Mdau katembelea alipozikwa mfalme wa Kung-Fu (Bruce Lee) na Mwanae Brandon Lee mjini Seattle na ameona si vibaya akishea nasi taswira hiyo. wapenzi wa filamu za hawa kina Lee walikuwa wanapata burudani ya pekee kila zinapooneshwa kwenye majumba ya sinema kama vile Empire, Empress, New Chox na Avalon ambayo yote yamekufa toka TV ilipoingia nchini.
Na hili linaamsha mjadala wa kwa nini wabongo hawapendi kwenda sinema kama ilivyokuwa awali. ni kichekesho kukuta kwa wenzetu ambako hizo TV zipo muda mrefu na tena zinaonesha sinema mpya mpya kila siku lakini bado utakuta foleni kwenye majumba ya sinema. Sie hapa kuna wakati majumba yaliyopo kule mlimani city na pale Mwenge saa ingine waoneshaji hugoma kufungua ukumbi kutokana na uchache wa watazamaji. Tatizo ni nini??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2009

    tatizo ni moja film hapa USA zinatoka mapema wakati Afrika zinachukua muda na zinakuwa tayari zimeshategenezwa copy nyingi mtaani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2009

    Filamu ikitoka Marekani, usiku wake iko Bongo na iko kwenye DVD. Halafu uanshangaa kwa nini majengo ya sinema yamekufa??? Piracy!!!! za kufa na mtu Bongo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2009

    ...kwa sababu ya kupiga vumbi kutafuta life...pesa yenyewe iko wapi wewe?

    heri ninunue copied CD nichek home

    ivi brandon kumbe nae alikufa?kwa kipi

    ok naona kila mtu siku izi anaitwa "KING" au "mfalme"

    king of pop,king of soul,king of kung-fu,king of R&B,king of gospel,king of reggae nk nk

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2009

    kaka michuzi, tatizo cc wabongo tunapenda vya dezooooooooo.....ukinunua TV basi na bajeti ya cinema imekufa hiyo....

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2009

    Tatizo ni gharama na pia uhamasishaji wa waonyesha sinema haupo. Yaani, huku ughaibuni, utajua ni sinema gani inacheza kwa wiki hiyo kupitia vipindi vya TV. Na bei sio mbaya kutokana na hali halisi ya huku, ila kwa bongo utakuta bei siku nyingine ni Tshs 7000 na familia zetu hizi za extended family, lets say its five of you. Muifate sinema huko mlimani city na mjiandae na Tshs 35,000. Nashauri bei iwe chini kidogo, sijui sasa hivi ni bei gani ila nlivyoondoka bongo it was around that amount.

    My two cents..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2009

    Wabongo hatuwezi kwenda kuangalia film, kwenye majumba ya cinema, kwa sababu, hatuna cinema mpya zinazo onyeshwa kwenye TV,usemi wako hapo juu ninaupinga.
    Uku ughaibuni, cinema ikiwa katika majumba ya cinema, inakua bado haipatikani kwenye DVD mitaani au madukani, wala huioni kwenye TV.ni vitu ambavyo vipepangwa na hati miliki,ukiwanayo kabla ya kutolewa rasmi kweye majumba ya cinema, utachukuliwa hatua za kisheria za hati miliki.
    sasa wenzetu utaratibu huo wanao, na ni wastaarabu.
    Kuna muda maalumu ulio pangwa wa kuionyesha cinema kwenye majumba ya cinema, ukimalizika, wanatangaza rasmi kua sasa inapatikana kweye DVD.
    Sasa cinema, ni lazima utakua na hamu ya kuiona cinema ikiwa bado mpya, hivyo ni lazima uende kweye jumba la cinema.
    Pia ni raha ukiwa na mpenzi wako, sio sawa na mkiwa nyumbani mnaangalia TV.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2009

    Tatizo la bongo wanazipata movie mtaani yaani bootleg then inakuwa ngumu kwenda kuspend pesa yako kuingia kwenye thetre. Kwa upande wangu mimi nashauri watu wajali zaidi quality maana kwenye thetre movie unai feel, kwa bootleg ama kanya boya mara saa ingine unaikuta inatoa chenga kupita kiasi. Mwisho aliyeuwa majumba ya sinema ni hao hao wadosi maana wanadubliketi na kuwapa chinga wanauza mtaani

