Mkuu wa wilaya ya nanihiii,

NAOMBA KAZI YA UKUU WA WILAYA - TARIME

Baada ya kufanya kazi ya kubeba maboksi hapa marekani kwa karibu ya miaka kumi, nimeamua kustaafu ili nirudi nyumbani. Ninataka kurudi kule nyumbani nilikozaliwa. Ninataka kurudi nyumbani nilikofundishwa kuandika, hesabu, na kusoma a - e - i -o - u na mwl Nyansambo.

Nimesoma kwenye vyombo vya habari kuwa serikali inataka kuanzisha utawala wa kijeshi nyumbani kwetu (Tarime) ili kukomesha mapigano yasiyoisha. Hali ambayo inaelekea kubadili mawazo yangu ya awali ya kustaafu ubeba bokisi na kurudi nyumbani ili kufanya kazi ya kuchunga ng'ombe. Hali hii badala ya kunikatisha tamaa, imenitia hamasa ya kuharakisha mpango huu wa kwenda nyumbani na kujaribu kusaidia.

Kabla ya kujaribu jeshi, naomba serikali ijaribu uongozi wa kiraia kwa mara nyingine tena ili kujaribu kutatua tatizo hili. Mazungumzo yenye nia ya kuleta mwelewano yakiwa na msukumo/nguvu ya serikali, vinaweza kusaidia na kulipatia ufumbuzi tatizo hili.

Kwa vile sina ndugu yoyote serikalini ninayeweza kumuomba anipigie debe kwa wakuu huko Magogoni, Na kwa vile nina imani kubwa sana na hii bulogu ya jamii - kama miongoni mwa vyanzo muhimu sana vya habari Tanzania;

Ninaomba kutumia bulogu yako hii kuomba kazi ya ukuu wa wilaya ya Tarime. Naomba mheshimiwa Kikwete (najua kuwa yeye au wasaidizi wake wanasoma hii bulogu yetu) au waziri mkuu anijaribu mimi kwa kazi hii. Nitakubali kupewa muda wa kutimiza kazi yangu na niko tayari kufukuzwa kazi au kujiuzulu kma nitashindwa kufikia malengo yaliyotimizwa kwa muda uliopangwa.

Kama wakuu wanakubaliana na hili, naomba uwapatie email yangu kwa ajili ya mawasiliano. Nakuruhusu utoe email yangu kwa atakayeitaka ila tafadhali sana usiiambatanishe na bandiko hili. Ninajipa moyo kuwa nitaifanya kazi ya kuiendeleza Tarime kwa moyo wote.

Wako mbeba boksi aliye njiani kustaafu,

Magabe Kibiti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2009

    daa hii kali...
    kila la kheri kaka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2009

    oh plizzzz.... naona kweli tumechoka...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2009

    Magabe Magabe Magabe mura wetu acha usanii. Yaani wewe uache kazi marekani ili uende Tarime kuwa mkuu wa wilaya.

    Yaani angalau ungesema kuwa unataka kazi Dar au Mwanza au pale wizara ya fedha ningekuelewa. Kwa kweli sitaamini mpaka nitakapoona ukiapishwa.

    Ha ha ha, labda unajua kuwa hakuna atakayekupa kazi hii na ndio maana unaweka hili tangazo hapa.

    ReplyDelete
  4. Kweli bongo tambarareeezzz!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2009

    Magabe,
    Mang'ana gasarikire mura, nami nipo nyuma yako, hili box la hapa UPS ya Broadway Street nami nimeckoka nalo. Nipo njia moja.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2009

    Anon wa 08.58pm kwani ni ajabu kuacha kazi USA na kurudi nyumbani kufanya kazi? Mbona wengi tu wanafanya kazi mikoa/wilaya mbalimbali sasa na walisha wahi kuishi nje ya nchi? Nyumbani ni nyumbani. Wenye mawazo kama ya mdau tupo wengi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2009

    Mura Kibiti, amang'ana gao thatho? gya nsiku? Genda umothebi e jiniasi Joni Mashaka Mugende yieka. Omuroyo amanyire amaru. wote muende mukakutane na porisi wa Tharime abetheme rirungu ryao.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2009

    Hawa tunaowa-recycle ndio hivyo tunaona mzigo umewaelemea. JK mjaribu mbeba maboski huyu. Hawezi kuharibu zaidi ya palivyoharibika sasa hivi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 13, 2009

