Miss Ukonga Shoma Nkwabi
KAMATI ya kumtafuta mrembo wa Kanda ya Ilala imemtimua kambini aliyekuwa mshiriki wa kambi ya Redd’s Miss Ilala Shoma Nkwabi kutoka kitongoji cha ukonga kutokana na utovu wa nidhamu.

Akizungumzia tukio hilo jana jijini Dar es Salaam Mkuu wa nidhamu wa kambi hiyo iliyopo kwenye Hoteli ya Lamada & Apartments, Alex Adel alisema kuwa Nkwabi ambaye alikuwa ndiye Miss Ukonga ameondolewa kwenye orodha ya washiriki wa kinyang’anyiro hicho na kwamba uamuzi huo umeanza kutekelezwa.

Adel alisema kuwa ingawa kamati imesikitishwa na kitendo hicho lakini haikuwa na jinsi kutokana na utovu wa nidhamu wa hali ya juu uliooneshwa na mshiriki huyo wa Redd’s Miss Ilala.

“Ni kweli Nkwabi ameondolewa kwenye orodha ya washiriki wetu kutokana na sababu hizo na kwamba kitendo cha kumfukuza hakitoleta pengo lolote kwani warembo waliopo wana sifa zote za kuifanya kanda hiyo kutoa Miss Tanzania kwa mwaka 2009,” alisema Adel. Shoma hakuwahi kuripoti kambini hata siku moja toka kambi ianze kiasi cha siku 10 zilizopita.

Akizungumzia kuhusiana na hali ya kambi hiyo iliyoanza Julai 14, mwalimu wa warembo hao Regina Mroni aliyewahi kuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2006 alisema jana na juzi washiriki hao waliendelea na mazoezi ya kutembea na kucheza kama kawaida na kwamba wanaendelea vizuri.

“Jana warembo wote walipiga picha za video kwa ajili ya promosheni na kupata fursa ya kutembelewa na ndugu, jamaa na marafiki ili kubadilishana mawazo,” alisema Mroni.

Leo kamati hiyo ya kumtafuta mrembo wa Kanda ya Ilala itakuwa na mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari na Maelezo ili kuwatambulisha rasmi warembo hao, kutangaza tarehe rasmi ya mashindano na kuelezea mikakati mbalimbali waliyojiwekea ili kushinda taji la Miss Tanzania mwaka huu.

Shindano la kumtafuta mrembo wa manispaa ya Ilala mwaka huu limedhaminiwa na Redds original akiwa mdhamini mkuu.

Wengine waliodhamini ni Vodacom, Lamada Apartments, Syscorp group, CXC Africa,Vam general Supplies,Travel Partners, Primetime,Sofia production, Fabak fashion,Clouds Fm, channel ten, Valley springs na www.issamichuzi.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    Tunaomba mtueleze huyu dada amekosean kitu gani.Hii itasaidia kwa wale wadogo zake watakaoshiri mashindano hayo miaka ijayo kujifunza kutoka kwake kuwa nini wafanye na nini wasifanye.Iwapo kosa lake halitowekwa hadharani basi hapakuwa na sababu ya kutueleza kuwa katimuliwa.Uamuzi wa kutimuliwa unakwenda sambamba na kosa alilolifanya kama peanutbutter and jelly

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2009

    yaani wewe umetoa point kabisa lazima tujulishwe hilo kosa otherwise there is no point ya kutuambia kwa ufupi tu wengine watajifunza vipi kusudi wasirudie utumbo kufanya utumbo kama alioufanya mwenzao hata kama ni kali sana kuna jinsi ya kudokezea bila kutoa maneno makali sana au vipi kumbukeni no secret under the sun itajulikana tu kwa hiyo bora tu kutujulisha asante mkereketwa!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2009

    Haya wadau muko wapiiiii!!!!!!!!!, kwanini tuko kimya, hatusemi kitu kuhusu mashindano haya. Kwani sioni tafauti ya mashindano haya na yale ya sexiest. Yote ni mambo ya kipuuzi tu. Tuache unafiki, huku nako ni kuwafundisha dada zetu kujiuza. Au kwa sababu tunapenda kuwaona wanawake nusu uchi wakiwa wamevaa chupi za under wear ndio tuko kimya. Au kule mlikuwa na kisasi na dada DEVA ndio mkashambulia kwa nguvu. Amkeeni mkemee na hli, huu sio utamaduni wetu.

