Kaka michuzi,
Habari za kazi na pole kwa majukumu. Naomba msaada kwenye tuta tafazali. Waosha vinywa tafazalini sana, hii si utani. ni REAL!
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27 mtanzania asilia ninatatizo kubwa ambalo ningependa wadau wenzangu wanisaidie kwa ushauri,nimekuwa sina bahati ya kupata mwanaume mwenye msimamo na mimi wote wamekuwa wakinitenda kila mara nakujikuta katika dimbwi la mawazo na huzuni nyingi.
Hivi sasa nninaishi denmark lakini bado ninahofu ya kupata mwenza yaani nimeingiwa na woga sana nahisi kama yatanirudia ya nyuma.
Ninaomba wadau kaka zangu na dada zangu mnishauri nifanyeje. Mie nimesoma, ni mzuri ila tatizo sina bahati na ninachohitaji ni mwanaume atakae ungana nami katika kujenga maisha yetu wote wawili.
Nitafurahi kupata ushauri utakao nitoa katika kiza hiki; maana nimeshaumia mno.
Mdau Marium

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2009

    dada kusema kweli,,,
    nimependezwa sana na wewe, na mimi pia ni singo,, mimi naishi hapa malekani kwa miaka mingi sana. nafanya kazi kule wostliti huko juu ya ny mjini katikati, na mimi pia sijaoa hata kidogo,,, ninataufta mchumba na mimi ila kwa hiyo kama unaweza tuwailiane ili tujuane vizuli emair yangu ni mashaka.john@yahoo.com
    mimi ni mpenzi mtalajiwa yohana mashaka wa wostliti. unaweza kuniandikia ili tujuane vizuli kwa sababu yule sasa nimebaki singo nakusubili ww tu.

    ReplyDelete
  2. Pole bi Marium kwa yaliyo kupata. Nafikiri umesahau ya kua ulitakiwa usile tunda kwanza kabla ya kua na uhakika wa ndoa, mwisho mungu akubariki upate kijana mcha mungu, bila kusahau ya kua ukipata mtu awe mtu anakuja kuchumbia na kuoa sio kukaa kinyumba "Boyfriend/Girlfriend" na ku "test" chungwa akiona chungu anakimbia. ops smahani.
    Mungu akulinge na kukuongoza, tubia na toba yako itapokelewa, omba maombi yako yatapokelewa, na uwe mvumilivu

    ReplyDelete
  3. NautiakasiJuly 01, 2009

    Nyama ale mwengine, mifupa utafute mtu wa kumpa...! Chenza limeliwa weeeeeeee, mpaka lishageuka belungi aka danzi ndo wajatafuta ushauri kwa michuzi... ha ha ha! Nani alokwambia ataka used tena la mchina?? Hatujui mtumiaji wa kwanza alitumia vipi? wengine hulazimisha kueweka laini mbili, wakati SIMU imetengenezwa kwa ajili ya laini moja...!

    Michuzi najuwa utabana hii lakini pouwa tu, ntafanyaje na ndo mawazo yangu yanavyonituma, siwezi ku comment kama yapendavyo mawazo yako!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2009

    Pole sana! Nakushauri urudi Bongo utafute kazi/ ufanye biashara. Wanaume Bongo wapo wengi. Ni vigumu sana kupata mchumba katika mazingira ya Ulaya! Tunakutana na waafrika kwenye matram na mabasi, wanaume wa kizungu ndo kabisa hayataki kuoa yanakunywa pombe tu! Usionyeshe sana kama unataka mme utakuwa pitio la kila mwanaume maana wanaume tunapenda loose ball, wenyewe wanasema Hit and run!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2009

    Dada nadhan kama umesahau kuwa Mwenyezi Mungu ndie mtoaji pia atakupatia kwa mda aliopanga yeye kama kakupangia kukupa kwani ushasema wewe ni mzuri na umesoma ila kumbuka kuna wengine hawajasoma ingawa walitaka ila hawakpangiwa,kuna wengine wabaya ila wameolewa kwa kuwa wamepangiwa.Endelea kumuomba Mungu kama kakupangia utakuja kupata tu,ila pia kila likuepukalo una kheri nalo dadangu usidhani kila mwenye kuweko kwenye uhusiano au ndoa basi anafurahia,yanayotokea huko ni siri ya aliyekuweko kwani wapo wanaotamani kuwa single kama wewe ila wanashindwa pia.Mh nisiongee sana isije topic kunigeukia bure watu wakaanza kupigwa mswaki hapa kisa mie.Wish you all the best

