Home
Unlabelled
policeman woes
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hivi kuandika kwa kiingereza ili iwe nini!! hii ndio kasumba kubwa kwa nchi yetu kila mtu anadhani kiingereza ndio dili na kujua mambo. bango hilo lilisitahili kuandikwa kwa kiswahili ili kila mmoja aweze kujua kilichomaanishwa hapo.
ReplyDeleteWabongo tusipobadilika na kuacha kasumba ya kukumbatia kiingereza ipo siku tutakuja kujiuza kwa weupe kwa bei chee na wao wakachukua nchi.
Duh!
ReplyDeleteNilidhani mwalimu ndiye ana hali mbaya zaidi!
jana nilikuwa naangalia american action moves, nikawa najiuliza, polisi wao wanaigwa vibaya kweli, kama watu fulani wasio na akili, wanaokimbia na magali yao bila tahadhari, wanakufa ovyo katika maonyesho yale, je kweli hii inarefrect kaukweli. sasa kova kasema ukweli.KAZI MBAYA SANA HII.
ReplyDeleteLAKINI WENGI SHULE HAKUNA
Kasumba ya kudhani kuwa ukijua Kiingereza basi wewe ndiye msomi itatuisha lini? Bango kama hilo haliweandikwa kwa Kiswahili mpaka kwa Kiingereza!! Afande Kova, Watanzania wangapi wanakimudu Kiingereza sawasawa? Achana na hiyo kasumba Afande. Hiyo ni Polisi jamii, na jamii yenyewe inajua zaidi Kiswahili katika mwasiliano yao kila siku!
ReplyDeleteHilo Bango lingekutwa ktk ofisi zozote za polisi ktk nchi zilizo endelea, Basi Mkuu wa Polisi au wa hicho kituo hangefukuzwa kazi kwa kupotosha umma ya kwamba Polisi ni kazi mbaya ambapo anawaambia raia wachague kazi nyingine na kuacha hiyo kazi ya polisi, pia inapotosha umma kwamba polisi wanachukia ambapo wao ndio wanatenegeneza hiyo chuki,n.k. Wanataka nini cha zaidi?
ReplyDeletePia inasema kwamba Polisi hawatendewi haki zao mbele ya raia, Serikali, mahakama n.k. Ina maana Mahakama haijui kazi yake na sheria? Ina maana Wanasiasa, Bunge, Serikali hawajui kazi yao na wanaonea Polisi?
Kama mfanyakazi wa umma na raia wote, Polisi hautakiwa kupiga kelele hizo za kitoto, Polisi sio sehemu ya kukata nywele na kukutana na mabango yasio kwenda shule, Polisi ni sehemu kubwa na kuheshimika na ningemuomba yoyote anaye husika watoe ilo Tangazo lenye kuonesha Utoto uliokuwepo ndani ya ofisi hiyo mara moja. Pia aliye liweka haelewe hiyo sio ofisi yake binafsi au nyumbani kwake kwa kuweka mabango ya ovyo ovyo na ikiwezekana awajibishwe.
Natumai Viongozi na Raia wote wataona mantiki yangu.
Pamoja na mapungufu ya kuandika lugha hiyo ila maneno yote yana ukweli!!!! hongera Kova.
ReplyDeleteMhhh...brother Michuzi una kazi kweli kweli. Sasa hawa wanaolalamikia hili bango eti tu kwa kuwa ni la kiingereza si ni watu wa ajabu "waosha vivywa" Je kama afande ameyapata hayo maneno yakiwa yameandikwa kwa kiingereza, wanataka aanze kutafuta hati miliki ya kutafsiri ama??!! mfyuu. Bora anonymous huyo wa pili na wa tatu wamejaribu kuchachangia kwenye muelekeo, nyie mnolaumu lugha iliyotumika, kama mlikimbia umande kazi kwenu. Ha ha haaaaa!! ki maisha plus!!
ReplyDeleteHILO BANGO LIPO HAPO TOKA ENZI ZA KAMAMNDA WA KANDA MAALUM YA DALISALAMA KAMANDA TIBAIGANA
ReplyDeletekaka Michu , lugha ni lufgha tu watuw asijipendekeza,. Ujumbe umefika hatutarajii mtu anayekuw apolisi awe anajua kishwahili pekee tunatarajia awe anajua angalau kiswaenglish. kamanda kova naipenda hii staili yako ni kweli tunalazimika kubadilika na kutoa ushirikiano kwa polisi. Ni kweli kila kitu hapo na waoshwa vinywa vyao wakome kabisa kama huwezi kusoma achana nao hata mtoto wangu ataenda kusoma na kuona madhila yanawakumba polisi wka sababu ya ubazazi na upuuzi wa kuanzia viongozi mpaka sisi tunaolindwa. Big Up kamanda kova umenipa somo kubwa la kujali polisi.
