Kwa Watanzania wote na marafiki zetu,

Kamati ya chama cha kirafiki kati ya Finland na Tanzania inayo heshima kubwa kuwakaribisha Watanzania / Wafini wote pamoja na familia na marafiki zao kwenye pikniki itakayofanyika tarehe 26/07/2009 kuanzia saa 6.00 (sita) mchana, katika kisiwa cha Iso Vasikkasaari.

Maelezo ya jinsi ya kufika sehemu ya pikniki Iso Vasikkasaari unaweza kuyapata hapa:
http://www.espoo.fi/default.asp?path=1;28;11866;15440;16054;16056

Sehemu nzuri ya kuondokea ni kutoka Nokkala, Matinkylä Nokkalanpuistontie ambako boti inaondoka kwa ratiba ifuatayo:
Nokkala - Iso Vasikkasaari: 10.30, 11.45, 12.30, 13.45, 14.30, 15.45, 16.30, 17.45, 18.30

Kutoka kisiwani boti litaondoka kwa ratiba ifuatayo:
Iso Vasikkasaari - Nokkala: 12.00, 13.15, 14.00, 15.15, 16.00, 17.15, 18.00, 19.15, 20.00

Gharama ya tiketi ya usafiri wa kwenda na kurudi kutoka kisiwani ni Euro 4, bure kwa watoto wote chini ya miaka 7.

Jitokezeni kwa wingi katika siku hii muhimu ili tupate kufahamiana na kujumuika pamoja kama familia.

Tafadhali kamati itashukuru kama utamjulisha yeyote ambaye hajapata taarifa hii.

Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga namba:
040 7333397 / 040 5892123

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    Kama ulikuwepo kwenye mawazo yetu. Hii siku tumeisubiria kwa muda mrefu, tunakushukuru sana DC wa nanii kwa kutuhabarisha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    Haya ndio mambo tunayotaka kuyaona, sio longo longo nyingii, vitendo hakuna. Big up kwa waandaji.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2009

    Vijana wa Helsinki tuwakilisheni kwenye pikniki, mdau nipo kwenye vakesheni, nikiwahi lazima tutaonana hiyo J2.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...