Wadau na Mh. Mkuu wa wilaya ya nanihii....
Naomba kuuliza, hivi ati ni kweli dayati kuu ya watani wangu Wapare ni Makande? Sababu ni nini haswa - Kuuliza si ujinga, halahala waosha vinywa tuheshimiane. Maana najua mmeshaamka saa hizi...
Ujumbe: Wapiga Boksi oye!
Wala Vumbi oye!
Mdau Moshi






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2009

    Sio makande, ni pure.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2009

    Siyo pure ni mpure.
    Nafikiri sababu hasa ya watani zako kula mpure ni kuendeleza ufupi.
    GJK

    ReplyDelete
  3. Mh. mkuu wa naniii ya naniiii, mbona wapiga boksi tunaandamwa hivi jamani. Mabox yenyewe mazito kikweli kweli, hebu tupeni break kidogo jamani. Na sie ni binadamu kama binadamu wengine, ila tu shule ndio hatuna, Ni hayo tu.
    Ahsante sana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2009

    Pure makende mchanganyo ni ule ule.Wenyewe tunaojua utamu wa kande ni wabena;asubuhi ni chai kwa kande,lunch ni ugali na maharage au kande na same thing kwa supper upo hapo mwenye swali la kizushi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2009

    Hicho chakula cha kuvimbiza tumbo wao ndo wanafanya dayati....makubwa!!! makapi kibao...halafu huyo aliyepika anaonekana mtaalam haswa lazima atakua mpare huyo..Cheki harage lilivyokolea!

    ReplyDelete
  6. Thithi tunakula pure wewe! thatha unachoshanga ni nini we mbwange?
    Likipikwa vizuri lazima husahau ujilambe na usahau vijisupu vyenu vya ndizi....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2009

    "Hey waosha vinywa Oyee...!!!Wabebabox Oyeee..!!!.Wala vumbi ziiii...!!!.Kidumu chama tawala...Chukua Chako Mapema".

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2009

    KABISA MIMI MWENYEWE NI MPARE NAMBA ONE HICHO NDICHO CHAKULA CHETU KIKUU!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 07, 2009

    OK KWA KUKUSIDIA KAMA ULIVYOSEMA CHAKULA CHA KANDE AU MAKANDE KUWA CHAKULA KIKUU CHA WAPARE UKWELI NI KAMA IFUATAVYO WAPARE NI WATANI WAKUBWA WA CHAGA,WACHAGA WANALIMA NDIZI NA CHAKULA CHAO KIKUU NI NDIZI SASA KWA WAPARE KWA KUWA WANAISHI ENEO AMBALO HALISTAWI NDIZI WANALIMA SANA MAHINDI NA MAHARAGE UKILINGANISHA NA WENZAO WACHAGA HIVYO IKAONEKANA KWA KUWA WANALIMA SANA MAHINDI NA MAHARAGE NA HAWANA NDIZI NDIO CHANZO CHA WAO KULA MAKANDE .

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 07, 2009

    Jamani tuacheni masihara hicho chakula sio cha diet. Au wewe umdau ulivyosema cha diet ulimaanisha nini coz mimi najua diet ni kile chakula cha kuufanya mwili usijae jae ovyo. Mfano kula tuu matunda na mboga mboga pasipo vyakula vya wanga.

    Ila tukubalini chakula hiki ni kitamu japo mimi sio Mpare lakini nakifagilia, ila kipate anayejua kukipika either kwa nazi or kwa nyanya sio tuu ilimradi.

    Weeee utajing'ata. Ila ukikaa baada ya masaa kama tumbo lako alipendi usumbufu ujue litasumbuliwa, na utasumbua watu kwa perfume.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 07, 2009

    Wewe uliosema walavumbiiiz! Plse tuhesimiane. Wenzio wanakula vumbi wewe unakula nini? Tuoneshe chakula chako cha utamaduni ndipo upate kusema utamaduni wa wenzako.

    Tatizo ni kwamba walio wengi wanadharau tamaduni zao ndio maana mnaishia kuwa watumwa wa tamaduni za wengine.

    Mwafrika kama mwafrika lazima ujivunie tamaduni yako. Usipojivunia japo tamaduni yako wewe ni mshamba, na mpumbavu.

