Millen Magesse (mwenye njano) na Miss TZ 2008 (mwenye kijani) wakipozi na warembo wanaowania taji la Miss Temeke 2009 kwenye mazoezi yao TCC club, Dar

MWANAMITINDO Millen Magesse atatoa zawadi kwa mshindi wa kwanza wa Redd's Miss Temeke 2009 ya maandalizi yote ya ushiriki wake wa Vodacom Miss Tanzania baadaye mwaka huu, ikiwa ni zawadi ya kwanza kutangazwa katika mashindano hayo ya Kanda.

Akizungumza katika kambi ya mazoezi ya washiriki hao juzi, Happiness ambaye pia amepata kuwa Miss Temeke mwaka 2001 na Miss Tanzania mwaka huo, aliwaahidi warembo hao mbele ya kamati ya Miss Tanzania kuwa mbali ya vivazi vyote, pia atasimamia vipodozi sanjari na utengenezaji wa nywele zake.

"Mshindi nitamwandaa kuanzia nywele hadi ya ukucha nini mavazi na viatu vyake jukwaani", alisema Happiness ambaye hujulikana pia kwa jina la Millen katika kazi zake za mitindo anazozifanya nchini Afrika Kusini na sasa akijiandaa kwenye kuanza mkataba mkubwa wa mavazi nchini Marekani.

"Nafanya hivi mahsusi kama shukrani zangu za kumbukumbu za mlezi wa Miss Temeke, marehemu Jargis Merali ambaye alinidhamini kila kitu baada ya kushinda Miss Temeke na kwenda kushiriki Miss Tanzania, amefariki nikiwa Afrika Kusini sikuwepo nafanya hivyo kama kumbukumbu kwake", alisema Magesse.

Mwanamitindo huyo ambaye jukwaa lake la kwanza katika shughuli za urembo zilizofikia kumtambulisha Kimataifa, ilikuwa katika Miss Temeke aliambatana na kamati ya Miss Tanzania ambao walitoa miongozo mbalimbali kwa warembo hao ikiwemo sheria, kanuni na taratibu zinazoendesha mashindano hayo.

Awali Lundenga, aliwaeleza umuhimu wa kujijua katika jamii, kuepukana na vishawishi vya ulaghai ili washinde na kauli mbiu ya Miss Tanzania mwaka huu ambayo ni kukuza utalii wa ndani. Miss Tanzania, Nasreem Karim aliyehudhuria hafla hiyo kwake aliwaeleza uzoefu wake zaidi katika kipindi chake cha urembo na ushiriki wake wa mashindano ya Dunia.

Redd's Miss Temeke inafanyika Agosti 1, mwaka huu katika ukumbi wa TCC Chang'ombe ambapo mbali ya Redd's, wadhamini wengine ni Vodacom Tanzania, Aurora Security, 88.4 Cloud's FM, Screen Masters, Mariedo Boutique, Sofia Records, Raque Studio Valley Springs, gazeti la Jambo Leo na Renzo Salon.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2009

    Siku hizi anaitwa Millen, Hilo jina limetika wapi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2009

    Miriam Magessa from nanii....now........Utandawazi bwana ww Anon 14:00 PM vp???

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2009

    Millen jamani Happiness lilikuwa baya au? hebu aseme wazi jina lake maana kubadilisha jina ukubwani lazima uwe na reasons zako any way she is cute ila kubadilisha jina is grrrrrrrrrr

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...