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2009

    Dada tatizo sio uzuri au kusoma. Linapokuja suala la kuoa tabia ya mtu ni muhimu kuliko sura au elimu. Tatizo dada zetu wa Ulaya mnataka usawa kila kitu, controlling!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2009

    ww mbuzi anony wa kwanza unayejiita jonh mashaka, hebu hacha kumkashifu mwenzio. kwa nini unacheza na jina la mwenzio hivyo kwani alikutuma umtafutie mtu. rudini kwenu ukichoka kubeba boxi ukafundishwe adabu bagalagashia kunguru weye, shika adabu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2009

    Just lower your std and try again. Mimi nina MS in Mechanical Engineering and my hubby is just a form four grad. Mweeeee hata viatu ananivua na jiko silijui mwaka wa pili sasa hahahahahah. Tuna watoto wawili na maisha yetu yana love and respect hujapata kuona.

    Before nilikua na date wasomi kama mimi nikaona wananiletea upuuzi tu. Wanaume wakibongo uwashinde kwa hela au ubongo watakulamba hata miguu lakini wakiwa wao ndio sole bread winner au wamesoma kuliko weeee watakunyayasa sana tu na kucheat juu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2009

    Pole sana na naamini kuwa hii ni ya ukweli kwani haina chenga japo kuwa kuna mambo huja yaweka bayana.Kumbuka kuwa ukweli uko pale pale kuwa bahati unayo.Lakini yawezekana kuwa na wewe ni mmoja ya machuna buzz.huku Ulaya buzz huwa halikai haswa haya meusi.
    jambo ambalo nahisi limekukumba ni kushindwa kufahamu kuwa jamaawa west Afrika kina a beg huwa hawana dogo.Na sisi wewe tu wamelizwa wenzako wengi tu.Napenda kukushauri kuwa kuwa na msimamo na ujuwe unataka nini itakusaidia sana.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2009

    Kwahiyo ndio kusema unataka mwanaume au mbona hujafanya request?
    Msaada ni jaribu kuwa mdadisi kabla hujatumbukia, What I see ni kwamba hufanya homework yako vyakuutosha unaparamia tuu!
    Mimi natafuta mke wa pili je uko tayari? mimi ni ustaadh na mujibu wa msahafu ruksa mpaka wanne.
    kama jibu ni yes ntakuandikia mimi naishi UK.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2009

    Miaka 27 hujachelewa bado. Kwani huko Denmark unafanya nini? Kama unasoma maliza shule rudi bongo upate mume. Kama unafanya kazi nenda likizo moja bongo ila ukifika home tulia utapata mtu bila shida.Ila kama una kazi angalia sana hao wanaotaka kula vya bwerere maana ukishatamka kua una kazi Den Mark vinyamkela kibao watajitia kukutaka ili mradi wakwee pipa waende wakaone huko majuu kulivyo halafu watakutenda pia. Good luck!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2009

    Kiswahili kingine kinatia mashaka kama mtafutaji!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2009

    Wewe Yohana Mashaka, unatafuta mchumba halafu unaandika broken maneno kibao unafikiri huo mchumba ambae amesoma atavutiwa na hayo? Ni kama kwenda kwenye interview halafu lugha hujui. Email unaandika emair,jamani!!Single unaandika singo!! Jaribu kuwa mtanashati wa kila kitu ndio utapata appointment.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2009

    We una mika 27 unasikitika kama mwanamke wa miaka 50 na zaidi ya yote unasema waosha vinywa wasikupe ukweli mh! Binafsi naona kama we waogopa vinywa may be hio ndo imekuwa sumu kubwa katika kupata mwenza.We relax sio wakutana na mtu tu wamshikia bango enhe utanioa lini?, msimamo wako nini? Ushauri wangu slow down acha kusononeka learn to be happy and love yourself single before you get involved with someone.And if your looking for love that hard may be it is time for you to sit and wait for love to find you.Shoga mara we mzuri una elimu hapo dada banaharibia wengi be nice if u want love.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 01, 2009