    ReplyDelete
  4. KUKOSA KUUDHURIA KATIKA MAZOEZI KWA SIKU 10 LABDA ALIKUWA ANAUMWA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2009

    Anaonekana ni msichana mwenye akili. Hakuingia kambini kwa sababu ameona kuwa ni "mashindano" yasiyo na maana na yatampotezea muda wake. Mbona hana nafasi ya kujieleza???

    ReplyDelete
  6. Jaman mrembo wawatu sio siri kama nikosa dogo alilo fanya plz kamati imifikirie kwan she is so beuty so plz kama vipi mumsamehe.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2009

    Atakuwa kamnyima mtu tu huyo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 20, 2009

    hulka za kijinsia: mwanamke ni kiumbe anayependa sana mwili wake na pia kupenda wengine wauhusudu kwa maana ya admire (sio tu na wanaume bali pia wanawake wenzake). mwanamke anapenda sana kuwa admired si kwa sababu ni malaya wala nini, ni hulka. ndio chanzo cha kujitahidi kadri utamaduni unavyoruhusu kuonyesha sehemu za mwili wake awapo hadaharani (mapaja, vitovu, maziwa, mgongo, nk)pamoja na mapambo kemkem (hirini, mikufu, pete vidole vyote, nk). Na ni kweli mwanamke ni kiumbe mwenye mvuto. alitengenezwa hivyo kutoka katika upande mmoja wa Adam!!
    Mfano (kwa wanaume tu) angalia ukiwa unavinjari mitaani na mke au hawara (girlfriend) mkapishana na mwanamke aliye na mvuto na amejikwatua vizuri kisura na kimavazi: nyote wawili mtamtumbulia macho kwa chati kwa sababu tofauti, wakati baba atakuwa anawazia ingekuwa mali yake (ndio hayo ya akina wababa), mama atakuwa anajiuliza maswali mengi kama na yeye anaonekana hivyo, kama angekuwa na wasaa angemuuliza nani kamshonea nguo yake, nk.
    Ninafikiri u-miss au tuseme fani ya ulimbwende inafuata mantiki hiyo; hawa mabinti wanatoa burudani kwa kuchangamsha macho ya watu (wanaume na wanawake) na papo hapo kama wasanii wengine wanataka kuwa admired kwa huo u-jinsia uke wao, of course, bila kusahau mshiko!!
    Wanaume ni watu wa maguvu ama ya pesa au ya mwili, na kuhusian na maumbile mahali pa kuwa admired ni katika mchezo wa ngumi. mnakumbuka bingwa wa zamani wa ngumi, Mohammed Ally, hakuwa admired kwa sababu ya sura yake, bali kwa uwezo wake wa kutupa masumbwi!!!!!! mke na mume huyo huyo mkipishana na mwanamume inaweza ikatokea msikumbuke alikuwa amevaa nini iwapo mtu anawauliza iwapo mmekutana na mtu wa aina fulani!!! ni masuala ya kimaumbile asilia. wadada na wamama mnaweza kunisahihisha!