    ReplyDelete
  8. Bill gate- SeattleJuly 10, 2009

    Kweli Mdau naona kweli uliapania siku utakayo ingia USA toka Bongo lazima ufike kwenye kaburi la Bruce .. lazima watu wajue umeshaingia USA welcome jiji la Seattle...
    nakumbuka enzi hizo kila mtu alikuwa najifanya .. mbabe kama Bruce Lee lazima atembee na chain zilitengenezwa na Magongo
    siku moja nilikula mkon'goto sitohusahau nilipofumua kitanda cha baba na mimi kuiga kutengeneza hizo chain ,,

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2009

    MKUU WA NANIII...TATIZO LA MAJUMBA YA CINEMA BONGO BAADA YA WAMILIKI WA MJUBA HAYO KUWA WABABAISHAJI MWANZONI MWA MIAKA YA 80'S BADO WANAONYESHA,SHOLAY,FRIDAY,FOX BROWN,THREE THE HARD WAY,DEATH WISH NK.KWA KUWA WALIKUWA HAWANA UWEZO TENA KULIPIA PICHA MPYA,WAKATI HUO MAJUMBA YA KENYA YANAJAZA KWA PICHA MPYA KAMA FIRST BLOOD,FULL METAL JACKET NK.NASIO KWELI UKU DUNIANI PICHA MPYA ZINAONYESHWA KWENYE TV,NO ZINATOKA KWENYE MAJUMBA YA CINEMA MPAKA BAADA YA MUDA ZINAONYESHWA KWENYE CABLE TV,ALAFU DVD BAADAE NDIO KWENY CHANEL ZA KAWAIDA ZA TV NA PIA WANALIPIA.HIVYO SIZANI WAONGOZAJI WA MAJUMBA HAYO ULIOTAJA YA MWENGE NA CHUO KAMA WANAUWEZO WA KULETA PICHA MPYA NA WAKIWEZA KUFANIKIWA HILO MAJUMBA YAO YATAJAA TU,TATIZO LETU WABONGO KURUKIA BIASHARA BILA KUFANYA UTAFITI WA KUTOSHA BASI WAONYESHE GAME ZA BWAWA LA MAINI ISIWE TABU.

    ReplyDelete
  10. Al MusomaJuly 10, 2009

    Let me see what I can recall. Yes, in Fist of Fury the hero appeals to some wapambes: "I have come here to avenge my teacher. This does not concern you. I allow you to leave. Out, out, ouuut..." Just what he does to the poor wapambe ngangaris as they resist going out peacefully. He then goes to the poor Japanese who had killed his teacher and the whole game goes bang...That was him, the greatest - yes, like Maradona, like Muhammad Ali and, of course, like you...

    ReplyDelete
  11. mbona makaburi ya wenzetu wanajenga simple hivi wakati sisi tunajenga kufuru wakati hela yetu ndogo ukilinganisha na hao watu.hapo angekuwa ni bongo mimi siujui.lakini nimeshaona.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2009

    It's very funny kwamba wabongo tuliona TV ndio replacement ya majumba ya Cinema,kwenda jumba la cinema kuna raha yake as an outing for a family or friends,for a date and so on so forth,then there is that Mighty huge screen and the sorround speakers...wow.the point here is wabongo tunajifanya tunaendelea faster matokeo yake twachemsha [Nairobi majumba ya cinema yapo mpaka leo]na bado yana attract customers.so it's a matter of wao wenye hayo ma-Theaters kuwa creative na business zao,kama watu walienda enzi zile DRIVE-IN kuangalia sinema za kidosi bila kuelewa kinachosemwa, sembuse saa hii ambapo at least watu wanajua hata cha kuombea maji.so ni ulimbukeni kwa waendaji sinema, na kugive up kwa wenye biashara zao.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 10, 2009

    Tatizo bongo usalama ni mdogo, vibaka wengi usiku,tutaendelea kutazama akina ze komedi nyumbani.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 10, 2009