    ReplyDelete
  12. hahaha MREVEDI(hamjambo??)

    ngoja nikuambie wewe,sie tuna kande na ikipikwa hiyo huta sema umeshiba lakini ukila yes that will be enough maana ita kuja tumbo sana, au KISHUMBA huwa ni ndizi na maharage kusongwa pamoja ,safi sana ilale halafu upate kesho asubuhi na chai wakati kishumba ni cha baridi wewe

    mie wa Kirongaya mwenzenu

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 07, 2009

    ETI KUNA MSEMO WA WATANI WA KICHAGA NA WAPARE UNAOSEMA,KULIKO AFE MCHAGA MMOJA NAFUU WAFE WAPARE 50,IMEKAAJE HIYOO MNAIPATA,,,,NIMEONA HUO MJADALA KATIKA BLOG MOJA INAITWA WWW.KILINYEPESI.BLOGSPOT.COM

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 07, 2009

    Jamani mkazana na wapale kwa kusema chakula cha asili, nadhani hamjawai kukaa na wabena au kutembelea huko kwao. Njombe, hicho ndio chakula chao haswa, wakibadilisha ni ugali na maharege, na wanalima sana mahindi na maharage

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 07, 2009

    weka na iliki umo ndani weeee!!!

    chakula iki tulikula saana bording skuli,sitaki ata kukiona now kivonkinaisha

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 07, 2009

    Bora wapare wafe 50 kuliko mchaga afe. Mchaga akifa maendeleo hakuna, mpare akifa anapunguza idadi ya wabahili.
    Japo mchaga anabahili lakini ni kwamaendeleo anajua uchumi. Angalia Dar or sehemu nyingine wachaga walivyojenga na kuendelea lakini wapare wakibahili wanabahili kinoma. Huoni akijenga, huoni akila basi ni shida tuu. Anaweza kula hata ugali kwa picha ya samaki au harufu. Mchaga hawezi hivyo.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 07, 2009

    Kwa mujibu wa swali lako muuliza swali ni kwamba siri ya chakula hiki kuliwa na hao uliowataja ni kuwa ni chakula halisi na kinafaa kuliwa na binadam yeytote yule ndiyo maana kinaliwa mpaka kesho kokote kule, Na siyo tu hao uliowataja bali hata makabila mengi na watu wengi wanakula tu!Swala la kusema hicho chakula kiko hivi na hivi ni mitazamo tu ni kama vile wenine wanapenda kula nyama wengine wanahitaji mboga za majani huu ni mtazamo wangu!Tusipende kuwa watumwa wa fikra potovu tutafika tu!

    ReplyDelete
  18. oya mi pia nimpare na kubali pure ni chakula chetu sisi ila achen kashifa hizo kande mnazo ponda ndo wengi wenu zina waweka mjin hahahaha achen unafki nyie mnaoponda nampa big up mdau alie sema ukweli but mnafki nooooooooooooooo.PURE NA PARACHICHI WEWE ACHA TU ALAFU LIKAUNGWA NA MAKWEME WEWE UTAJINOMA.

    ReplyDelete
  19. Jamani hawa Wapare na Wachaga vipi wana blog ya jamii?Kila mahali ukifika ni wapare na wachaga,mpaka hata Johanesburg South ukifika shughuli ndio hii watani wa jadi wapare wachaga,Nairobi,Mombasa,Maputo yaani sasa karibia miji mingi hata ulaya kila mji ukifika utamkuta mpare na mchaga,hii imekaaje wadau,hawa watu vipi?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 07, 2009

    Naungana na mwenzangu mmoja hapo juu,hivi kwanini siye wabeba box tunawapa shida sana?,maana kila kitu wewe mbeba box ,niwaambieni hizo box tunabeba inatusadia sana kulea familia zetu huko bongo,na wengine tumejenga kwa hizohizo box,ndugu zetu wanapendeza huko nyumbani shauri ya box,tukija likizo nyie ndiyo wakwanza kutubabaikia ,lakini kutwa hamuishi kutusema kwenye mitandao acheni zenu jamani kama alivyosema mwengu hapo juu nasiye ni watu kama wengine. box juuuuuuuuuuuu box oyeeeeeee

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 07, 2009

    we unaesema wapare ni wabahili hawali, tafadhali nenda shule,unaonekana bado una mambo ya kale sana,ulishaingia nyumba gani ya mpare anakula ugali napicha ya samaki,achana na wapare wanapanga bajeti na ni wachumi,mbona hukusema wachaga ni wezi wafe,bora wafe wachaga ili majambazi ya pungue nchini,na mpare mbahili anaomba kwako,au wataki wagawe pasa barabarani ili uwakubali,wapare wanakula vizuri na wanapeleka watoto wao shule na wapo kwa ajili ya familia zao na si kwa familia yako so waache na maisha yao na kande ni chakula kama chakula kingine chochote na maisha yanaenda,havacheni

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 07, 2009

    achana na wapare wewe wako juu

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 07, 2009

    Mandondo!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 07, 2009

    Thela wee !!

    avae avae!!!

