Mheshimiwa Michuzi,
Nakuomba unipe fursa ya kuzungumza na jamaa waislam. Aidha kwa ndugu wa dini mbali mbali naomba radhi.
Ujumbe wangu ni kuwa ramadhani is approaching“If Allahs servants knew what Ramadhan was, they would have wished it lasted for the whole year(Prophet pbuh}
And I would like to remind my brothers and sisters to consider fasting the six days in Shawwal ie the month immediately after Ramadhan. The reward is very great, for your fast of Ramadhan will be counted as a whole year fast.
You can fast consecutively or at intervals during the month of ShawwalI only wish your prayers are accepted and your troubles and those of the whole creation are minimal
Allah Yebarik
Wakatabahu
Mdau
Jazzaka llahu khayra. Kama alivyotufundisha mtume Muhammad Sallalahu alayhi wasallam, kuma tukatazane mabaya na tukumbushane mema, Allah subhaanahu wa taala akulipe kwa hili.
ReplyDeleteAmeeen.
huna haja ya kuomba msamaha ndg yangu sisi sote watz ndugu. hata mimi hufunga baadhi ya siku kuwaunga mkono ndg zangu waislam maana we are 1 people.
ReplyDeletewalah umeanza vizuri lakini una tuchanganya kilugha katikati sisi itabidi tufungue kamusi ili tupate ujumbe wako -shukran
ReplyDeleteAllah ibarik to you too. Mungu atupe siha njema na atuepushe na maradhi, tuipate Ramadhan kareem na Shawwal inshaAllah. Nawatakia nyote Ramadhan Njema, Allah atujenge katika kumuabudu, atuepushe na machafu katika maisha yetu yote inshaAllah. Funga hutufanya tuwe wacha mungu na hili ni la kuzingatia sana(2:183)
ReplyDeleteSheikh Michuzi ikiwa umeamua kutoa nasaha za dini basi tafuta watu wenye elimu na wanye kuijua kazi yao, kila jambo lina utaalamu wake na taratibu zake.
ReplyDeleteJazak a.k tunashukuru sana ndigu kwa kutukumbusha, na katika kukumbushana juu ya jambo lililo jema hapahitajiki utaalam umesikia anon wa 07.33
ReplyDeleteMdau ujumbe huu ulivyoutoa unaendana kabisa na Utanzania wetu. Mimi sio Mwislamu lakini nawatakieni heri ndugu zangu Waislamu katika kutekeleza imani yenu. Tuonane Eid el Fitri.
ReplyDeletewatu wengine bwana! sijui wanaufahamu mfupi kiasi gani? mfano ni huyu mtowa maoni wa Wed Jul 22, 07:33:00 PM. hivi wewe unadhani kila post itokayo hapa imeandikwa na michuzi? watu wanamtumia post michuzi na ni uamuzi wa michuzi kuziweka au kuzitia pakachani.
ReplyDeleteNasaha nzuri ila ndugu hii ni copy and paste, si angalau basi ungelijaribu kuibadilisha kidogo angalau kwa kuitafsiri? ha ha ha ha ha ha!!!
ReplyDeleteHili ndio tatizo la mtandao, huwezi kujichukulia cha mtu na kukifanya chako kuna watakaogundua kuwa wameshaona hayo hayo sehemu nyengine.
Mdau,
ReplyDeleteJazakallahi hairan!
Asante kwa kutukumbusha kwamba mgeni yuko njiani na manegine.
Mungu akubariki.
Amin
Na kwa mdau unayefunga siku moja nakupa hongera kwa jitihada zako, keep it up.Funga husaidia sana kuboresha afya yako ya kimwili na kiroho.
ASSALAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAQATU.
ReplyDeleteNI WAZO ZURI SANA KUTUKUMBUSHA JUU YA MWEZI MTUKUFU RAMADHANIL QAREEM. KITU CHA MSINGI NI KUWA SIO TU TUFOCUS IBADA ZETU KATIKA RAMADHANI BALI INATUBIDI TUJIANDAE TOKA SASA, NI VYEMA KWA KILA MTARAJI MEMA SIKU YA KIAMA AKAANZA KUFUNGA KTK MWEZI TULIONAO WA SHABAAN WALAU KWA KILA JUMATATU NA ALHAMIS (ISHALLAH), TUFANYE IBADA SANA, WALE WAZEE WA KUGONGA MTUNGI PAMOJA NA MAOVU MENGINE NI BUSARA SANA WAKATULIA KIPINDI HIKI, TUKATOA SADAKA KWA WINGI PAMOJA NA KUJIKITA KTK KUTEKELEZA MEMA MENGINE NA KUACHA YALE YANAYOMCHUKIZA MUNGU, NA ISHALLAH MUUMBA WETU ATATUSAMEHE MADHAMBI YETU YALOPITA NA YA JAO, TULIYOYAFANYA KWA BAHATI MBAYA NA KWA MAKUSUDI MANA YEYE MUNGU AMETUHAKIKISHIA KUWA YEYETO ATAKAYE MUOMBA MAGHFIRA ATAMSAMEHE.