    Kwa kweli ubora wa sinema ya bootleg ni aibu. Watu sio kwamba hawapendi kwenda sinema. Tatizo kubwa ni uwezo. Kuna mdau amesema kiingilio ni shs 7,000. Hizo hazifikii dola 6. Kiingilio cha sinema Marekani kutegemeana na sehemi ni kati ya dola 7-10. Lakini ukilinganisha buku saba ya kipato cha mbongo na dola nane ya mbeba maboski basi mbeba boski anaenda sinema. Kitu kingine ni kuwa wenye majumba ya senema ughaibuni biashara yao kubwa sio kuonyesha snema. Biashara yao ni vyakulavyakula. Wanavutia watu wengi kwa snema ili wawauzie bisi na soda. Wenye majumba yetu ya snema waangalie namna gani wanaweza kuwafanya wateja wao wamepata kingi kwa kidogo ili mtu awe tayari kutenga 35,000 ya bajeti yake ya mwezi kwa ajili ya kuitoa familia walau mara moja kwa mwezi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 10, 2009

    Wote mliotoa komenti zenu mko sawa kabisa, lakini tatizo kuu pale bongo ni 1-NO MONEY NA 2-No SPENDING POWER. Asilimia kubwa ya wananchi ni mapato yao ni kidogo sana- Hivyo hawako comfortable kutumia vijiela vyao kwenda muvi badala ya kuibajeti kwa chakula.
    Ni asilimia ndogo sana ya watu wenye uwezo na waliocomfortable kuspendi.Hawawezi hata kujaza Mlimani movie. Hii inasababisha majumba ya sinema kukubali cheaper deal from holywood na kuonyesha muvi ambazo tayari zishashuka bei maana Marekani zinaanza kuingia kwenye DVD-Ndo maana utaona filamu chache zinaletwa bongo(Baada ya Muda hii Inakill Hizi thieters). Wachina wanaturahisishia wanajua Majority Africans are poor & spending power yetu iko low wanatuuzia Buutleki walizorekodi kwenye thieter zao china-Ndo tunazoweza afodi.(Simaananishi ni vizuri lakini tunaitaji kuona movie pia-hata kama ni maskini!)- Hii inasababisha kufa kwa thieters.
    Hali ya kiuchumi inavyozidi kuwa mbaya-WanaNCHI WANAUMIAAA sanaa na wanaweka Pleasure kama kwenda muvi pembeni-lakini wanakula BIA na kajiBarMAID mwisho hununua CHEAPER Bootlek DVD or VCD kuyatuliza maumivu ya kiuchumii.....Huu ndo ukweli.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 10, 2009

    Jamaa ni mu england au?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 10, 2009

    Mdau 01;04 thanks for the narration,but that wasn't the point.au na wewe ulikuwa unazungukwa na washabiki kijiweni ukiwahadithia movie[chumvi kibao], so concerntrate here people are trying to discuss important business issues,PEACE.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 11, 2009

    piracey! na bootleg ya bongo utasikia sauti za watu wanacheka nyuma...Ujue hiyo movie imerekodiwa watu walivyokua wanaiangalia kwenye cinema na camera za simu.....

    Bongo hiyo mwemenyo mwemenyo tu no quality = good time - dezo

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 11, 2009

    Kila sehemu unaweza kupata movie mtaani, kwanza huku majuu unaweza ukapata movie hata haijatoka theater so, hiyo sio point. Kwenda theater kuna raha yake Wabongo ushamba mwingi, si wanasema Bongo tambarare kwa maana hiyo basi peza inatakiwa isiwe ni tatizo na pia huyo aliyesema sijui usiku kubakwa or sijui kitu gani pia hiyo sio point ni mambo mangapi watu wanafanya usiku mbona hawaachi kwenda kwenye majumba ya music hebu mstake kutuletea hapa.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2009

    unaesema "wabongo ushamba mwingi"
    wee ni kitu gani???

    au kubeba box ndo wajiona umefiiika

    wewee grow-up poor chick!!

    watu wanaenda na kurudi majuu km hawana akili zuri!!

    ni hali duni ya maisha na life style yetu,wengi hawajalelewa mazingira ya ki-vekeshen mtu anajifuzia ukubwani exposure!!incuding balozi wa nanihii!!bisha

    sio muhima kiivo jumba la sinema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...