    BAHILI BINGWA

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 07, 2009

    UNAJUA MAKANDE YANA KAA MUDA MREFU TUMBUNI NA KWA SABABU WAPARE WABAHILI NDIO MAANA KIKAWA NDIO CHAKULA CHAO KIKUU!!WE FIKIRIA MPARE ANAKULA UGALI NA PICHA YA SAMAKI!!MPARE HATA TUMBO LAKE LENYEWE ANALIONEA UBAHILI..MCHAGGA..NORWAY

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 07, 2009

    Wadau tuwe makini, kuna tofauti kati ya makande na makende.
    Achana na pure bwana. Unapokula hujisikii kushiba. Kasheshe masaa kadhaa baadae. Unaweza kushiba wiki nzima kama hujui siri hii.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 07, 2009

    JAMANI SISI WAPIGA BOKSII BIN BOX TWACHENI TUPUMUWE LAU KIDOG
    NASI KAMA NYINYI WANGALAMTONI JAMANI MBONA HESHIMA UANWAPONYOKA
    MDAU FOTO BARAZA

    ReplyDelete
  28. enzi za Nyerere wakati anafika UPARENI kwa mara ya kwanza kuitangaza TANU. hakujua kama Wapare wana maumbo , mafupi . wanaonekana wadogo .. kimaumbile .. "Akawaambia.. nyie watoto hamruhusiwi . kwenye mkutano .. nendeni kawaitani wazazi wenu ".. aitheee!! huyu mzee anatutukanaaa!!!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 08, 2009

    Wewe uliyeandika hili ulikuwa na lakojambo, kwasababu sio kweli kuwa chakula kikuu cha wapare ni Makande, inategemea unazungumzia Pare ipi. Ukienda Gonja na Usangi huko wanalima ndizi kwa wingi, chakula chao kikuu ni KISHUMBA, KIOMBO NA HAYO MAKANDE. Ukienda tambarare ambapo nahisi mhusika ndipo alipoangalia, wao wanakula ugali, hayo makande na mboga zao ni samaki. Na ukiangalia Kilimanjaro na Tanga vyakula vyao ndio hivyohivyo, ndizi, makande, ugali, maharage nk. Mengine ni utani wa kukosa kazi,au kuchangamsha baraza. Na huo ufupi mbona hamuwasemi wachina?

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 08, 2009

    Makande sio dayati yeti ila ni cha kula hupikwa kwa ajili ya mapunziko katika siku ya Bwana... Mpure jiliwa si kwa kilanga kana makadha. Thi kijo tha vijo vingi. Vampare ni vantu vakumtogola Mfumwa, he-na mithi ya kumtogola Uu Mfumwa ni mithi ya kuhena. Heicho hedikwa "MPURE" thiku fuhi twethinafikia ii siku mbaha ya kumtogola Mfumwa. "Kumbuka Mthi wa Mfumwa uugimbike": Mithi mtandatu ni ya ndima, uhire ndima jako jose;mira mthi wa kafungate ni wa kuhema ,ni muthi wa Mfumwa Mrungu wako. Uo mthi hasikete cho wehira, we mwenye neri vanao, neri vandima vako, neri nyama jako weyaja jehira ndima, neri mgheni eho hako...Sasa ndio maana tuna pika Mpure ili tupate kupumzika siku ya Bwana.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 09, 2009

    Mimi baba mbena mama mpare, na kote kuwili kande ni one of the main dishes. Na ni chakula kitamu sana. Kwa wapare pia kiombo na kishumba, kwa wabena pia ugali na maharage - safi!!! Na ndio, mimi ni mfupi, na nafurahia ufupi wangu. Niko South Africa na hata huku wana kande (samp and beans), ziko supermarket zimefungwa vizuri, mahindi yameshatwangwa kabisa - naziweka kwenye pressure cooker muda wa saa moja tu, kande!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...