ReplyDeleteJamani hilo Bango limenunuliwa na hayo maneno. Kwa hiyo msimlaumu Kova kuwa hajatumia Kiswahili, siyo maneno yake. Kama akitokea Msanii aandike kwa Kiswahili nafikiri itanunuliwa sana. Wasanii wetu sio wabunifu. Hilo ndio tatizo.
ReplyDeletemimi nataka kujua kuhusu hilo tangazo
ReplyDeleteinamaana inawahusu police wa kiume peke yake? mimi naona kuna "he" peke yake, mbona hakuna 'she" au sijui kusoma vizuri?
Solder badala ya soldier kweli english is not reachable...nimesema mi maimuna.
ReplyDeleteUpande wangu ningemshauri Kova angeweka bango jengine linalowasifu Polisi kwa kuongoza kwa kuchukua rushwa , kuwafungulia raia kesi za uongo,kuua raia wasio na hatia , kutesa na kupiga mahabusu wanapokuwa kwenye selo zao na kushirikiana na majambazi naona ukumbi wake wa mikutano ungependeza zaidi.
ReplyDeleteEnglish hiyo ukiileta Marekani hakuna mtu ataielewa ..daah MBONA NYIE WABONGO MNAPENDA KUTUMIA kingereza kigumu .. wakati kiswahili hamtumii misamiati
ReplyDeletehivi nyie ma annony mnaolaumu bango kuandikwa kwa kiingereza, nadhani pia mnahisi ni Kova kaliandika..eti pia likikutwa nchi za wenzetu atashtakiwa.. guys take a break !! limenunuliwa hivyo hivyo, ukitafsiri lugha yoyote ile kwenda lugha nyingine unapoteza maana yake kwa asilimia 10 kwahiyo ibaki hivyohivyo, hata ofisini kwa nurses kuna mabango abt nursing jokes so as every profession especially lawyers, inaelekea ma annony mnapenda sana kuosha vinywa na kuponda mtu akiandika kiingereza, why ? are you scared of something? eti nchi itauzwa kweupee kwa kuponda kiswahili..kwa taarifa zenu nyie ma annony nchi inauzwa kwavile hamjui kiingereza ! and that's a fact !msijifiche chini ya uzalendo na kushindwa kubadilika kisa...??
ReplyDeletendo maana hatupatani nao
ReplyDeleteyan walishaanza kujinyanyapaa wenyewe ivo?
ndio ni polisi "he" wanaume tu
euwiiiii
Mdau #1,tujiuze mara ngapi? it's been done.so come with a solution,sio kukaa kulalama kuhusu kiingereza,kama mababu zetu hawaku object then wewe utafanya nini about it? njoo na majibu sio kelele za Universal languages,kwani unavyokuwa ulaya unaongea kiswahili hata wao hawafurahii,so eat that.
ReplyDeleteTATIZO WATANZANIA TUNAPENDA SANA WOTE KUWA CHINI. MASIKINI ANAMWOMBEA VIBAYA TAJIRI ILI AFILISIKE AWE MASIKINI KAMA YEYE BADALA YA KUFANYA JUHUDI NAE KUJIKWAMUA. WENGI WASIOJUA KIINGEREZA WANAWA-DISCOURAGE WANAOKIJUA WASIKITUMIE, ETI WANAJIFANYA WANAJUA SANA NA WAMESOMA SANA, USIYEKIJUA FANYA BIDII UKIJE OTHERWISE UTAACHWA NYUMA KWENYE DUNIA HII YA UTANDAWAZI. TUKO KATIKA KIJIJI KIITWACHO ULIMWENGU, HATUNA NAMNA YA KUJITENGA. KISWAHILI KINATUMIKA NA WATU WANGAPI KATI YA WATU BIL 7 WALIOPO ULIMWENGUNI LEO HII!! NA ENGLISH JE? KWA WANAOPENDA MAENDELEO KATIKA NYANJA ZOTE ENGLISH IS UNAVOIDABLE, MNAOTAKA KUJIFUNGIA TANZANIA NA KENYA TU ENDELEENI KUNG'ANG'ANIA KISWAHILI. SIO KASUMBA, NI ALAMA ZA NYUKATI! MSIDANGANYE WATU NYIE MSIOTAKA KUJIFUNZA NA KWENDA NA WAKATI. KALAGABAHOO! ANYWAY, UPOLISI NI KAZI NGUMU SANA, YA MASHUJAA TU! KEEP IT UP KAMANDA KOVA. VIATU VYA TIBAIGANA VIMEKU-FIT VIZURI SANA!
ReplyDeletenyie nyote mnaompiga mawe kova mko wapi? mnadhani hayo maneno kaandika kova? hayo magamba unaweza kuyaona sehemu tele za maduka (market places)
ReplyDeletekwa ufupi hayo sio maneno ya komba ila kwa kubandika hapo anaonyesha kukubaliana na kilichosemwa.