wakazi sita wa dar ambao wamefikishwa kizimbani leo kwa shtaka kusafirisha isivyo halali pembe za tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700 na kukamatwa Vietnam karibuni. wote wameshtakiwa mashtaka ya kuhujumu uchumi.

WAKAZI sita wa Dar es Salaam leo majira ya mchana wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa mashtaka lukuki lakini moja kubwa ni la uhujumu uchumi.

Shitaka hilo la uhujumu uchumi linauhusiano na usafirishaji wa pembe za ndovu zenye thamani ya zaidi Sh milioni 700.

Kwa habari kamili

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    ufisadi ndio aina mbaya zaidi ya uhujumu uchumi waa tanzania lakini cha kushangaza wanafumbiwa macho na kupeta tu mitaani. hawa wa pembe za ndovu si ajabu wakafungwa kesho tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    Mbona tunapigana changa la macho kila siku? sisi tunaowaitaji ni wenye mali hiyo, wako wapi? kuwashika watu walioklia mzigo sawa, lakini wamiliki wa mizigo hiyo ni akina nani? mbona awatajwi?
    Hao ndio wabaya zaidi kuliko hawa waliokamatwa, maana hao ndio walioua tembo wetu na kufanya ujangili mkubwa.

    Tatizo hili la kulindana litatumaliza kwelikweli.watajwe hata kama ni wakubwa ili tuwajue hapo ndipo tutakuwa tumetatua tatizo.na wala si kuwashika watu wanaohusika na ukaguzi na usafirishaji. ndio maana naita tukio hilo kama ni changa la macho.

    ReplyDelete
  3. jamani pia weye Gab.... umejiingiza katika hilo balaa...., mbona tamaa zitakumaliza....ama ndio unataka utajiri wa haraka haraka! kwakweli vijana wana madeal duh.....ukiwaona hata huwezi dhaniaa kumbeeeee.....yangu macho...

    ReplyDelete
  4. Asante Jakaya kwa kupambana
    Uhujumu uchuni!!!
    Hizi kesi zinanikumbusha kipindi cha mwalimuuuuu
    ataunaziomba mahakama zisiishie kwenye kesi tuu
    tuone watu wakihukumiwa pia

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2009

    Duuhh, watu wanatanua mjini kumbe shughuli ndio hii. Kaaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2009

    Kweli naungana na mdau hapo juu, Aliyesema waliokamatwa ni watendaji kwenye nafasi zao za kazi kila siku. Sisi watanzania tunapumbazwa tu. Tunataka wamiliki wa mali au Original dealer hapo tutaelewa somo. Vinginevyo ni usanii mtupu; We jiulize kesi za kina Zombe; Liyumba na Mafisadi waliotwa zimeishia wapi? kimya mazee ndio mnasahaulishwa kiaina . subirini 2009 mwisho na 2010 mwanzo mtaona vibarabara vya mtaani vinapingwa lami mara Mkopo kibao;yote hiyo nikujenga mazingira ya kusahau yote na kuchagua the same people next election. Amkeni watanzania jamani ;hii balabala mpaka lini;

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2009

    Jamani huyu kaka wa kwanza hapa kulia kwangu mi naeandika, mwenye blue jeans na white shirt, yaani namjua kabisa, sijui hata nimemuona wapi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2009

    chambo baba kamua kamua tuu hakuna lolote utatoka tu mwanangu hako kanchi kashaoza wahindi wakiiba its ok tena wao wanaiba ela bila kuzifanyia kazi hawa vijama wameifania kazi hii ela kuuwa tembo si mchezo mazee

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2009

    Hawa ndo wanaume wa nchi hii.
    Imefikia mahali unachokiona mbele yako chukua tu.
    Potelea mbali maisha yajayo.
    Uchungu,uchungu!!!!!!!!!!
    Uchungu anao mja mzito.
    Mie nsha jikatia tamaa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2009

    Pole Chambo, huo ndio uanamme, yatakwisha tu, cha muhimu na nyinyi muwataje hao wahusika halisi ili msitolewe kafara kwa kumalizia pass tu ili hali kunamtu aliyeanzisha na kucheza game nzima.

    L.P

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2009

    habari ya leo ndugu wachangiaji Katika hoja hizi,maoni ya wengi ni njia moja ama nyingine yakuleta ufanisi, ama kujua ukweli au vinginevyo.Watu wote waliokamatwa hakuna hata mmoja mwenye hatia kwa maoni yangu,kama watu wangeelewa maana halisi ya clearing and forwarding,basi hakuna anayeweza kusema hawa watu wana hatia,anayejua siri nzima ni mwenye mizigo yaani shipper ambaye ndiye mteja wa watuhumiwa hao sita ndio hasa muusika mkuu agent hana uwezo kitaalamu wakujua kuwa hizo ni pembe za ndovu au mkia wa tembo au vyotevyote vile yeye kazi yake ni kuhakikisha mzigo wa mteja mnapakiwa ukiwa salama na seal za usalama pia kujua kama nyaraka za mzigo zimekamilika na umepakiwa melini na kuondoka kazi ya ukaguzi niya afisa maliasili wa bandari sio clearing agent au customs officer, pia kuna usalama wa taifa bandarini walikuwa wapi au ndio changa la macho,hao washukiwa wote ni uoneu mtupu hakuna mwenye kosa hapo kwa waliokamatwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2009

    weee aanze tu kusema boss wake..kama hajapotezwa ktk sura ya dunia
    jamani kuna wizi wa chain kama mafia walhai Tz

    Mungu tu aingilie,

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 24, 2009

    mweee...ndo mumeo unamuona apa..tobaa

    wanawake tuangalie sanaaa izi njemba zenye mihela-hela tu mjini,wengi wamenunuliwa na vigogo

    afu vijana wabichi kabisa..huruma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...