    MDAU HAPO JUU KAJITOKEZA INGAWA ANASHINDWA KUTOFAUTISHA RI NA LI.ANYWAY,WE CHA MUHIMU HAKIKISHA "UNYOBANI" NA MTU KABLA AKIJAELEWEKA KAMA MDAU HAPO JUU ALIVYOKUELEZA,ILO TATIZO LAKO LA KUOGOPA WANAUME LIACHE MARA MOJA SABABU UMRI UNAENDA HUO UNAWEZA UKAJUTIA,SIO WANAUME WOTE NI WAONGO WAPO AMBAO WAPO REAL NA SERIOUS ILA INATAKIWA UWE MAKINI KABLA UJAANZA "KUNYOBANA" NA MTU YOYOTE,HAYO YALIOKUSIBU NI WADADA WENGI WAMEYAPITIA SEMA HUWA AWAWEKI HADHARANI SABABU YA UOGA AU AIBU,JARIBU KUTUMIA AKILI SANA UKIWA UNAONGEA NA WANAUME VILEVILE USISAHAU KUSALI.HONGERA KWA KUWA MZURI THEN!!

    MDAU,TX.

    ReplyDelete
  16. dada ayo ndo mapito make kila mtu anayakwake.kuna wasichana wabaya na hawajasoma wameolewa na ndoa zao zinakwenda vizuri.Jambo ambalo mimi nakushauri kama kweli uko serious omba na mwenyezi Mungu atakufungulia milango ikiwa kama unajua kuwa mme/mke mwema utoka kwa bwana.La mwisho usikubali kutoa tunda kabla ya ndoa waliokwisha lila wanatosha,muwekee mme wako mtarajiwa.kila la kheri.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 01, 2009

    Wewe anony wa kwanza, ndio nini kufanya matani wakati mwenzio yuko serious na hili suala. Bi Marium nakushauri uwe mvumilivu ndugu yangu na umuombe saana manani kwani mume hutoka kwake. Mkasa uliosimulia huwakumba wasichana wengi siku hizi. Wanaume siku hizi ovyo sana, hawana mipango zaidi ya kudanganya dada zetu. Wewe jitunze vyema na Mungu atakuletea yule aliyekuchagulia siku aliyokuumba.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 01, 2009

    Oooh pole sana bi mariam, siku nyingine uweke picha ili watu tujue namna ya kushauri. Mimi mwenyewe sijaoa kama vipi tunaweza kuwasiliana alafu baada ya mda fulani kila mtu akiridhika na mwenzake twaweza kuoana napatikana kupitia. issamichuzi@gmail.com

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 01, 2009

    YAANI WEWE DADA WAZUNGU WOTE WA DANMARK UMEKOSA KWELI!!MIE NAKUSHAURI KUNUNUA MAGADI NA KUOGA NAYO!!POLE SANA

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 01, 2009

    Dada
    Nakushauri kama Kaka mtanzania mwenzako.Nia yako ilikuwa ni njema sana kwa yote uliyoyapitia na hao waliokupitia.Dada nakuomba usiwe na haraka,tulia.Be profesional and enjoy every moment in your life.Always keep smile in your face,maintain good relationship with those who surroud you,eat healthy and exercise.Remember marriage cannot be constructed by an overnight process.This is a lifetime contract which needs a total commitment and self surrender from both sides.Tulia dada,huwezi kuvuna kabla ya msimu wa mavuno.When the right time comes you will meet your husband according to God's plan.Kila mtu ana staili yake waache wanaotangulia watangulie na wala wasikusonaneshe.Tulia,Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 01, 2009

    Mdogo wangu mariam, kwanza nakupa pole kwa sononeko ulilonalo moyoni. Lakini napenda kukutoa hofu kuwa haupo peke yako, matatizo ya mahusiano yapo meengi sana, na i wish kama kila mwenye nayo angepata wasaa wa kuyaweka hapa kwa mchuzi, ingekuwa balaa. Anyway kwa issue yako ilivyo kwanza, inaonekana una stress about men, na pia una demand kubwa sana ya kupata mwanaume mwaminifu. Kimsingi, kwa hali uliyonayo sasa naweza kukushauri kwanza utulie, then make analysis ya kuona uhusiano uliowahi kuwa nao ulikuwa wa namna gani, na if was unpromissing what roles did you play. Wakati mwingine mahusiano huvunjika kwa sababu za pande zote mbili so make sure that hukuhusika kwa lolote kuwa na unpromissing relationship.

