maktaba na daily news ya zamani
maeneo ya posta mpya

maeneo ya haidary plaza
upande wa st. alban





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2009

    upande wa st alban na maeneo ya posta mpya si ni picha ileile. upande wa4 wa dar uko ? wapi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2009

    BRO MICHU MIMI NITAKUSHUKURU SANA UKITUPA RAMANI YA DAR ILIYOJIKITA ZAIDI KWENYE KUONYESHA BARABARA KUU ZA JIJI. NAJUA MZEE WE JUNGU KUBWA HUWEZI KUIKOSA. WENGINE DAR TUMEKAA MIAKA ZAIDI YA 10 LAKINI UKITUDONDOSHA KARIAKOO GHAFLA AU MNAZI MMOJA AU PALE MNARA WA SAA HATUTAJUA PA KUTOKEA KWA SABABU MJINI NI MJINI TU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2009

    Yes nice view, you remind me of our maskani in the corner of dar instute those days, i remember michuzi some time you use to come and chill b4 after work b4 heading home for the next day of miangaiko. AKHSANTE SANA KWA PICHA HIZO ZIMENIPELEKA MBALI SANA BRO,THNKS AGAIN.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2009

    Manshallah
    Dar has changed so much
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2009

    Dar inapendeza!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2009

    Nice view from rooftops. I wonder how is Dar looking from the street level. I can just imagine.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2009

    Samahani wadau nina swali kuhusiana na hizi picha;hivi huu mji wa Dar Es Salaam ni mji wangapi hapa afrika? mbona unatisha sasa hivi mno! au ni majumba tu hamna maendeleo ndani yahayo majengo! au kwanini huyu mheshimiwa aliye tupa hizi picha za mji kwanini hakutuwekea picha za balabala?kwasababu mji unapendezeshwa na vitu kama nyumba ,balabala,mitaa ilivyo pangwa, sio shagalabagala,ila tz imejitahidi kubolesha jiji.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2009

    Wewe anon ambaye unadai ukishushwa Kariakoo hujui pa kutokea lazima utakuwa WAKUJA, nyinyi ndio mnaokuja Dar kuomba Visa tu, mtoto yeyote wa mjini hawezi kupotea Dar.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2009

    Labda ungesema pande 4 za katikati ya Dar.....Dar ni pamoja na maeneo ya USWAZI....tuonyeshe na pande hizo!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2009

    Kwani gorofa ndizo zinapendezesha miji? Je zingekuwa nyumba ndogo ndogo tuu, jiji la dar lisingependeza? Ebo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2009

    michuzi post hii tujadili




    Trafiki anyang'anya ndinga...atumbukia mtoni!
    Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa PC Omary, amenusurika kwenda kuzimu baada ya kupinduka mtoni wakati akiendesha gari alilomnyang'anya dereva mmoja akimtuhumu kufanya makosa.

    Mbali na kupinduka mtoni, askari huyo mwenye namba F 1634 alimgonga na kumvunja miguu yote miwili mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Mpanda, Juma Kilombili(13) aliyekuwa akiogoa mtoni.

    Kabla ya tukio hilo, askari huyo alilikamata gari hilo Toyota Mark II namba T253 AHD linalotumika kama teksi baada ya kufanya makosa ya kawaida ya barabarani na kuamua kuliendesha mwenyewe ndipo alishindwa kulimudu na kutumbukia mto Misungumilo.

    Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,baada ya gari hilo kutumbukia mtoni, lilimjeruhi kinoma msela huyo ambaye alikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu.

    Kwa mujibu wa suka wa gari hilo aliyejitambulisha kwa jinala Bw. Frank, alisema tukio hilo lilitokea Julai 12 saa 6 mchana wakati akimpeleka mteja wake eneo la Shule ya Wasichana Mpanda.

    Alisema alipofika maeneo ya mto Misungumilo, alikutana na trafiki huyo ambaye alimsimamisha na kumyang'anya kadi ya gari huku akimwamuru ampeleke mteja huyo halafu arudi eneo hilo.

