Home
Unlabelled
tuzo milionea apewa milioni 100 zake leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mpeni hongera zake, lakini mimi bado siafiki mtindo wenu huo wa kutoa zawadi, na sio kwamba nalalamika kwasababu sijaipata hiyo zawadi, la khasha. Mimi ningeona badala ya kumpa mtu milioni 100, hiyo ingeweza ikagawiwa katika zawadi ndogo ndogo ambazo zingewasaidia wateja wenu wengi, badala ya kumpa mtu mmoja tu.
ReplyDeleteHilo ni wazo langu tu
M3
Huyu mzee amekuwa mkombozi wa jamii kubwa sana ya watanzania.....MUNGU kaiona kazi yake kaamua kumtunuku.
ReplyDeleteMBIJE,A-Kafanabo
Wagagagigikoko bwana si mungemuandikia checki tu mpaka mumpe makaratasi yote hayo.Halafu eti wanamwita milionea.
ReplyDeleteMillionaire definition:A millionaire (originally and sometimes still millionnaire[1]) is an individual whose net worth or wealth exceeds one million units of currency in USD
Mdau
USA1
Columbus
huo mtindo sio mzuri kabisa wa kutangaza kumpa mtu kiasi hicho cha pesa,ameshinda mmemtangaza mwekeeni kwenye account yake kwisha.namna nyingine mnamtia kwenye matatizo makubwa kwenye jamii.
ReplyDeleteHongera. Hivi wadau hizo pesa huwa zinakatwa kodi?
ReplyDeleteTULIKOTOKA NI MBALI!!
ReplyDeleteLEO NAWALETEA MASWALI KATIKA SOMO LA SIASA.
MASWALI YA LEO!!!
Chagua jibu sahihi kwa kuzungushia herufi husika.
1. Raisi wa kwanza wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anaitwa Julius Kambarage ________
(a)Kawawa (b) Moringe (c)Sokoine (d) Mandela (e) Nyerere (Maksi 30)
2. Chama cha kisiasa cha kwanza kutawala Tanzania kinaitwa Chama Cha _________
(a) Mapinduzi (b)Mafisadi (c) Chadema (d) Maendeleo (e) a na c (Maksi 30)
3. Raisi wa awamu ya pili Tanzania anaitwa Ali Hassani Mwi____
(a)Nyimvua (b)ke (c)nyu (d)ko
(e) Hakuna Jibu
(f) Majibu yote Sahihi (Maksi 40)
MWISHO WA MTIHANI
Ahsanteni.
Huyo mai waifu wake ni Anganile au?? Kafanana nae.....
ReplyDeleteDaah! Nimekumbuka mbali sana, Mkinga ulikuwa unafuatilia malipo yako pale Home Affairs, kama sikosei uko au ulikuwa Uhamiaji, God bless you more and more, umeanza kuhangaika siku nyingi.
ReplyDelete100 MILLIONS ZINAKAA KWENYE HILI BOX, KUMBE NI CHACHE HIVYO, AU KWA VULE MNA DENOMINATIONS ZA PESA KUBWA KUBWA, ZINGEKUWA 100 MILLIONS ZA DOLLAR NI MAGUNIA, HATA HIVYO SINA UHAKIKA KAMA HIZO KWENYE BOX NI 100 MILLIONS AU HIZO NI SAMPLE ZA KUTUONYESHA KWENYE LUNINGA?
ReplyDeleteJamani nielewesheni. Hivi hapa watu kusifia dollars, USD n.k. na kuponda hela za madafu ni watumwa? Mi siwaelewi. heri umasikini wa fedha kuliko wa mawazo!
ReplyDeleteKweli maisha ni kama mchezo wa soka, usikate tamaa kama dk 90 hazijaisha. Mzee Mkinga bila kwenda SA kwenye BBA amekula Bingo ya kufa mtu...kwa ufupi hakuna lisilo wezekana.
ReplyDeleteHongera kwa aliyepata hizo pesa. Usemakweli, kama alikuwa anamatatizo mbalimbali ambayo yalikuwa yanahitaji kutumia pesa kuyatatua, basi Mungu kamwona.
ReplyDeleteTatizo ni kwamba ukitoa, hata shilingi miatano katika hiyo milioni miamoja basi sio milionea wa miamoja tena.
Subiria watu watakuja wengi kuomba msaada, kwani sasa hivi wanajua una milioni miamoja, halafu watakuwa wanasema, hata ukinipa laki tisa sio mbaya hela yote hiyo.
Wengine watakuja kujitambulisha kwako kama: Mimi ni binamu wa shangaziyako aliyekuwa jirani na mjomba wako aliyekuwa mdogo wake wa baba yako na alikuwa rafiki sana tena rafiki wa kweli, sasa bwana naomba unisaidie hata elfu kumi tu.
P.E.D
Hongera sana mshindi.
ReplyDeleteNina mtazamo tofauti kuhusu hii: Kwa kampuni kama Vodacom inayofanya biashara "Tanzania", kumpa mtu mmoja zawadi ya Milioni 100, sithani kama ni busara.
Mdau
Reading, UK.
Duh huyu jamaa si yule anakuaga kipindi cha sema usikike ITV anatoa michanganuo na mawazo mbalimbali kuhusu mustakabali wa nchi.
ReplyDeleteDuh jamaa mjua mengi sana.Ana data za ishu zote political,social.economical.
Kama sio maswala ya voda kupanga ushindi.basi jamaa mungu amemlipa kwa michango yake.Japo mwishoni MWA MADA ZAKE huwa ana malizia kwa kuonesha kua ni kada wa chama tawala.Hongera usiache tena kuwakilisha sauti zetu wanyonge.endelea sema usikike
NDUGU Zangu mnaojidai mmestaarabika acheni ushamba.. kwanza katika dunia hii kweli unaweza ukapewa hata Tsh 10m/- in cash? Nasema TSH kwa kumaanisha shilingi ya Kitanzania. Na kama mmetoka Tanzania siku nyingi, siku hizi BoT policy ni kwamba any payment above Tsh 10m/- hata cheki huandikiwi, it is paid direct to your bank akaunt via TT. mpe hapo wasomi wetu wabeba maboksi? Ok, na pia I believe mnafahamu maana ya Prize giving ceremony and an action for the press. That brief case full of makaratasi was for the press action, ili kupata action picture Watanzania tuliobaki nyumbani tuweze ona.
ReplyDeleteWaaleykum Assalaam