    Kitu kingine unapaswa kujua kwamba tuliumbwa na kwa imani we believe that God knows who is fit for whom and when, so what i see is probably kibinadamu tunaforce mambo mengi ambayo kwa Mungu bado wakati wake haujaatimia, so keep on praying and i belive one day, you will get a right person.

    Pia napenda kukushauri kuwa being without a men si tatizo kuubwa kiasi hicho, waweza kuendelea na maisha kama kawaida, isipokuwa roho na nafsi yako lazima ikubaliane na ukweli kwamba kwa sasa hutakuwa na mtu so let your heart relax, usiumie maana unaweza kuforce kupata mtu lakini baada ya muda mfupi ukaumizwa tena hata zaidi ya ilivyokuwa mara ya kwanza. Kisaikolojia inashauriwa kuwa upatapo tatizo hasa la kimahusiano, ni vizuri ukatulia, na kuchukua muda mrefu kiasi maana pia maumivu uliyoyapata si kidogo, bado yapo ndani ya nafsi yako.

    Mwisho: hapa utapata mawazo mengi, its you to choose which is which, lakini pia ukumbuke, wanaume wengi ni wa aina hiyo ya kutokuwa waaminifu lakini pia wapo wachache wenye utu na walio serious in relationship.

    Uwe makini usije ukaibuka na boya jingine ikawa balaa zaidi.

    Pole and get courage there is a day for you!

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2009

    pole dada marium, kumwomba Mungu ndo jawabu ,napenda kukushauri ebu niandike mail kwa email yangu hii gocmec@yahoo.com

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 01, 2009

    Mpendwa wangu pole sana, yani mimi nina tatizo kama lako ingawa kuna tofauti kidogo, nimesoma comment za watu humu kwa kweli na mi nimepata somo haswa, wengi wamekuwa waungwana mno kuchangia ingawa vichwa panzi hawakosekani hata bungeni kuna kura huwa zinaharibika. So turelax Mungu ipo siku atatunyoshea mkono, after row kuolewa sio lazima, wangapi wako kwenye ndoa wanalia kila kukicha, so kuwa mpole ipo siku mungu atakupa write person.

    ReplyDelete
  24. hii ni saikolojia tu.najua sana umri ndiyo unaoongea zaidi kwa sasa maana kwa vijana kilichombele ni kutazama mustakabali wa maisha ya mbele.fine; dada marium sioni kama hilo ni tatizo na naomba ujitahidi uweke hiyo hali kama ni maisha tu....fanya kazi,saka hela, jenga future, mme yupo tu.pia mwana sikia, akili inahiusika sana katika malovee, ndoa yataka upendo na kuendana basi. nadhani haujapata mtu wa kuendana nae mpaka sasa...na hilo hauwezi kuforce hata kidogo pia wakati mwingine marafiki mkijitambua mnaweza weka sawa na mkawa mna match safi. so, tulia fanya mambo yako....swali;unaweza olewa na kijana uliyemzidi miaka mitatu??? nataka uone jinsi hata wewe unaweza pata wakati mgumu. poa 4more comments and chats, am available lambertmbeye@gmail.com, tanzania, 24yrs,working. tchao!!!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 01, 2009

    Yani wanaume wengi wao ni matapeli, alafu hakuna tofauti aliyesoma na ambae hajasoma wote akili zao sawa tu, mimi nimepata pigo miezi mi3 iliyopija jitu limenipotezea muda miaka 7, alafu anakuambia its over, kanitumia weeeee ila Mungu yupo sisoneneki sana kwa sababu naami kila kitu hupangwa na mungu, pole sana karibu kwenye chama cha usingle just relax, yani ona kama vile wanaume wote wana virusi nakuambia wala hutatamani mwanaume.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 01, 2009