    "Niliporudi, aliniamuru kushuka kwenye gari, mimi nilimtaarifu bosi wangu kwa simu kuwa gari limekamatwa. Askari huyo alininyang'anya funguo na kujaribu kuliendesha, kwa kuwa nililiegesha pembeni mwa barabara alipowasha tu, liliserereka kwa kasi na kutumbukia mto uliokuwa karibu na kumgonga mtoto aliyekuwa akioga baada ya kufua nguo zake hapo mtoni,"alisimulia dereva huyo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 17, 2009

    jiji likua, natumaini baada ya miaka mitano ukipiga katika kona ulizopiga mambo yatakuwa tofauti. kila la kheri bwana michuzi kazi ni nzuri.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 17, 2009

    -mdau Fri Jul 17, 06:54:00 PM unatumia initials D K?..

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 18, 2009

    Ooohhhh Dar'salama. Siku moja nitarudi!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 18, 2009

    A spectacular view! Vipi kwa chini yaonekanajee? Please let us see it.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 18, 2009

    Shukrani mdau Tarehe Fri Jul 17, 10:10:00 PM, kwa taarifa yako hii, yaani nimecheka mpaka mbavu zinauma na machozi yanatoka... lol, naona leo ntaendelea kucheka siku nzima...
    Michuzi ibandike mezani hiyo post tafadhali watu waijadili.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 18, 2009

    WEWE ANON WA FRIDAY 8:37 ACHA MANENO YA KASHFA KWANI SUALA LA WAKUJA LINAHUSIANA VIPI NA HIZO HABARI? JARIBU KUTUMIA AKILI JAPO KIDOGO HII BLOGU SI SEHEMU YA KUTOLEA KASHFA..KWANI KUWA MTOTO WA MJINI KUNAKUSAIDIA NINI? USIDHARAU WATU.KUNA WENGINE WAMENYAMAZA LAKINI HUWEZI KUMECHI NAO ILA KWA SABABU WEWE UNA MAWAZO MAFUPI NA AMBAYO YASIYO YA KISTAARABU UNABWABWAJA BWABWAJA TU...JARIBU KUWA NA MAWAZO YA KARNE YA 24 USIENDELEE KULETA AIBU TUKAENDELEE KUKUCHEKA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 18, 2009

    PICHA ZOTE HIZI ZIMECHUKULIWA TOKA GHOROFA ZA JUU ZA JENGO MOJA TU, JENGO JIPYA LA HOLIDAY INN

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 19, 2009

    WABEBA MABOKSI MPO? UCHUMI WA DUNIA BADO UNACHECHEMEA, BONGO INASONGA MBELE. SWALI KUU: ARE YOU THE PART OF CHANGING TANZANIA. ARE YOU UTILISING THE OPPORTUNITIES AU WALEWALE MALALAMIKO KIBAO.... THE FUTURE OF TANZANIA BELONGS TO TANZANIANS.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 19, 2009

    Kwa muonekano picha hizi hazina tofauti na picha tunazoziona za majuu au kwa walioendelea. Tofauti ya kwetu na kwa waliostaarabika ni usafi tu, maana mpiga picha akishuka tu chini taswira yoote ni kinyaa kitupu.

    Picha zimenifurahisha japo nina uchungu na ubomoaji wa majengo ya zamani sana.

    GJK

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 20, 2009

    Hizi si pembe nne za dar. Labda tuseme ni pembe nne kutoka sehemu moja ya jengo pale picha zilipochukuliwa. Picha za uswahilini kama Manzese, Kwa mnyamani, Tandika huko ziko wapi? Au siyo sehemu za Dar?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 20, 2009

    haya mambo tulishayakosea siku nyingi bwana mji wowote unapendeza kwa kuwa na barabra za maana na parking za kueleweka haya majengo yote yangekuja baada ya barabara na sio barabara kuja baada ya majengo viongozi wetu utadhan hawaoni kwenye nchi za wenzetu huko wanakoenda kufanya ziara kila siku, tujifunze kujituma na tusiwe wavivu wa kufikiria jaman tutafika tu ila si leo wala kesho sisi tukifika wenzetu sijui watakuwa wamemaliza na kuanzisha sayari nyingine eeeeeh mola.
    Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...