Mgeni wa heshima Naibu Balozi wa Tanzania katika nchi za Skandinavia Mh. Jacob Msekwa akimkabidhi kombe nahodha wa kilimanjaro Kabrao
habari za saa hizi bwana michuzi. mimi bwana ni mmojawapo wa viongozi wa kilimanjaro na asante sana kwa kutoa taarifa ya mechi baina yetu Kilimanjaro FC ya Tampere na FC Bongo ya Helsinki ambapo tuliwachapa 8-1. Ila naona picha tumebaniwa kidogo. Kwa hiyo nakutumia hizi uzirushe kwenye globu yetu ya jamii ili jamaa wa nanihii waipate freshi....wangeshinda wao naona globu yote wangeinunua hahahaaa..! Yaani kama namuona Ezza alivyonuna. Ndio ukubwa huo kaka. Nasikia kazi yako ya ukocha imeota mbawa. Na bado...
kikosi cha kilimanjaro FC ambacho kiliwachakaza FC Bongo kwa mabao 8-1. Na kinasadikika kwamba ni kikosi bora cha watanzania wote wanaoishi ughaibuni.
Kikosi cha FC Bongo ambacho kilisambalatishwa vibaya sana na bila huruma na wana Kili FC.
Picha ya pamoja ya kilimanjaro FC wakiwa pamoja na mgeni rasmi kutoka ubalozi wa Tanzania katika nchi za skandinavia Mh. Jacob Msekwa



Huyu alietoa habari hizi kwa michuzi wala hajatoka kilimanjaro, kama angekuwa ametoka kilimanjaro asingesema kuwa wanatoka norway, huyu ni mshabiki wa TAS tampere na tunamkumbuka alipopiga picha hii.
ReplyDeleteMichuzi usiibanie hii komenti kwani jamaa kaongopa hapo wazi.
Mjomba Kablau tuwasiliane kwa e-mail godi80@hotmail.com
ReplyDeleteGodi-Bogota
kiongozi wa timu ujui uko nchi gani? wizi mtupu ati norway. mdau helsinki
ReplyDeleteWabongo kuleni dagaa za kigoma tuu.zenu nikubamizwa tuuu
ReplyDeleteHicho kikosi cha Kili kinatisha. Watu wa Norway, Denmark, Holland, Germany na kwingineko mpo? Njooni nanyie mpigwe.
ReplyDeleteMdau Stockholm
Hawa tampere wantapatapa kwani wanajua kiama kinawasubiri jumamosi hii vumbi stadium.
ReplyDeleteJameel nakuona hapo pamoja na baby. Salaam.
ReplyDeletema' mdogo
dar es salaam
Imesemwa mara nyingi rangi ya jezi inaweza kukuharibia watu wakawa wanabisha. Si mnaona wenyewe.
ReplyDeleteFC Bongo, Jumamosi sio mbali.. subirini kichapo kingine toka kwa TAS!
ReplyDeleteKILI FC LAZIMA WASHINDE, HAMUONI KAMA KUNA WACHEZAJI WA YANGA NA SIMBA NDANI YAKE? NAMUONA MACHUPA HAPO, CREDO MWAIPOPO ALIYEKUWA YANGA NA WADAU FLAN FLAN WANAOJUA KUKIPUTA...HAWA SAIZI YAO TIMU YA VODACOM, JAMANI TUNAOMBA MSAFIRI MJE BONGO HUKU, ACHENI KUONEA WENGINE...NJOONI MPIME UBAVU BONGO NA TIMU KAMA YENU SIO LAZIMA SIMBA AU YANGA AU AZAM, KUNA VODAOM, ZAIN,STANCHART, TIGO ETC...NJOONI KUDADADEKI NA MAJESHI YENU HAYO.
ReplyDeleteHUKU NI KICHAPO TU, HUMPHREY ANATUTAMBUA...MUULIZENI.
Jumaa habari za miaka mshikaji wangu tumepoteana naona umetulia nyuma hapo wewe ndiye coach nini...??? tuwasiliane bwana
ReplyDeleteBob
nilishauliza
ReplyDeleteivi ao watu wana rangi-rangi wa nchi gani??au wazenji?au chotara wa kibongo
mana naona sii kawaida
afu kuvaa "jezi" ambazo bongo ni vazi la watanzania wanaposhangilia timu ya taifa!!!!....!!!
Mbona watu wengine wana maswali yaajabu kwani watanzania wote weusi??? Tanzania ni taifa lenye mchanganyiko wa watu wengi iwe waarabu,wahindi,weusi,machotara,wangazija n.k Acha ubaguziiiiii......Hao warangi rangi pia watanzania na wanatambulisha tanzania ndio maaana wanacheza kwenye timu ya tanzania so simple.....
ReplyDeleteNyie FC Bongo msitapetape oh wana wachezaji kutoka yanga simba nk.
ReplyDeletekilimanjaro inatisha sana. na yule mtoto aliyewafunga bao la kwanza jee anatoka wapi Si Simba wala yanga na wengineo tu ambao wanasakata kandada kiukweli sio piga ni kupige na kuhusu rangi huku Skandinavia ni baridi hata wewe ukija utaiva tu. ha ha ha
Mdau Stockholm
kilimanjaro Club inatisha baadhi ya wachezaji ni Kipa Cabrao zamani kacheza Bandari Mtwara,Machupa kacheza Simba na Taifa Stars,William John kacheza Simba, Shekhan Rashid kacheza Simba, Bwana mdogo Richard(Messi) keshaitwa Barcelona kwenye trial. Huyu bwana mdogo ni nuksi hasa akiwa na boli anaweza kumfaa sana Maximo.
ReplyDelete