    Mimi nakushangaa Marium,
    wewe bado mtooto,lakini umeshaona tayali umekosa bahati!! acha mungu asije akapoteza bahati zako kabisaa,kwani kama unawashwa? haufii na inamaanisha umzima,,sasa wewe tuliya kichwa kiwe namawazo yakuplani maisha tu,hivi unajua kama unaweza kupata huyo mwanaume na ukawa namatatizo zaidi yahayo?tena ujue kwamba wanaume wahapa ulaya ni dun sana wengi hawaowi ni umalaya tuu.sasa ukiendekeza eti mwanaume mpaka utaishia juu juu,sio kama bongo unajipodoa tu tayali mwanaume unamkuta amekusubili njiani,,tena hayo yoote kitu muhimu ni kumuomba mungu,,kasababu mume mwema na mke mwema hutoka kwa mungu,,na aliye kupa uwezo wakusoma ukawa na elimu mpaka ukafika ulaya! atakupa hicho unachohitaji,unajua wasomi waliohangaika kutafuta jinsi yakufika au kuishi ulaya mpaka sasa walishindwa?ila wewe unadunda tu hapo Denmark,,yote maisha dada.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 01, 2009

    marium uzuri wa mwanamke sio sura nii tabiaaa .WASICHANA WAKIBONGO HAPO NDO MNACHEMKA UTAMSIKIA DEMU OH MI MZURI ,NATONGOZWA NA WANAUME WENGI TU .SASA JIULIZE KWA NINI HAO WOTE WANAOKUTONGOZA NA UZURI WAKO HAMNA ANAYETAKA KUKUWEKA DANI KAMA MKE.MNABOA KWA MISIFA ISIYO NA MAANA.HOVYOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 01, 2009

    We dada inaonekana huko Denmark unajiuza na hakiya mungu ukikaa huko huolewi NGOO wazungu wamekuchoka nakushauri rudi nyumbani unaweza kupata mume.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 01, 2009

    Salaam dada Marium,
    kwanza jaribu kuangalia Ibada yako(ikiwa wewe ni Muisilamu) chunga salah zako kwa wakati.Pia kabla hamjapatana na huyo mchumba kuoana muomba mola fanya na mola wako mshawara(Istikhara) akupe maono bora juu ya suala hili la ndoa uliendealo.
    Kuna suala la kijicho , mashetani na ulozi .Jaribu kuwa unasoma sana Quraan hususan Surat Baqara , Yasin , Ad-Dukhan , Safat na ayah za kinga kama vile Ayat Kursiyu.Pia fanya kusikiliza kama hutoweza kusoma.Unaweza ukapata magwiji wa tiba za Kissunah hapa nyumbani wakakutibu.Kumbuka sio pekee yako(ikiwa hii usemayo hapa ni kweli) wapo wengi kama wewe waliofuata ushauri huu na wakafanikiwa.
    Ndugu yako
    Mdanzi

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 01, 2009

    Wewe unalalamika miaka 27? Mbona bado upo upo ingekuwa 35 hapo ndio. Tena kumbe unaelimu ya kutosha, unauwezo wa kufanya kazi ukakidhi mahitaji yako then unalalamika Why? Sifa ya mwanamke ni kufanya kazi sasahivi, kutokuwa golikipa. Wewe aminiutajampata tuu wako usikate tamaa wanaume ndivyo walivyo wapo wastaarabu na wapo wachafuzi. Ila jitulize, heshima ndio muhimu uzuri wa mwanamke si sura bali tabia. Ukitulia utajapata tuu atakayekata kiu yako.

    Lakini tungependa kujua Je wewe unahitaji watu wa aina gani?

    Sababu usijekuwa unataka tuu wale wenyepesaaa hayo ndiyo madhara utadanganywa hadi ukome. Maskini / wa hali ya kawaida wapo kibao wanaohitaji kuoa bora tuu uwakubali then umpe mtaji au umtafutie kazi musaidiane katika maisha. Nahakika huyo atakupenda sana.