    ReplyDelete
  9. Nasikia alimkataa jamaa....wabongo bwana, hongera sana dada yangu kwa ushujaa wako, ikiendelea na mtindo huu, utafika mbali vilevile kale ka-ugonjwa katakupitia mbali.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 20, 2009

    Mzee Michuzi tafadhali tuambie huyu dada alifanya nini." kukosa nidhamu ya hali ya juu" vipi!.Huyo dada is very beautiful naona lazima kutakuwa na jealousy ya aina fulani hivi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2009

    wabongo wengi walifyonza maji wakiwa tumboni ndio maana wanaona kutokuwasili kambini kwa muda wa siku 10 bila kutoa taarifa ni sawa kabisa hata kama kuna sababu nyingine lakini hio tu inajitosheleza kumtimua na ikiwezekana na kifungo kabisa kwavile hao tukiwachekea ndio kesho wanaenda kutuwakilisha kwenye miss world siku ya mashindano kisa bf wake hajampigia simu analeta kisirani mwisho wanaishilia kushika mkia tu kwavile ni UNPROFESSIONAL

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2009

    I know the lady, ana msimamo mkaali sana na sio rahisi kina nanii kutaka kumchezea. Keep it up dada waache waseme eti huna nidhamu, wadau tunajua hakika nani hana NIDHAMU.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 21, 2009

    Nafikiri kweli atakua kamnyima mtu,si mshayaona kwenye miss BONGO(UKWELI USIOJULIKANA)?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 21, 2009

    Kili unanikumbusha mchumba wangu wakati fulani aliwahi kuniambia chuoni walikuwa wanambembeleza akashindanie u-miss! Nikamwambia siku utakapojaza hiyo fomu nitafutie na mchumba mwingine kabisa na nilikuwa serious! Namaanisha haya mabo ya kuombwa na kulazimishwa ngono kwenye mchakato na baada ya mashindano ya urembo yapo sana! Na unajua Hulka ya mwanamke na udhaifu alionao naamini ni wachache sana ambao hawagongwi na mapedeshee kibao kutokana vitu kama mshiko na tamaa nyingine! Wewe Bf huna uwezo wa kununua gari linakuja pedeshee linamwambia mmego mmoja gari demu mwenye tamaa kweli atakataa kisa tu keshakuwa maarufu!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 21, 2009

    shosti kila likuepukalo wala usisikitike kama mzuri ni mzuri tu huna haja ya kutembea nusu uchi eti wengine waaprove, anaejimini kwa uzuri hasa huwa hana sababu ya kujionesha halafu watu wamkoments,

    asikudanganye mtu wazuri wote wameolewa

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 21, 2009

    Napingana na wewe! Wasichana wengi wazuri kwa silimia kubwa hawajaoelewa na kama wameolewa matatizo mengi kwenye familia zao maana kila kitu anachofanya ana refer uzuri wake ama wengine ndio hao unasikia leo kaolewa baada ya miezi 4 au 6 ndoa imevunjika kutokana na tamaa za kijinga jinga! Unaolewa unaanza kumwambia mumeo lazima anunue gari hata kama pesa hana na kumtolea mifano ya mapedeshee waliowanunulia vidosho wao magari kutokana tu na tamaa za kuwamega tu na si kuwaoa! Kwani wakati hajakuoa hukujua kuwa ana uwezo wa kukununulia gari au hicho kitu ya milioni 10 unachotaka?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 22, 2009

    Kama kweli kakataa kumegewa personality yake, afadhali atoke nje kuliko kuvaa taji la aibu. Bali tuwe macho waTZ, tusiwapake matope dada na binti zetu kama hatuna evidence ya ubahau katika mashindano haya. tusijawe na shuku kwani tutaondoa maana ya mashindano haya. Mtunzi mashairi Kandoro alisema, shuku zilileta vita, watu zikawagombanisha,...shuku nyingi jiepushe, nk. Kuwe na kamati za nidhamu, msiwauwe watoto wetu. Mlahabwa, UK

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 22, 2009

    I guess she's not only beautiful but intelligent too.Stand tall and keep your head high girl!you will achieve anything you want one way or the other.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 22, 2009

    annoy wa Tue Jul 21, 07:12:00 PM

    hiyo inaitwa jelous, lakni mzuri still si ameolewa hata aliachika, hiyo unayo jurge wewe ni personally ya mtu, still ameonekana mzuri ndio ameolewa kubali ama kataa, ikiwa kwa tabia, sura au vyenginevyo lakni ameolewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...