ISHALLAH TUJIBIDIISHE BASI.
MAASALAM,
MWANNAZANZIBAR.
Ramadhan kareem. Nimefarijika na ndugu waliopost comments zao za kuungana nasi au kututakia heri katika kutimiza ibada hii muhimu. Mungu atujaalie hii harmony iambukize kila mtu. Watanzania wote tukiweza kuvumiliana na kuheshimu dini za wengine kweli itakuwa heri.
ReplyDeleteAssalaam Alaykum Jamia,
ReplyDeleteShukran kwa ujumbe mzuri toka kwa mjumbe wa kwanza pamoja na wachangiaji.
ninachotaka kuengezea ni kuhusu manufaa/madhumuni ya Ramadhani.Jamani mwezi huu ni darasa la kutufundisha kuacha tabia mbaya. tutafanya mazoezi ya kujizuia kutenda mambo mengi yasiyo na faida kwa mwezi mzima (Mfano;matusi, kusengenya,uongo,zinaa,ulevi nk) INSHAALLAH BASI IWE MWANZO WA KUYAACHA MOJA KWA MOJA.
Wabillah Tawfiq.
Kyk.
Assalaam Alaykum Jamia,
ReplyDeleteShukran kwa ujumbe mzuri toka kwa mjumbe wa kwanza pamoja na wachangiaji.
ninachotaka kuengezea ni kuhusu manufaa/madhumuni ya Ramadhani.Jamani mwezi huu ni darasa la kutufundisha kuacha tabia mbaya. tutafanya mazoezi ya kujizuia kutenda mambo mengi yasiyo na faida kwa mwezi mzima (Mfano;matusi, kusengenya,uongo,zinaa,ulevi nk) INSHAALLAH BASI IWE MWANZO WA KUYAACHA MOJA KWA MOJA.
Wabillah Tawfiq.
Kyk.
Nakushukuru sana Mja wa Allah kwa kutukumbsha, Insh-Allah tutafunga.
ReplyDeleteNawatakia kila la kheli ya mfungo wa, Ramadhani ndugu zangu wote, mfungo mwema
ReplyDeleteinshallah tunamuomba mola atuwafikishe kufanya mema na kuacha mabaya, uwe mwezi wa kuvuna kheri na kupata mafanikio kwa Allah Subhana Wataala, Tunashkuru kwa kutukumbusha wajibu wetu.
ReplyDeleteNawatakia waislam wote Ramadhan Kareem, waliotangulia mbele ya haki Mola awasameh makosa yao.
Ameen.
Nielewesheni jamani, wakati wa ramadhani itakuwa sawa kupost na kushiriki mambo ya anasa kama 'the sexiest man in Tz', nk? Je baada ya Ramadhani? Mimi naona waumini wanaomcha Mungu wanatakiwa kufuata mafundisho yake mwaka mzima!
ReplyDeleteNaomba msaada kidogo kwa wadau wenye ufahamu wa hili jambo.Kwa sasa sehem nyingi Marekani jua linachelewa kuzama,inafika mpaka saa 3 usiku lakini bado kweupe.Je kuna namna ya kupata muda wa kufungulia au inabidi kusubiri mpaka jua linapozama??naomba msaada wenu wadau..
ReplyDeleteAsalaam aleykum mdau wa friday 0546
ReplyDeleteHakika ni matatizo makubwa suala hili la jua kugoma kutua mpaka usiku mwingi. Nafikiri hapana jibu rahisi bora zungumza na mashekhe walio kwenye misikiti yenu.Jana hapa UK baadhi yetu tulifunga kwa kuwa ni siku ya mwisho ya mwezi Rajjab na pia ni alhamisi, magharib ilikuwa saa tatu na dakika ishirini na moja usiku. Yote ni rehma zake Subhana.
Wakatabahu
Mimi si muislamu ila nafahamu kwamba kama jua likizama ndipo unaweza ku-break the fast. So mdau, kama likizama saa tatu utakula saa 3. Ramadhan karim
ReplyDeleteEwe mheshimiwa wa Jul 02.14 PM
ReplyDeleteWasema hakuna ku-break the fast mpaka jua likizama, jee unafahamu kuwa within the arctic circle around June 21st jua halizami abadan kwa masaa ishirini na nne. Part of extreme USA Canada etc are within the circle
Wakatabahu
Assalaam Aleykum mdau was friday 0546 ukienda kwenye islamicfinder.org unaweza kupata muda wa kufungulia na pia ratiba ya swala zote.Natumaini hii itakusaidia. Assalaam Aleykum.
ReplyDelete