharama? Naomba tusiwe masikini wa kufikiria kiasi hiki.
    Hivi kweli tumefikia hatua ya kudhalilisha watu namna hii...kwa ku question gharama zake na ni nani anayezilipa? Lowassa had money before becoming a PM and before EPA, Lowassa had lots of $$ way before then...kwa nini tunakuwa hivi? Wale wanaomjua kuanzia Arusha wanafahamu vizuri.
    Nafikiri tuki direct hizi nguvu kwenye vitu ambavyo vita yield positive outcome tutakuwa better off siku zote.
    Phatlorenzo-Minnesota

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2009

    ha ha haaaaaaaaa mie msikilizaji tu semeni nyie

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 09, 2009

    phatlorenzo..umesema yote..bless u

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...