Japhet Kaseba akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uwezo wake katika mchezo wa boxing pamoja na kwamba ni Bingwa wa Kickboxing na ana uwezo mkubwa wa kucheza mchezo huo kushoto ni rais wa shirikisho la ngumi za kulipwa tanzania PST Emanuel Mlundwa.

Rais wa Shirikisho la ngumi la PST Tanzania Emmanuel Mlundwa akitambulisha rasmi pambano la Ubingwa wa dunia wa Middle Weght wa International Circuit Boxing (ICB) baina ya bingwa mtetezi Francis Cheka kutoka Morogoro na Bingwa wa dunia wa Mchezo wa Kickboxing Japhet Kaseba pichani kulia.

Mpambanao huo hautakuwa wa kickboxing ila litakuwa ni la Boxing na litakuwa la Round 12 za dakika tatu kila moja.


Mlundwa amesema pambano hili limeidhinishwa na shirikisho la masumbwi la Dunia ICB na na shirikisho la ngumi la Tanzania PST pambano hilo liatachezwa tarehe 3 mwezi ujao kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar.


Naye Japhet Kaseba amesema amejiandaa kuonyesha upinzani kwa mpinzani wake Francis Cheka ukizingatia kuwa ni bondia mzuri, ameongeza kuwa kabla ya kuhamia kwenye mchezo wa Kickboxing alishawahi kucheza mapambano kama nane hivi ya Boxing na akashinda yote hivyo anazielewa vizuri sheria za Boxing na atacheza kwa uwezo wake na mbinu mmbadala ili kumtwanga mpinzani wake Francis Cheka.

Bondia Francis Cheka (mwenye mikanda na mikono juu) akiwa na maafisa wa chama cha Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST) wakiwemo rais wake Emmanuel Mlundwa (tatu kulia), na maafisa Bakari Selemani (shoto) na Anthony Rutta (pili shoto) pamoja na kocha wa Cheka (kulia) mara baada ya kuongelea mpambano kati ya Cheka ambaye ni bingwa wa ndondi na Kaseba, bingwa wa Kick Boxing.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    Wish you all the best Japhet Kaseba.

    Robert.
    Your friend/neighbour

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    Du! Mzee kama umeshindwa mapambano yote nane, sasa hilo la tisa utashinda kweli? au umegundua sehemu ya kupata nguvu za giza? Mi naona ni bora ungeendelea na kickBoxing maana hilo Cheka lenyewe linaonekana na Usongo wa kupiga mtu..!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2009

    Mdau hapo juu si kuwa kaseba kashindwa mapambano nane isipokuwa kashinda mapambano hayo nane.soma tena hiyo taarifa utaelewa.
    Ila mimi ninamtahadharisha bwana japhet,kuwa bondia francis cheka hana mchezo na mtu, hivyo kama kweli anataka kushinda ni lazima ajiandae kwelikweli.
    Kuna vigogo vya ngumi hapa nchini vilijalibu kupigana naye, wakaangukia pua.
    Hongera kwa kuamua nakutakia maandalizi mema.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2009

    Naomba kumtahadharisha Ndg. yetu Kaseba kuwa asije akachanganya MADESA ya kickboxing na BOXING. Nijuavyo mimi, mchezo wa boxing ukikolezewa mchezaji huchanganyikiwa vilivyo. Tafadhali usije ukajutia uamuzi wako kwa sababu kama binadamu wengine unahitaji MSHIKO kwa ajili ya mkate wako wa kila siku. OTHERWISE tunatarajia kushuhudia mpambano mzuri wa kiwango cha hali ya juu. Nawatakia maandalizi mema.

    ReplyDelete
  5. Aisee mie wananitega cos mie ni fun wa kasema kwenye kick boxing na upande wa ndonga na mzimia Cheka ukizingatia ni home Boy anawakilisha Morogoro....HAYA TUTAENDA KUWA WACHANGIZI...ILA WANATUTEGA WAPENZI WAO

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2009

    Yaani miaka imepita kweli,Emmanuel Mlundwa ameanza kuzeeka.Enzi zetu yeye ndie alikuwa anatamba na ma-olympics.Nice guy, always humble.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2009

    mbona misuli hatuioni?

    ReplyDelete
  8. Waosha vinywa naomba mnielekeze huo uwanja wa uhuru ulipo mie sipajui japo ni mzaliwa wa DSM.
    Ili tarehe tatu nikashuhudie mpambano.hatujaambiwa unaanza sh ngp na kiingilio ni sh ngapi

    Pia ningeomba serikali itupie macho huu mchezo utatujengea heshima na kututambulisha kimataifa

    Alaf pia itawezesha mambondia na wasimamizi
    maana nikiwaangalia hapa hao wadau wamechoka kweli,kwa hali hiyo wakikabithiwa chochote kitafika kweli kwa walengwa.Wizara husika sidhani kama imewajibika kwenye mchezo huo effectvly

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2009

    Kwanza kabisa napenda kumshauri mdau aliyechangia hii mada kama mchangiaji wa pili kwamba awe anasoma maelezo vizuri, sio kuperuzi peruzi tu juu kwa juu kama vile unatafuta habari ya kuisifia Yanga kwenye magazeti.

    Mdau wangu hapa mwingine yeye hajui uwanja wa uhuru ulipo, mdau huo uwanja ni ule wa taifa wa zamani, yani shamba la bibi.

    Kwaheri.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2009

    Mbese Hongera naona umejikita kwenye ndondi sasa. Mafanikio mema.
    -Mimi mwana Gojuruu mwenzako enzi hizo pale Zanaki safarini ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...