Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Yona Killagane wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliopo Ubungo jijini Dar
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (wa pili kulia) akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Ethur Mwakapugi na kushoto kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.


Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiweka gesi katika gari wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama nyuma ya waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.


Mfanyakazi wa PanAfrican Energy (T) LTD akimuonyesha Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) jinsi ya kuweka gesi katika gari maalum wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika leo huko Ubungo jijini Dar es Salaam. Aliyesimama kulia kwa waziri ni Meneja Mkuu wa PanAfrican Energy (T) Ltd Pierre Raillard.








Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akimsikiliza mkazi wa Ubungo Maziwa kuhusiana na maombi yao ya kulipwa fidia ili waweze kahama eneo hilo na kupisha ujenzi wa mitambo kupeleka gesi majumbani, kwenye taasisi na kwenye magari. Waziri Ngeleja alifika katika eneo hilo leo kwa ajili ya uzinduzi wa mtambo wa kushindilia gesi asili uliofanyika. Picha na An na Nkinda wa Maelezo






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2009

    Michu hivi hiyo PanAfrican Gas imetokea wapi? Maana nilipoenda kule Twiga cement wakati Rais anazindua mitambo mipya nikakuta hao jamaa wanahusika na gesi inayotumika tanuru mpya, na pia Songas wanahusika na gesi kwenye tanuru za zamani. Sasa ndio kusema PAG wao wametokea wapi maana hata jamaa wa kule twiga walishindwa kunijibu maana wanasema hata ikitokea jamaa wamechemsha kutatua tatizo huwaita Songas kurekebisha, inakuaje hiyo au ndio yaleyale?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2009

    PAE ndio Songas au? Tungane bwana Michu maana yaonekana ulikuwapo hapo ukasikia utambulisho.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2009

    Ngeleja alikuwa yanki handsome sasa naona siasa zinamzeesha

    ReplyDelete
  4. Inafurahisha na ni hatua nzuri tumefika.
    1. wananchi kuja na mabango na kuruhusiwa kuwa nayo kwenye ziara ya waziri bila virungu vya FFU
    2. Waziri kuwasikiliza wananchi wenye malalamiko (Sijui kama atafanyia kazi)
    3. Wananchi kutotumia fujo kupeleka malalamiko yao kwa Mh. Minister

    Kupishana Imani, Ideology, Mitazamo sio uadui, wapinzani na watawala wote ni watanzania, wananchi na watawaliwa wote ni watz, waislam/wakristo.wapagani sote tu ndugu, Tubishane Tukiamini sisi sote ni wamoja, Watanzania tuna haki sawa ya kuongoza, kuongozwa, kupata sehemu ya pato la taifa

    MUNGU IBARIKI BONGO

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2009

    Nijiavyo mimi PAE ndo wenye visima vya gesi songosongo. wanauza gesi kwa songas, na makampuni mengine kama tbl, twiga serngeti nk. songas ni wateja wa PAE.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 15, 2009

    uwa sielewi kabisa aya maswala,,me kila siku naona ni uzushi tu na kelele nyiiingi za siasa!!

    ivi why wamejenga mtambo mzito km uo apo ubungo??raiani na daraja kuu linalounganisha mji..sielewi

    agghh..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2009

    huyo anaeongea kafanana na P DIDY

    ReplyDelete
  8. Siunajua tena, P. DIDDY nae si ngozi ya tak.. kama sisi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...