    Pia usiforce sana kuolewa pengine Mwenyezi Mungu bado hajakupangia. Mtegemee Mungu atakupa umpendaye na akupendaye. Atakuja tuu siku moja kesha ukiomba.

    POLE SANA.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 01, 2009

    Marium, wachumba wapo ila ukiwa ulaya kupata mmbongo kazi sana kila mtu huko amekuja kutega mitego,hivyo njoo bongo, mimi pia nipo nataka mke wakuoa ila awe muadilifu. Ulaya kulishanishinda huko.Jielezee vizuri watu wakujue unaweza ukapata mume mwema. niite jj

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 01, 2009

    Marium, usife moyo kabisaaa, we bado mdogo na umri si kigezo. Yupo tu mtu mzuri Mungu hajamuelekeza kwako. Mimi nina miaka 45, watoto 3 Nimeishi na lijamaa maisha ya upendo kwa miaka 18. Aliamua hiyo siku moja kutuacha mimi na watoto bila ugomvi wala nini mpaka leo ni miaka 5 tunapishana tu mitaani. Namshukuru Mungu nina kazi nzuri na maisha si mabaya kwani naendelea na watoto wanasoma vizuri. Sasa ungekuwa wewe si ungechanganyikiwa? Some men can really screw your life!

    Life is Good and please Thank God for everything cos he knows what's best for you. Don't waste it crying for men!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 01, 2009

    Hebu tupe dondoo kidogo. Je mwanaume wako unataka awe vipi? Sifa zipi?
    Kazi:
    Elimu:
    Mnene/mwembamba
    Rangi:
    Dini:

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 01, 2009

    ...umenisikitisha sana dada...

    pole kwanza afu jua hauko pekee,yani wengi tu tumepitia uko dada ila km wavosema annons apo juu,jipe moyo mkuu,chapa kazi,soma tu,tafuta good life,treat urself well well,yan kwa ufupi enjoy

    usiwaze weeee kiivo mwisho uingie ndoani ndoano-yan upate sklepa la kufa mtu ukajutia ndoa iyo maishani

    pili,usilale-lale ovyo na iyo mijitu JAMANI,just control urself dada,weengi mijanaume inayokutaka kukulala jua basi uyo ataka kukupitia tu,wachache saaana atakuoa later

    mume utapata tu,27 yrs mbona mdogo ivo?sie wa 32yrs tusemeje??

    SUBIRI USIWE NA PUPA,UTAINGIA CHAKA

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 02, 2009

    Pole miss marium sali kwa raha zako zote enjoy life when you still young do not be unhappy.''life is short, and it is up to you to make it sweet.''Maisha hayana gurantee,nowadays is better off to be single,cause all men are catastrophic of life.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 03, 2009

    Mariam nilisha toa comment yangu ila i was thinking about your story today and I thought i should tell you this.This is from your love story above; Since you have been hurt with men you cared about you should start dating the traditional way.Usishobokee kulala na mwanaumme wakati mnaanza kudate ukadhani ndo atakaa kwenye mahusiano.Kuwa na mtu hata ikiwezekana miezi mitatu bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi, I promise you,you will learn lots about this person and then you will be able to decide wether you should invest you emotions on this person.I have tried it myself and it has served me a great deal from heart aches.
    Start with someone as friend though you have feelings for them,then slowly take things to the next level if it is working after three months.I wish you read this book Think like a man, Act like a lady by Steve Harvey.Search it from the book stores.You will learn a lot from this book.I have a lot i want to tel you but would prefer to do it in private.Indicate here if you want more contact by dropping your email on the comments page.
    I wish you well.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 03, 2009

    UNAJUWA MAISHA NI MAFUPI SANA, WATU HAWAJUWI, MUDA SI MREFU TUTAKUWA WAZEE NA KUACHA DUNIA HII, USIMTENDEE MTU KITU USICHOTAKA WEWE KUTENDEWA, THINK OF OTHER PEOPLES' NEEDS BEFORE YOURS. WEWE DADA WALA HUSITAHILI HAYA YOTE ULIYOTENDEWA, IPO SIKU MAMBO YAKO YATAKUWA SAWA. NINASALI NAKUOMBEA NA MUNGU ATASIKIA KILIO CHAKO.

    MIMI EDWARD

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...