    Nitakuunga Mkono Kaka yangu, japo tumesahauliana kabisa, uliwahi kuwa tuitor wangu wa nguvu mlimani.... please write to aldegunda.ngowi@britishcouncil.or.tz. Poa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 13, 2009

    Kibiti, Honestly speaking
    You have great idea, I support your vision 105%.
    Kama serikali wafikiria kupeleka utawala wa kijeshi Tarime, huo utawala uanzie Dar Es Salaam, Huwezi kupeleka mikono hospitali halafu ukaambia miguu nyie nendeni kazini.
    I mean lazima tuwajibike pamoja, Mkuu wa Wilaya hakuwajibika, manake Mkuu wa Mkoa hakuwajibika, Waziri wa S/Mitaa naye hakuwajibika. Ukifuata huo mlolongo utagungua, wote kwenye msuru huo ni failure.
    Kwanza Mwema amwondoe Masawe haraka sana Tarime. Pinda amwondoe Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa mkoa ashikilie nafasi ya Mkuu wa Wilaya kwa muda,yaani awe na kofia mbili, kwanini!! anauwezo wa kucommand more respect, halafu akihitaji msaada kutoka wilaya zingine ni rahisi kupata, ana uwezo wa kumfanya Mkuu wa Rorya awajibike ipaswavyo upande wake.
    Watendaji watawajibika kwasababu wanajua anaweza kuaachisha kazi including MKuregenzi/Halmashauri. Ana mawasiliano ya karibu sana na Ikulu na vyombo vya usalama kuliko Mkuu wa Wilaya, anaweza kumptatia PM habari za Tarime akaziamini kuliko mkuu wa Wilaya.
    Atakuwa anawafanyia rotation wakuu wengine kwenda Tarime kwa nyakati tofauti ili kusiwepo na mazoea katika kazi na watendaji wasijue kesho wako na nai bali ni kufanya bila kujali nani bosi leo au kesho

    Kazi umepata, ila unahitaji makamanda, ukipata Ukuu wa wilaya, nina leseni hapa Mexico ya kuendesha lamo,nitakuwa dereva wako

    Mexican Blogger

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 13, 2009

    Ni magabe huyuhuyu aliyetuacha njiapanda pale chuo kikuu Mlimani ile miaka ya new millenium?kama ndiye labda anaweza akarudisha enzi za akina DC Pascal Mabiti

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 13, 2009

    Ndiye magabe huyu huyu wa enzi za akina Rais wa DARUSO, John K na makamu wake Emile Kivugo!! Namfagilia kwa Solidarity Together mlimani!!!!! 1999/2000.Ri gwaride analiweza mura huyuuu! we acha tuu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 13, 2009

    una akili sana mdau

    jamani km ikulu inasikia wamwite uyu jamaa,me sioni utawala wa KIJESHI ndo suluhisho,yan mwataka sema tarime imeshindwa tawaliwa?mbona mnatutisha,na mnaleta mambo ya zaire umu?

    ebu wajibisheni viongozi pale na wekeni utawala wa kiraia,hii nchi sio ya kijeshi/mabavu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 13, 2009

    Magabe ametumia hekima kufikisha ujumbe wake, wenye kuelewa wataelewa, haieleweki akilini watendaji wawepo washindwe kazi mpaka eneo litawaliwe kijeshi? Basi hata nchi itawaliwe kijeshi!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 13, 2009

    wewe anon wa 8:45am, mliachwa njia panda na nani? Mimi nilikuwepo mlimani miaka hiyo ila sisi wanafunzi ndio tulimuacha Magabe na wenzake solemba pale tuliporudi na kuendelea na masomo huku tukimuacha Magabe na wenzake wakisota rumande.

    Ama kweli watanzania kwa kugeuza mambo siwawezi. Mura Magabe, we baki huko huko Marekani. Hapa bongo hutaweza longolongo za waosha vinywa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 15, 2009

    magabe mura! usipoteze muda wako kwa watu walioshindikana you cant change them unafikiri wewe na marekani yako ndio watakusikia nyumbani ni kuzuri lakini rushwa ,rongorongo na ukichaa umekithiri mtu aliyetoka nje ni kama unapigia mbuzi gitaa anyone ambaye anajaribu kuchange system anaoondolewa before hajajijua so be careful hiyo ni bongo mzee nenda pole pole wako wapi waliotangulia??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...