Watanzania waishio katika Jimbo la Gauteng (Johannesburg na Pretoria) wanatarajia kufanya mkutano wa kuanzisha jumuia yao tarehe 22 mwezi wa Agosti 2009 jijini Johannesburg. Mkutano huu utatoa fursa ya kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu jumuia hii pamoja na kuchagua viongozi wa kudumu.
Watanzania wanaoishi kwenye miji ya Johannesburg na Pretoria ambao wangependa kuwa wanachama na pia kushiriki kwenye uchaguzi wa uongozi wa jumuia wanakaribishwa kuwasiliana na wajumbe wafuatao kwa maelezo zaidi:
Brian Mshana b_mshana@yahoo.com
Laurean Rugambwa bwanakunu@gmail.com
Faustine Ndugulile drfaustinen@aol.com
Shukrani
KAMATI YA MAANDALIZI
KAMATI YA MAANDALIZI
wadau wa bonndeni
ReplyDeleteLabda sasa hivi inaweza kuwa jumuiya ya ukweli maana tumeshafanya hiyo mikutano mara nyingi,na tumeshachagua viongozi mara kadhaa ila mwisho hatujui huwa inaishia wapi.Nakumbuka mwaka 2005 baada ya kumaliza kusafirisha mwili wa MTANZANIA mwenzetu kuelekea nyumbani kukawa na kikao na tukaambiwa ianzishwe jumuiya tukaandikishwa majina na picha mbili kwa kila aliyejiandikisha ili BALOZI ajue idadi ya wanachama na tukalipishwa R50 kwa kila mwanachama,hiyo ada ni kwa ajili ya kujiunga na jumuiya na tukaambiwa kila mwisho wa mwezi tutakuwa tunachangia R50 kwa kila mwanachama cha ajabu tulifanya hivyo kwa muda wa miezi mitatu tu baada ya hapo ikawa longolongo na hadi sasa anapokufa MTANZANIA tunachangishana sisi wenyewe kwa wenyewe nikimaanisha hakuna chochote kinachohusiana na jumuiya na hata uende UBALOZINI kuomba mchango(chochote)kwa ajili ya msiba wa Mtanzania mwenzetu watakuambia hawawezi kutoa chochote sababu hawana idadi ya waTANZANIA wanaoishi hapa anzisheni jumuiya ili ubalozi uwatambue na uwasaidie,hii ndio hali halisi.
ReplyDeleteNi mimi MDAU
Johannesburg(Gauteng Province)