
hivi ndivyo teksi za dar zinavyoonekana sasa ambapo kila wilaya ina rangi yake. wilaya ya ilala ni kijani, kinondoni ni njano na temeke buluu. hii ni katika kurahisisha utambuzi wa magari haya. picha hii imepigwa kona ya mtaa wa mkwepu na samora avenue zamani maarufu kama salamander ambayo jengo lake limeshapigwa nyundo.
Michuzi km sikosei hizo zilikuwa zimebadilishwa kuwa mikoa au zilirudishwa kuwa wilay tena? Anyway inawezekana maana Tz management sometimes inafikiri backwards.
ReplyDeletehiyo system nimeipenda maana ata huku europe taxi zote zina rangi maalum ili kurahisisha utambuzi wa magari hayo ila kwa mabitozi wa bongo wanaotesa kwa kukodi taxi na kufanya magari yao sasa wameumbuka
ReplyDeletenaona ilala na kinondoni ni YANGA tupu....
ReplyDeleteNa wale Mabitoz wenzangu tunaonunua corolla kwa multi purpose.yaani ku kutanulia na kuiweka kijiweni ilete hesabu.tumeumbuka..Huu mstari noma kweli.hatuendi tena kwa watoto wa getini.hata ukibadili kibao cheupe to njano bado mstari unaumbua
ReplyDeleteHivi hii mistari anapiga mtu binafsi mmiliki mwenyewe au ni dili la VETA?aU NDO MAMBO YA MKANDARASI ALIYESHINDA ZABUNI?
ReplyDeletekwa sisi mabitozi mhh kwa kweli Noma lakini ninampango wa kuagiza Magnetiki stiker yenye rangi hizi ukiwa kiwanya unazitoa tu nipo ktk risachi suuni i wili kam beki from ze taxii owner driver
ReplyDeletemweeeeeee
ReplyDeleteila bei ya tax bongo dar balaa
bora upigane na daladala tu